NE-YO kutua nchini Tanzania; Kufanya Tamasha Mwanza, Mei 21

NE-YO kutua nchini Tanzania; Kufanya Tamasha Mwanza, Mei 21

neyo-1024x627.jpg


Mwanamuziki nguli kutoka nchini Marekani NE-YO ambaye amekuwa akitamba kwa muziki ya mahadhi laini, anatarajiwa kuwasili nchini Mei 19 kwa mwaliko wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Jembe Media Limited.

Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 36 Mmarekani mwenye asili ya Kiafrika, anatarajiwa kufanya onyesho mei 21 jijini Mwanza kwenye uwanja wa CCM kirumba kwenye tamasha lililopewa jina la JEMBEKA NA VODACOM 2016.

Kwa mujibu wa waratibu wa Tamasha hilo, NE_YO pia anatarajiwa kushiriki kwenye shughuli za kusaidia jamii kupitia taasisi ya Vodacom.

Source: Channel ten
nasikiaga nae ni mmojawao wa wapigania haki za binadamu za kimarekani
 
Hii ndo bongo bhn!!!! Wakat msanii fulani anasema kafanya collabo na ne-yo tulishangilia na kutabir itakua hit song but leo tunaskia atakuja kirumba jukwaa moja na msanii fulani twasema KACHUJAAAAAAAAAAAA na TUNAOMBA HIYO SIKU ISIFIKE...........
""HAKA KAMCHEZO HAKAITAJI HASIRA""
Hivi mkuu wewe uko wapi ........ hii show atapanda jukwaani na huyo msanii aliyefanya nae collabo( DIAMOND) na ukichunguza kwa mbaaaaaaaaaali hawa wanaosema hivi ni wale wenye vinasaba vya "roho mbaya na chuki iliyopitiliza KWA DIAMOND sio NE-YO" Lakini wajue tu kuwa wataona mrejesho ( mipicha picha kibao) hapa hapa jinsi shoo itakavyojaza watu, na hapa tunavyoongea maana yake hao wasanii wameshachukua 50% ya hiyo shoo na siku ya shoo kabla hajaenda jukwaani inamaliziwa salio lililobaki kwahiyo wewe ukiongea hivi TAYARI PESA WATU WAMESHAINGIZIWA KWENYE ACC WEWE HATA UKIONGEA HIVI HUPUNGUZI KITU.
 
Uncle wa tembo amesahaulika kabisa. Lakini uncle pori anajishusha mwenyewe kwa kukosa ubunifu na kuwa na mgt dhaifu.
 
NEYO KASHACHUJA.... WAMLETE DRAKE.. AU MEEK MILLI
 
Baby hebu panga ratiba zako vizuri tuibukie Mwanza hiyo tarehe.
[emoji133] [emoji133] [emoji133] [emoji133] woyoooooo afadhali mchepuko wangu yule muuza vifuniko vya asali kisha habari yake
 
[emoji22] [emoji22] [emoji22] beiby umenipotea mwenzako hadi nashawishika huku
Teh teh..Usishawishike..Kuna mazuri mengi yanakuja..Kuwa na imani mtoto mzuri..Sawa
 
Bora wangemleta Busy Signal

Busy Signal - Nightshift / One More Night


Busy Signal - Come Over (Missing You) HD Official Video
 
Back
Top Bottom