sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Tangu uwanja wa Mkapa ulipoanza kutumika Simba imekuwa ikipata matokeo mabaya, Al Ahly waliokuwa hawatoki salama kwa Mkapa walitoa sare, Yanga imejipigia zake 5,
Leo hii umetumika uwanja wa uhuru lakini bado hili sio suluhisho.
Kipindi cha marekebisho ya uwanja, Yanga waliwazidi kete Simba wakapenyeza wataalam wao wa kamati za ufundi kuzuga ni vibarua kwenda kuharibu miundombinu ya ndumba za Simba, Shughuli nzito zaidi ilikuwa ni kuitoa Ndumba mama ya simbailiyokuwa imesakafiwa kwa zege zito sambamba na ulinzi wa majini,
shughuli ya kuitoa ndumba kuu ilihitaji wiki nzima, Kwanza kabisa ni visomo vingi sana na kafara za kuyapooza majini yanayolinda ndumba kuu, kisha baada ya hapo ndio magreda ya kutindua zege yanatumika, ni shughuli nzito sana zaidi ya kungoa visiki ndio maana zoezi hili lilifanyika kwenye marekebisho.
Ndumba mama ni roho ya ndumba zingine, bila ndumba mama ya Simba inakuwa ngumu ndumba zingine kufanya kazi kama zile za wachezaji kuvaa viunoni, wachezaji kutumwa kumwaga dawa kabla ya mechi, n.k.
Kilichofanyika ni kuifukua ndumba mama na kuichoma na kisha kuweka ndumba ya kuzuia nguvu za ndumba za Simba, Ndumba iliyowekwa kwa sasa inafika mpaka uwanja wa uhuru , ni sawa na ukipitisha sumaku karibu na chuma, Ndumba hii pia inaweza kutumika kama rimoti kutia mikosi kwenye mechi za Simba hata za uwanja wa karibu, mipira kugonga mwamba, wachezaji kupata majeruhi, kujisahau, n.k.