Kaka;
Naomba kutofautiana na wengi ka sio wote waliokushauri. Kwanza pole zangu kibao kwako kwa yalokupata. Pili, elewa kuwa hakuna mwanamume mwenye uwezo wa kusema wazi kuwa watoto hawa ni wangu. Tumefika pahala pa kusema; Kitanda hakizai kharam!! Upo hapo?? Maudhi huja pale mama mnakorofishana anakuambia; Usimgombeze mtoto wangu huyu, hujui nilivyo mpata miye. Ndo unaanza kuwaza, moja na moja ikawa 10.
Nakuomba, angalia maelewano yako na mkeo. Amekuvumilia muda mrefu saana tu kuhusu mtoto uliyeshindwa kumpatia. Sasa akafika pahala akaamua kujaribu nje ya ua. Akafanikiwa, sasa amerudi home na kukuambia mtoto mtarajiwa ni wako. Swali la kujiuliza, Je, unayo nguvu ya kufyamba?? Kama huna nguvu, vumilia ila mwombe kuwa, akizaliwa awe ndo wa mwisho kwenu. Mtakuwa mnahesabiwa kuwa mlizaaga mtoto mmoja. Ng'oa kizazi chake kabisa kabisa. Akubali hivyo kinyume na hapo atakuletea tena mwingine. Umeshajua wazi kuwa huna uwezo wa kumfyamba sasa ya nini kuendeleza ukoo usio wako??
Pili, akizaliwa mtoto, aandikwe jina lako, tuone ka atajitokeza kidume kuja kusema ni wake. Mambo haya yanahitaji uvumilivu kwani wewe unajua wazi kuwa huna nguvu ya kuleta kiumbe duniani. Sasa, kuficha aibu, pokea huyo mmoja tu na asije tena mwingine. Huyo mama akitaka kuendeleza kwa nguvu, jua hana jema na weye. Na uhusiano na jamaa yake akuhakikishie utakoma kabisa.