Tarehe 09.08.2022 taifa la Kenya lilifanya uchaguzi mkuu ili kupata viongozi mbalimbali wa taifa hilo.
Upigaji kura ulifanyika vizuri kwa amani kwa mujibu wa waangalizi wa Kimataifa, kwa muktadha huo naipongeza IEBC yenyewe, serikali na police wa Kenya kwa kutekeleza majukumu yao vizuri.
Jambo muhimu NEC ya Tanzania inalopaswa kujifunza kutoka IEBC ya Kenya ni kuendesha uchaguzi ulio huru na wa haki. Huko Kenya tangu mwanzo hakuna Cha mgombea kutekwa akapoteza form na hapakuwa na mgombea yeyote aliyepita bila kupingwa hili NEC walichukue.
Jambo jingine ni uwazi wakati wa kutangaza matokeo, NEC iige kuruhusu vyombo vya habari kama ilivyotokea kwa wenzetu huko Kenya, vyombo vya habari viliruhusiwa kutangaza idadi za kura alizopata mgombea wa nafasi fulani katika jimbo fulani.
Hii Itasaidia viongozi wote wenye mamlaka kuogopa kuingilia tume ya Uchaguzi kwani jamii itakuwa inajua idadi ya kura mgombea fulani alizopata katika jimbo fulani hivyo sio rahisi kuzigeuza kuzibadili kura.
Police wa Tanzania wakati wa uchaguzi wawe walinda amani na mali za watu wasigeuke kuwa wapiga kampeni wa viongozi wa Chama kilichopo madarakani.
Mwisho NEC wanapaswa wasiwe waoga wasimamie haki, aliyeshinda atangazwe na aliyeshindwa asitangazwe.