Ndugu zangu wakenya acheni kuharibu nchi yenu

zandrano

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Posts
7,893
Reaction score
8,816
kinacho endelea kwa jirani zetu wakenya sio maandamano ya amani bali ni vurugu ambazo hadi sasa zimepelekea watu sita kupoteza maisha na kusababisha uharibifu wa mali.

Wananchi wanayo haki ya kuandamana lakini tunacho kishuhudia kwa jirani zetu ni vurugu tupu ambazo zinapekea kutatiza shughuli za kiuchumi.

Mzee Raila chonde chonde usiingize Kenya kwenye machafuko, tumieni njia za amani kudai haki zenu, vurugu hazisaidii zaidi ya kusababisha mauaji.
 
watumie njia zingine kama vile Bunge n.k, maandamano ya vurugu ni machafuko mkubwa sio njia sahihi, sio njia muafaka kwa sasa.

watu 6 wamepoteza uhai. ni wazi kabisa maandamano sio njia sahihi kwa wakati huu.
 
kinacho endelea kwa jirani zetu wakenya sio maandamano ya amani bali ni vurugu ambazo hadi sasa zimepelekea watu wawili kupoteza maisha na kusababisha uharibifu wa mali.

Wananchi wanayo haki ya kuandamana lakini tunacho kishuhudia kwa jirani zetu ni vurugu tupu ambazo zinapekea kutatiza shughuli za kiuchumi.

Mzee Raila chonde chonde usiingize Kenya kwenye machafuko, tumieni njia za amani kudai haki zenu, vurugu hazisaidii zaidi ya kusababisha mauaji.
Wewe bwege nchi yako CCM wanaiuza kwa waarabu umekaa kimya then unashadadia mambo ya wakenya
 
watumie njia zingine kama vile Bunge n.k, maandamano ya vurugu ni machafuko mkubwa sio njia sahihi, sio njia muafaka kwa sasa.

watu 6 wamepoteza uhai. ni wazi kabisa maandamano sio njia sahihi kwa wakati huu.
Wamepoteza maisha kwa kuandamana au wameuliwa???....
 
kwasababu ya vurugu za maandamano.
chanzo ni maandamano.

kiongozi aliye hamasisha maandamano yasiyo na kibali cha polosi ndiye anapaswa kuwajibishwa kwa vifo hivyo.
 
Maandamano sio vurugu mkuu...
Tafuta vizuri maana yake.
 
Wewe bwege nchi yako CCM wanaiuza kwa waarabu umekaa kimya then unashadadia mambo ya wakenya
Kenya ni jirani zetu ni ndugu zetu, wakifa wakenya lazima tuumie, huo ndio udugu wa kweli sio kushdadia.
hapa nazungumza ukweli, weka ushabiki wa vyama kando
 
Kwahiyo walitangaza kupora mali zz watu?
kama wangeandamana kwa amani bila kufanya vurugu, kuvunja na kuchoma moto barabarani na kurusha mawe na vyuma askari wasinge tumia risasi.
kumbuka panapo kuwa na vurugu lolote laweza tokea.
tuache maandamano ya vurugu, tumieni njia sahihi kudai haki kwa amani na utulivu.
 
Kama zipi? Kama wanataka kuandamana kwa amani wanakataliwa!!
Nchi za dunia ya tatu hizi......
 
huo ujeuri na ukorofi ndio unawaponza.
lazima kujifunza kufuata taratibu zilizopo, toa taarifa kwa Polisi mkiambiwa mandamano Mjini Nairobi haiwezekani kwasababu za kiusalama na kiuchumi mnapaswa muelewe na mtii.
 
Nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara haziruhusu maandamano!!!!
Labda ya kupigia makofi viongozi.
 
Back
Top Bottom