NEC na ZEC ni Tume Huru kwa mujibu wa Sheria, nongwa inatoka wapi?

NEC na ZEC ni Tume Huru kwa mujibu wa Sheria, nongwa inatoka wapi?

Deogratias Mutungi

Senior Member
Joined
Oct 1, 2019
Posts
140
Reaction score
181
NEC NA ZEC NI TUME HURU KWA MUJIBU WA SHERIA, NONGWA INATOKA WAPI?

Deogratias Mutungi

Uchaguzi wa kisiasa lazima uwe huru, na ni mtamu unapokuwa huru, maana unapokuwa huru unogesha demokrasia na mifumo yake, raha ya uchaguzi kisiasa ni kuwa huru, demokrasia ustawi na kunoga kisiasa endapo tu haki itatamalaki wakati wa kupiga kura, haki ya kura ujenga imani, usawa na amani kwa viongozi wateule ndani ya jamii na nje ya mipaka yake, dhambi ya kupora haki haipimiki wala kulinganishwa na chochote kile hapa ulimwenguni, bakora ya mpola haki kutoka kwa Mungu ni chungu sana na kamwe uwezi kuifananisha na uchungu wowote ule katika uso huu wa dunia.

Siasa na falsafa ya uaminifu kwa kiongozi ndani ya jamii inayomzunguka upimwa kwa mizania ya upatikanaji wake, aidha heshima ya kiongozi ni tunu inayojitambulisha kutokana na uhalali wake kwenye sanduku la kura, kura na haki ni moyo wa kisiasa wenye mapigo na mishipa inayosambaza amani ndani ya jamii ya watanzania, Mapigo ya moyo wa siasa yakikosa haki bin kura ni chanzo cha maelewano mabovu ndani ya nchi yanayoweza kupelekea uhasama wa kisiasa ikiwa ni pamoja na machafuko ya ndani kwa ndani “ Political Chaos”

Kwa sasa tupo kwenye kipindi cha uchaguzi wa kuwapata viongozi watakao tuongoza miaka mitano kwa maana ya Rais, Wabunge na Madiwani, nyakati hizi zipo fununu zinajengewa hoja hasi juu ya tume hizi mbili yaani NEC “National Electoral Commission” Kwa maana ya Tanzania bara na ZEC “Zanzibar Electoral Commission” Kwa maana ya Zanzibar, Bila shaka fununu hizi ni sehemu ya nongwa za kisiasa ambazo pengine uwa ni kawaida kwa mataifa yenye kufuata mkondo wa mifumo ya vyama vingi.

Hatahivyo ni dhambi kukaa kimia dhidi ya fununu hizi, Japo historia ya siasa inasomeka na kuonyesha kuwa nongwa hizi zimetamalaki zaidi Afrika na viunga vyake na kwa uchache bara la Asia, Sababu kuu ya nongwa ikiwa ni vyama vya siasa kutoamini mifumo rasmi ya vyombo vya utoaji haki mathalani tume zao za uchaguzi licha ya vyombo hivi kuwepo kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni za nchi lakini bado kuaminiana imeonekana kuwa tatizo kubwa kwa wanasiasa wenye mrengo wa upinzani.

Makala haya yanatambua uwepo wa hoja zenye mrengo tofauti zinazojengwa na baadhi ya wadau na wanasiasa juu ya tume katika dhana ya utoaji haki kwa nukta ya upendeleo, hatuwezi kubeza hoja zao isipokuwa tu kuzijibu hoja hizo kwa hoja, Japo dhana ya upendeleo kwao inazungumziwa katika muktadha wa jazba na hamaki tele pasipo na mantiki halisi inayotambulisha takwa lao, Je hoja hii ni sahihi? na kama si sahihi kusudio lake ni nini hasa?

Je ni upotoshaji kisiasa au ni nongwa tu za kisiasa ili kupata huruma ya wananchi, Je ni kweli tume inakengeuka au wanao hoji ndio wanaokengeuka kwa sababu hawajui mamlaka na sheria zinazoiongoza tume au wanajua tu ila wanapotosha mantiki ya uwepo wa tume ya uchaguzi kwa sababu za kisiasa tu, maswali ni mengi na yanafikrisha.

