Mimi ni mtumiaji mkuu wa Jeep; nina Grand Cherokee na binti yangu nilimnunulia Patriot. Ni magari mazuri sana yenye stability nzuri sana kwenye barabara. Ila baadhi ya sifa zake mbaya ni kama ifuatavyo hapa chini, ikiwa wewe siyo fundi yanaweza kuwa kero hasa yakishafikisha umri kama miaka 6 hivi au kutembea kama km 100,000: (a) Yanakula mafuta sana, (b) Suspension system yake siyo confortable barabarani; ni kama yametengezwa kwa ajili ya matumizi ya offroad zaidi ya barabarani. (c) Yana tabia ya kuchoma oil na kusababisha oil kupunguka haraka sana; usipokuwa makini unaweza siku moja kujikuta unaendesha bila oil. (d) Kukiwa na tatizo, matengezo yake yanaweza kukulazimisha kushusha injini zima kwa vile hayana nafasi ya kutosha mtu kufanya matengezo wakati injini imefungwa, (e) yana tabia ya kumisfire bila sababu yoyote hasa wakati wa baridi.