Ndugu zetu wahindi...kina Kanjibhai

Ndugu zetu wahindi...kina Kanjibhai

nzalendo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
12,106
Reaction score
12,916
Zamani tulipokuwa vijana wahindi wengi sana walikuwa wanafanya kazi Bank...hata humu NBC kabla haijavunjwa na kuzaa NMB wahindi walikuwa kibao...kuanzia miaka ile ya 60 mpaka sabini mwishoni wakaanza kupungua...wengi wanafanya biashara zao na wengine walikimbilia CANADA..
uzi tayari..... 🙂 😀 🙂 😀🙂😀
 
Amir Jamal alifia Canada, huyu muhindi Nyerere ndiyo alimpa fuko la hela ( waziri wa Fedha), na alizikwapua hasa, na akawa anatumika kuficha minoti ya wakubwa zake ughaibuni, alivyoaga dunia siri-kali walitaka kuurudisha mwili Tanganyika, wakaambiwa na watoto wa marehemu baba yao siyo raia wa Tanzania, alishaukana kitambooo....
 
Baada ya azimio la Arusha Nyerere alitaifisha nyumba zao na kuanzisha NHC. Wahindi wakajikuta ni wapangaji kwenye nyumba zao, hadi leo wahindi hawana hamu ya kujenga au kumiliki nyumba Bongo.
Nyumba zilizotaifishwa zilikuwa chini ya MSAJILI WA MAJUMBA. NHC ilikuwepo kabla ya utaifishwaji. Miaka ya 90 I guess MSAJILI WA MAJUMBA ilivunjwa na nyumba zake kukabidhiwa kwa NHC.
 
Kuna Kitabu kiliwekwa humu Wahindi walitimuliwa Uganda na Nduli ,walikuwa na maviwanda na biashara za mahoteli wakaenda zao Canada wakarudi tena Uganda wakatajirika mara 10 zaidi miswahili inashangaa shangaa tuu.1922 Bukene -Tabora tayari kuna muhindi alikuwa na duka la kuuza mafuta ya taa na ndio raia wa kwanza kuleta gari na kufanya biashara ya magari kanda ya Magharibi yote.
Majamaa kinachoyabeba wanajituma sana na wana family support system .Sisi tunapwaya kwenye hayo.
 
Amir Jamal alifia Canada, huyu muhindi Nyerere ndiyo alimpa fuko la hela ( waziri wa Fedha), na alizikwapua hasa, na akawa anatumika kuficha minoti ya wakubwa zake ughaibuni, alivyoaga dunia siri-kali walitaka kuurudisha mwili Tanganyika, wakaambiwa na watoto wa marehemu baba yao siyo raia wa Tanzania, alishaukana kitambooo....
hivi wewe unamjua amir jamal au unakurupuka tu kusema,unajua mchango wake kwa ujenzi wa nchi hii?
 
Seems walipiga sana pesa! Shamba la bibi tangu enzi!
Unawakumbuka wale Mamuu studio?..walikuwa pale Kariakoo! Walikuwa wanarekodi nyimbo za wasanii mbalimbali na kutengeneza makava ya kanda!, msaniii anaacha master tape!, kwa ujira kiduchu jamaa wanafyatua idadi kubwa na kupiga mahela, kipindi kile muziki wa Congo upo juu sana, wanatengeneza kava jipya yaani kama katoa new Album, humo ndani wanachanganya nyimbo mbalimbali za zamani, mzigo unaenda Zambia na Zimbabwe, hapo sasa ndiyo walizipig hasa...
 
Akili mkuu
 
Kuna Kitabu kiliwekwa humu Wahindi walitimuliwa Uganda na Nduli ,walikuwa na maviwanda na biashara za mahoteli wakaenda zao Canada wakarudi tena Uganda wakatajirika mara 10 zaidi miswahili inashangaa shangaa tuu.1922 Bukene -Tabora tayari kuna muhindi alikuwa na duka la kuuza mafuta ya taa na ndio raia wa kwanza kuleta gari na kufanya biashara ya magari kanda ya Magharibi yote.
Majamaa kinachoyabeba wanajituma sana na wana family support system .Sisi tunapwaya kwenye hayo.
Hapo kwenye family support system.....wapo vizuri sana.....ni kwa vizazi na vizazi.....
Kuna muhindi anaitwa Panjwan wao kazi yao ni kutengeneza pipi..
kwa sasa ni kizazi cha 6 wanatengeneza pipi....toka enzi za lawalawa.....hata wakienda shule wakawa madaktari.....pipi hawaachi kutengeneza.....kuna siri hapo.....
 
Muhindi ana uwezo wa kumwambia mwanae siri kuu ya utajiri wake (hata kama aliiba, aliua , magendo au kuzindika) atamwambia yote mwanae na namna ya kuzilinda..

Ila Mbongo hawezi , siri ya utajiri wake atabaki nayo moyoni na ndio maana akifa na mali hupotea
Waswahili kila siku tuna anzisha kitu kipya.....wenzetu wanarithi na kuendeleza.....
Kwa mfano Iringa kuna Thakor....inatamkwa (TAKO) Babu alianzisha kimgahawa na pia kukamua mafuta hapo nyumbani....mtoto akafunga mitambo mikubwa kiasi hapohapo nyumbani kukamua mafuta ya alizeti ni pale karibu na saba saba Iringa.....baadae wakahamia kule Ipogolo na Kiwanda kikawa kikubwa zaidi kwa sasa nadhani aliyepo ni mjukuu...wanajiita IVORI.........
 
Back
Top Bottom