Kwa muhtasari tume ya uchaguzi kwa maana ya NEC na ZEC ni vyombo vilivyopo kwa mujibu wa katiba ya nchi na sheria zake, ukirejea ibara ya 74,-(1) inataja bayana uwepo wa tume ya uchaguzi, aidha 74,-(6) inataja majukumu ya tume ya uchaguzi, rejea vifungu vidogo vya (a), (b),(c),(d) na (e) vyote hivi vina hainisha wajibu wa tume katika kusimamia uchaguzi na kutenda haki kwa wagombea wa nafasi mbalimbali za kisiasa.

Aidha ZEC kwa maana ya tume ya uchaguzi ya Zanzibar ipo kwa mujibu wa kifungu cha 119(1) cha Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1994, ikiwa sambamba na kifungu cha 4 cha sheria ya uchaguzi namba 11 ya 1984, Je hapa nongwa ni nini hasa kama tume zote hizi mbili zipo kwa mujibu wa katiba za nchi?, wasomaji wa makala haya tunahitaji kufikri chanzo cha nongwa hii dhidi ya tume ya uchaguzi kinatokana na nini.

Pengine inawezekana nongwa si neno “tume ya uchaguzi” bali tu watumishi wa tume, kama hoja ndio hii basi ni hoja nyepesi na inayojibika bila kuumiza kichwa, kama kilivyo kitendawili cha kuku na yai nani alianza kuwepo kabla ya mwenzake pengine kuna ugumu wa kutegua kitendawili hiki cha kuku na yai, lakini si kwa dhana ya watumishi wa tume.

Ni dhahiri kuwa watumishi wa tume wapo ndani ya tume ya uchaguzi ili kutenda haki na kanuni za uchaguzi zinawaelekeza hivo, ni ngumu kwa mtumishi wa tume kuikwepesha haki iliyowazi na kuutangaza uovu wake kinyume na matakwa ya tume kisheria na kikatiba, Mfano ushindi wa wazi wa asilimia 87%, 90%, 95%, au 100% kamwe hauwezi kuminywa na tume ya uchaguzi na kutangaza ushindi wa 13% 10% 5% au 1% tatizo la wanasiasa na wadau wa siasa wanaongozwa na kuishi katika “siasa za kutoaminiana na hofu iliyopitiliza”

Iko wazi kuwa nadharia ya “hofu ya haki” katika mazingira yoyote yale ni chanzo cha imani ndogo kwa Yule unayemjengea dhana hiyo, Wanasiasa wa Tanzania na wadau wa siasa hofu yao dhidi ya tume inaanzia kwenye ibara hii na vifungu vyake, ibara ya 74,-(1) “Kutakuwa na Tume ya uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao watakaoteuliwa na Rais”-(a). (b), (c) na 74,-(2) ikumbukwe kuwa hawa ni binadamu wana mapenzi yao ndani ya mifumo ya kisiasa, wanaweza kuwa wamechaguliwa na rais lakini bado wakapendelea upande mwingine usio kuwa wa chama tawala.

Aidha tunahitaji kuongozwa na dhana ya “Watumishi wa tume” katika kufikri yaani “Sapere aude” ikiwa na maana ya kutoogopa kutafakari mwenyewe na kuumiza ubongo juu ya jambo fulani. Wanasiasa wa Kiafrika utanguliza hofu ya kuporwa haki kabla ya kujenga hoja za ushawishi wa kushika dola, Mantiki ya tume ni kutoa haki na si kupora haki za wanasiasa na vyama vyao, Vyama vya siasa na wadau wa siasa waache lawama na nongwa kwa tume za uchaguzi badala yake tutambue kuwa hivi ni vyombo vilivyopo kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi.

Andiko hili linatafakari juu ya hoja inayojengwa juu ya tume kupora haki, na kuminya baadhi ya wanasiasa kifitina, tafakuri hii inakuja na jibu lenye historia na mfumo wa vyama vingi na kujiuliza mbona vyama vinavyoinyoshea kidole tume dhidi ya utendaji wake wamekuwa sehemu ya watu waliotangazwa na tume hiyo kama washindi wa nafasi zao aidha ubunge, uwakilishi au udiwani sasa nongwa ni nini hasa, bila shaka kuna jambo lililojificha juu ya agenda hii inayojengewa hoja na baadhi ya vyama vya kisiasa.

