NEC igeni Mfano wa IEBC ya Kenya

Hakuna cha kuiga toka Kenya kwani Kenya wao walianza na kubadili katiba kwanza ili kujenga mazingira ya utendaji wa IEBC. Kusema kujifunza ni kupoteza wakati na hizi ni kauli za kisiasa zaidi kuliko uhalisia.
 
Waige nn? Thubutu 🤣🤣🤣🤣
 
Mkuu, wakati mada hii inaonekana kuwa na nia njema kabisa, mimi naamini unapotosha matamanio ya wengi. Sioni cha NEC kujifunza toka IEBC kwa sababu wenzetu wamepitia mchakato sahihi wa mabadiliko ya Katiba yaliyopelekea kuzaliwa kwa IEBC na hivyo hayo mazuri tunayoyaona ni matokeo ya Katiba Mpya.

Sio sahihi kujidanganya kuwa NEC kwa muundo wake inaweza kutenda haki kwani iko hivyo kwa kusudi maalum. Huwa ninashangaa ninaposikia majigambo ya kijinga eti, "wakenya wamejifunza kufanya uchaguzi kwa amani toka kwetu", ama kweli sisi tumerogwa. Hawa hawa wakenya waliopitia mateso makubwa kufika hapo walipo wana lipi la kujifunza kwetu? Ujinga?

Narudia tena, wakenya wamelipa gharama kufika hapo walipo, sisi ndio wenye jukumu la kujifunza toka kwao, jinsi gani haki inatafutwa, jinsi gani mabadiliko ya kweli yanaletwa. IEBC wamepewa nguvu ya kutenda hayo na katiba, sio HISANI kqma tulivyozoea wengine. Hatuhitaji NEC ijifunze lolote toka Kenya, tunahitaji WATANZANIA WOTE wajifunze maana ya demokrasia toka Kenya.

I rest my came
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…