kifo kinatisha, hasa kama huna uhakika kama una Mungu, hivo ukifa unaenda moja kwa moja motoni. pia watu wengi wanaogopa ukimwi na maradhi mengine, ni sahihi, ila hawamwogopi Mungu, ukimwi unaua mwili, hauuwi mwili pamoja na roho, ila Mungu ndiye awezaye kuua sio mwili tu bali na roho yako katika moto wa milele. Mwogopeni Mungu, ukimheshimu Mungu hautamfanyia dhambi ya uzinzi hivyo utapona na mengi. Jahenum inatisha, mrudieni Mungu, uwe umepata ukimwi au bado, mwogope Mungu, mheshimu yeye, tengeneza mambo yako na Mungu kabla giza halijaja kwako, kwa sababu hatujui siku wala saa aidha tutakayokufa au tutakayokunana na unyakuo wa Yesu, nawaasa, mpeni Yesu maisha yenu, muokoke ili muwe na uhakika wa maisha ya sasa na ya baadaye.
tutatangatanga katika dhambi hadi lini? tutazini hadi lini? tangu tuanze kuzini tumevuna mangapi? Mungu anatuona, tutamdharau Mungu hadi lini? hivi unajua kila unachokifanya Mungu anakuona? hata wewe uliyekuwa umeokoka ukaacha wokovu, maadamu upo hai,ni nafasi Mungu amekupa, rudi haraka kwa Mungu, mheshimu Mungu, bado anakupenda mno na anataka ubadilike. Wokovu ni wa bure, Yesu alilipa deni lako, ni wewe tu kuamua kuupokea wokovu wake au kuendelea kubaki katika dhambi, mpe Yesu Maisha yako, alikufa kwa ajili ya hayo yote unayopitia, atakuokoa, atakuponya, atakukomboa na utapata raha nafsini mwako.