Makala haya yanatambua bayana kuwa ulimwenguni kote kisiasa tume ya uchaguzi ni chombo muhimu sana katika utoaji wa haki dhidi ya vyama vya kisiasa, aidha ni chombo muhimu chenye kubeba dhamana na mustakabari wa amani ya nchi kwa sababu tume ubeba matumaini ya watu walio wengi dhidi ya haki bin haki, kuminya haki kwa tume dhidi ya haki ya mpiga kura ni sawa na mtoto Koku kuchezea rupia karibu na tundu la choo maana kifuatacho uwa ni kilio cha kusaga meno, tume ni kichocheo cha ustawi wa demokrasia ndani ya siasa za mfumo wa vyama vingi, tume imara na yenye weledi katika maamuzi ya kiutendaji ujenga imani ya kitaasisi katika utoaji wa matokeo ya kweli ndani ya vyama vya kisiasa.

Fununu za kisiasa zinazojengwa na wadau wa kisiasa na wanasiasa wenyewe ni hasi na zinafikrisha sana dhidi ya tume zetu za uchaguzi ambazo zimetambuliwa na sheria, kanuni za nchi na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wanaojenga hoja dhidi ya tume ni Watanzania wenzetu sharti wajibiwe na mamlaka husika au na mwanahabari yoyote anayeweza kutoa “elimu hoja” dhidi ya watu hawa ili wapate kuelimika na kuondoa upotoshaji unaoendelea kwa sasa na ndilo kusudio halisi la makala haya kutoa elimu pande zote mbili wanasiasa, wadau wa siasa na wale wanaojiandaa kuingia katika ulingo wa siasa sambamba na wananchi ambao ndio wapiga kura.

Makala haya yanahitimisha uchambuzi huu uliojikita kuweka sawa uhalali wa uwepo wa tume za uchaguzi kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi kwa kusema ni vema kujenga hoja na kuziwasilisha katika muktadha wa fikra pevu zinazojenga na kulinda amani ya nchi yetu ili kuepuka nongwa isiyo na mantiki, aidha tunalojukumu la kutafakari neno kwa neno pale hoja za kisiasa zinapowasilishwa kwetu na wanasiasa, zipo hoja zinazojenga zipo hoja zenye kusudio la kubomoa, waswahili wanasema bora kujenga kuliko kubomoa, aidha ni bora kubomoa nyumba kuliko amani ya nchi maana ni ngumu kujengeka kama ilivyokuwa awali.

dmutungid@yahoo.com

0717-718619
 
1. Kwanini NEC na ZEC ziteuliwe na Rais zilipwe na Rais, na zimtangaze huyilo huyo Rais wakati wa Uchaguzi?

2 .Vipi NEC inasemaje mgombea anapoongea Lugha ya kikabira?

Tuanzie hapa tu kabla hatujaenda kwenye Engua na Mapingamizi ya Ubunge na Udiwani kwa wapinzani pekee.

Andiko lako ni refu sana umeweka ngonjera nyingi sana wakati ulikuwa na uwezo wa kulifupisha kwa kujikita kwenye hoja za msingi.

# Nashukuru hujasahau kuweka namba japo umechelewa.
NI YEYE.
 
Huu muda ulitumia kuandika ujinga unge utumia kutafuta maisha ya watoto wako ingekusaidia sana, kama tume ni huru kwanini Lema asiteuliwe kuwa Mkurungezi wa tume ama professor J? pia kwanini wote wanaoteuliwa wawe na mlengo wa CCM pekee? shame on you kujifanya hujui hujuma wanazofanyiwa Chadema na ACT
 
1 .Vipi NEC inasemaje mgombea anapoongea Lugha ya kikabira?

Andiko lako ni Lefu Limejaa Porojo tupu.
Umekosa hoja za msingi.

Tuanzie hapa tu kabla hatujaenda kwenye Engua na Mapingamizi ya Ubunge na Udiwani kwa wapinzani pekee.
Hata mie sijalisoma nmelidharau tu
 
Chadema wanajua hawez toboa , ndo mana wanatafuta chokochoko za vurugu , Sisi kazi yetu ni moja tuu , upigaji kura uishe Kwa Aman , tuhesabu kura mshindi atangazwe baada ya hapo hatutak maneno maneno tena , anayekaidi anakula rungu, mwendo uleule kampeni mpak August 2025
Usomi wako bure kabisa !!. Ni kweli tume ipo kisheria, lakini sheria inayoiunda tume za uchaguzi ni mbovu.

1. Anayeteua viongozi wa tume na kuwaapisha pia ni mshindani mwenye maslahi na uchaguzi unaofuata. Kama ilivyo sasa !!. Hapo sheria hiyo imekaa kimya.

2. Watendaji ngazi ya Jimbo ni wateule wa moja wa washindani. Anawaapisha na kuwakemea. Kama ilivyotokea safari hii na sheria hizo zimekaa kimya.

