Uchaguzi 2020 NEC, lugha ya uchochezi wakati wa kampeni ni ipi na dhidi ya nani?

Uchaguzi 2020 NEC, lugha ya uchochezi wakati wa kampeni ni ipi na dhidi ya nani?

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
21,741
Reaction score
26,735
Kampeni ya kutaka Rais ni aina ya uchochezi dhidi ya Rais aliyeko madarakani, huu ni wakati wagombea wengine wanawashawishi wananchi waachane na aliyeko madarakani wamchague yeye, ukifanya ushawishi huu nje ya wakati wa kampeni ni kosa la uchochezi dhidi ya serikali

NEC inaposema lugha ya uchochezi ni dhahiri kuwashawishi wananchi waachane na aliyepo madarakani kwa kushindwa kuiongoza nchi hivyo wanatakiwa wachukuliwe hatua za kisheria! Vinginevyo wagombea watumie kampeni kumsifu Rais aliyeko madarakani.

NEC hii ni ya Tanzania tu na hawezi kukubalika nchi nyingine kwa mtindo wake huu wa uchaguzi wa vyama tofauti, hasa inapotokea NEC kumlinda mgombea aliyeko madarakani.
 
Niliposikia hivyo nami nilijiuliza maswali. Mipaka ya uchochezi ni ipi? Lugha ya kampeni ni propaganda. Je propaganda ni uchochezi? Halafu adhabu yake ni kuenguliwa katika kinyanganyiro.

Je, huu si mtego kwa Lissu? Si ni kijisababu kinatafutwa? Ni wazi kuwa makatazo yote ya sheria katika uchaguzi huu yanahusu vyama vya upinzani tu. Hakuna diwani wala mbunge aliyeenguliwa hadi sasa. Ni wapinzani tu.

Jiwe amevunja sheria waziwazi za uchaguzi na amelalamikiwa lakini wala hajaitwa kwenye kamati. Hakuna wa ccm anayevunja sheria ila upinzani tu. Utasikia Lissu akiengeliwa. Subiri.
 
NEC yenyewe yote imeteuliwa na mgombea wa CCM na hao Wateule wote ni makada Waaminifu wa CCM! halafu Wapinzani bado wanategemea kutendewa haki!

Bora mimi niliyeamua kutoshiriki kwenye haya maigizo yanayoitwa UCHAGUZI chini ya huyu Rais wa sasa asiyependa kusikia masikioni mwake kitu kinachoitwa Demokrasia au mfumo wa vyama vingi.
 
Babu madevu ......
Huyu mwanamke msimchague ni malaya...

Hizi kauli zingetolewa na upinzani NEC ingetoa adhabu lkn kwa kuwa ni CCM kauli hizi zimejaa ustaarabu.
 
Kwenye kampeni za siasa huo si uchochezi kwani unamlenga mpinzani wako akiwa ni mgombea si rais.
Tatizo la hii nchi huwa unagombea na MTU ambae anakuwa anamamlaka yote hivyo akiona unataka kumfikia anakuundia zengwe ili usifanikiwe
 
Lugha ya uchochezi ni kama ile aliyoitumia bwana mmoja aliposema wapinzani wakipewa nchi watavunja vunja madaraja wakauze scraper
 
NEC hii ni ya Tanzania tu na hawezi kukubalika nchi nyingine kwa mtindo wake huu wa uchaguzi wa vyama tofauti, hasa inapotokea NEC kumlinda mgombea aliyeko madarakani.
Uchochezi ni kuipinga ccm
 
Back
Top Bottom