Nebukadneza: Mbabe wa vita, muabudu sanamu aliyekula majani kama ng’ombe

Hiyo sehemu inaitwa Israel Kipindi cha Yesu iliitwa jina gn?
 
Sasa najiuliza tu. Kama Waisrael hawa si wale, kwamba hawapo tena, hawa ambao Biblia imewaandika wote watarudi, ni akina nani? I don’t know.
Hapo Waisraeli wanaozungumziwa ni wale waliojuwa mateka Babiloni chini ya utawala ya Nebukadneza

Mungu aliwaahidi kuwa watarudi nchini kwao Israeli kwenda kuanza maisha mapya na kujenga upya Yerusalemu baada ya miaka 70 ya utekwani Babiloni
 
Sasa jamani mnapoona Israel anapigana vita na kuua watoto na wanawake, hakuanza leo, ilikuwa tangu miaka hiyo ya nyuma, ni vita ambayo walizoea kupigana, hakushangai kwenye Biblia, tunakuja kushangaa sasa hivi.
Tofauti na vita ya sasa kipindi kile walikuwa wanapigana chini ya kibali cha Mungu sasa hivi hawana baraka zake ni Shetani tu ndiye anayewapelekesha waue hadi watoto wasio na hatia
 
Alikubali Mungu gani mkuu? Maana Mungu wa Wayahudi wala sio Mungu unamuamini wewe Mkristo. Tazama njia zenu za kumfikia huyo Mungu mnavyotafautiana pakubwa.
Mungu ninayemuamini mimi Mkristu ni Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Mungu aliyegawanya bahari ya Shamu waisrael wakapita Mungu aliyenena kwa Kinywa cha Nabii Isaya kwamba fimbo ya chuma itainuka katika kabila la Yuda atakayetawala milele!
 
Unajitahi kuelezea vizuri. Naaamini baada ya hapo utasogea mbele zaidi ya Daniel 4 uende hadi Daniel 12.

Nikupe Nyongeza kidogo ili ubaki njia kuu.

1. Babilon ndio nchi ya Iraq kwa sasa.
2. Nebkadneza ndio aliuhurusuru/ Aliuteka Yuda na kuwachukua hao vijana -
3. Nebkadneza ndio alichukua vyombo vya hekalu.
4. Sababu ya kuuteka Yuda ni kibali toka kwa Mungu, yaani Yuda walifanya maasi na kuuwa watu wengi sana, ndio Mungu akampa maelekezo Nebakneza kuuteka huo mji ili kuponya watu wake. Kiufupi Nebkadneza alimpendeza Mungu kwenye utawala wake. Hadi alipokuja kumkosea Mungu hapo badae.
 
Jina la mfalme wa Babylonia ambaye alitawala katika karne ya 6 KK ni Nebukadneza.

Hilo jina Nebukadreza labda ni kutokana na kukosea matamshi tu
Siyo makosa ya kimatamshi ila huyo, nimetoka kusoma hapa Wikipedia anaelezwa kuwa alikuwa mfalme bora sana wa babeli katika karne ya 6 KK.

So nazani ni watu wawili tofauti 🤒😎
 
Hapo Waisraeli wanaozungumziwa ni wale waliojuwa mateka Babiloni chini ya utawala ya Nebukadneza

Mungu aliwaahidi kuwa watarudi nchini kwao Israeli kwenda kuanza maisha mapya na kujenga upya Yerusalemu baada ya miaka 70 ya utekwani Babiloni
Jamani eeeh kama aliwaahidi watarudi kwao lakini kipindi hicho Israel ilijulikana kama koo tu sio kwamba ilikuwa sehemu fulani inaitwa Israel, hakuna sehemu iliyokuwa inaitwa Israel na ndiyo maana ata Abraham hakuambiwa aende Israel ila Canaani akitoka Hulu yawakalidayo.

Jina Israel limekuja kuchomekwa kwenye version mpya hizi kama mnavyoambiwa leo kuwa Musa ni (Moses) wakati Wayahudi wenyewe wanaitwa (Moshe) sasa jiulizeni hizi pronounce zenu zimetoka wapi ilihali mnaambiwa manabii hawa ni wayahudi?
 
Ilikuwepo na mipaka ilikuwepo mjii wao mkuu uliitwa Yuda
 
Ukiendelea naomba uni-tag
 
Hivi miaka hiyo wahaya mlikuwepo?
 
Kijana usipotoshe, hakuna sehemu Mungu alipowaagiza Waisraeli kukata miti yote kwenye nchi ya adui wakati wa vita.
Ukisoma kumbukumbu la torati 20:19 Mungu anawakataza Waisraeli kukata miti wakati wa vita.
Ni vyema kuchuja maneno kwa umakini na kuzingatia ukweli pale unapotaka kumhusisha Mungu katika madai yoyote.
 
Jina la Israel limetokana na Yakobo kwahiyo kabla ya Yakobo hilo jina halikuwepo.
Waisraeli walipotoka utumwani Misri waliingia nchi ya Kanaani na kuanzisha Taifa la Israeli ambalo mipaka yake ilipangwa na Mungu mwenyewe, Kutoka 23:31
Kuhusu tofauti ya majina ya Mitume na Manabii, ni jambo la kawaida jina moja kutamkwa na kuandikwa tofauti kutoka lugha moja kwenda nyingine lakini maana inabaki vilevile.Mfano, John na Yohana, England na Uingereza.
Kama nchi ya Israel haijawahi kuwepo je Wafalme Daudi na Suleimani walitawala nchi gani.
 
Kuhusu kula majani ni lugha ya picha...
Kimsingi jamaa alikuwa anavuta bangi....ndio majani ya kondeni...
Usifikiri kila mtu hapa ni MPUMBAVU mwenzio.
Biblia imeweka wazi kuwa Nebukadneza alikula majani kama ng'ombe halafu wewe unakuja kutuletea stori za vijiweni hapa.
Jiheshimu.
 
Usifikiri kila mtu hapa ni MPUMBAVU mwenzio.
Biblia imeweka wazi kuwa Nebukadneza alikula majani kama ng'ombe halafu wewe unakuja kutuletea stori za vijiweni hapa.
Jiheshimu.
Haidhuru si kitu
Bangi ndio iliyomsaidia kuwa na busara ya kuhifadhi vyombo alivyoteka toka hakalu la Sulaiman Salalah aleeii wasalaam..tofauti na alivyofanya mwanae....
Na majani hayohayo ya kondeni(bangi)ndio iliyompa kibri na hakutaka kutubu ndani ya mwaka mmoja baada ya ile ndoto.
Na kwa nyongeza ninajiheshimu sababu ki umri mie ni baba yako au mke wa mama yako...Asante na karibu.
 
Jamiforums sihami, nimejifunza mengi na kubarikiwa na mengi, hii mada iendelèe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…