3. Tumeona ngazi ya kata watendaji wakiitwa ikulu na walipotoka huko, kazi ikawa ni kuwakimbia wagombea wa vyama vingine. Na sheria hizo zimekaa kimya.

Imeundwa kwa mujibu wa sheria lakini sheria mbovu.
 
Sheria inaweza kusema hivi but what is really happening on the ground might be quietly different! Additionally, Sheria sijui Katiba kusema NEC itateuliwa na Rais ambaye, at some point, naye ni mwathirika/mnufaika wa maamuzi ya NEC tayari hilo ni tatizo! Rais anateua chombo ambacho ndicho kitakachoamua hatma yake halafu hamuoni kuna tatizo hapo? Be serious dude!
 
1. Kwanini NEC na ZEC ziteuliwe na Rais zilipwe na Rais, na zimtangaze huyilo huyo Rais wakati wa Uchaguzi?
....
# Nashukuru hujasahau kuweka namba japo umechelewa.
NI YEYE.



Usomi wako bure kabisa !!. Ni kweli tume ipo kisheria, lakini sheria inayoiunda tume za uchaguzi ni mbovu.

1. Anayeteua viongozi wa tume na kuwaapisha pia ni mshindani mwenye maslahi na uchaguzi unaofuata. Kama ilivyo sasa !!. Hapo sheria hiyo imekaa kimya .
2. Watendaji ngazi ya Jimbo ni wateule wa moja wa washindani. Anawaapisha na kuwakemea. Kama ilivyotokea safari hii na sheria hizo zimekaa kimya.
3. Tumeona ngazi ya kata watendaji wakiitwa ikulu na walipotoka huko, kazi ikawa ni kuwakimbia wagombea wa vyama vingine. Na sheria hizo zimekaa kimya.

Imeundwa kwa mujibu wa sheria lakini sheria mbovu.

Watumishi wa Serikali wote hulipwa na Serikali ambayo Kiongozi Mkuu ni Rais. Isitoshe watumishi wa Serikali wa ngazi za juu, huteuliwa kwa taratibu zilizowekwa kikatiba na hatimaye kuthibitishwa na kuapishwa na Rais.

Hoja zenu hizo za kitoto.
 
Watumishi wa Serikali wote hulipwa na Serikali ambayo Kiongozi Mkuu ni Rais. Isitoshe watumishi wa Serikali wa ngazi za juu, huteuliwa kwa taratibu zilizowekwa kikatiba na hatimaye kuthibitishwa na kuapishwa na Rais.

Hoja zenu hizo za kitoto.
Kwa vile zina masilahi upande wako utaziona za kitoto.

CCM, chama kikongwe na inayokubalika, inaghwaya nini TUME HURU YA UCHAGUZI?!. Hofu ya nini?!
 
Wana sayansi kuna watu huwaita "authorities" na hawa huwa vyanzo vya elimu fulani. Mkapa Marehemu Benjamin hata usimpende alijua mengi kuhusu siasa za Tanzania. Alikuwa mmoja wa authorities wa siasa na uchaguzi Tanzania, kwani chini yake uchaguzi wa 2010 ulifanyika. Sasa mkapa katika kitabu chake amesema wazi wazi kwamba angefurahi nchi yetu kupata TUME HURU ya uchaguzi. Sasa sisi ni nani tupingane na mkapa (Raisi Mstaafu na Mwenyekiti wa CCM)? Tusichanganye watu.
 
Nec na Zec ni tume huru.kulalamika kwa Chadema ni kawaida kabisa hawana namna ya kujipanga zaidi ya kulalamika kwa kila jambo.
 
Acha kujitoa ufahamu ilihali unaujua ukweli, mbona watu mnapenda kujipendekeza kiasi hicho? Unatetea ushetani huo ili ufaidike nn? Ulaaniwe ww na kizazi chako mfe haraka kama Shana.
 
ZEC hii hii ilikuwa chini ya mzee Jecha ndo tume huru?

NEC hii hii iliyopo chini ya Mahela aliesema atailinda ilani ya ccm kwa nguvu zote ndo tume huru?mkuu naona umevimbiwa kwa kula makande si bure!

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app
 
Tanzania ni moja kati ya The Poorest Countries in the World inashika nafasi ya 8 kutoka chini. ( Focus economy 2019- 23)

CCM imetufikisha hapa.
 
Umejitahidi sana kurembesha maneno ili kutetea dhambi lakini moyo wako unakusuta.

Sijui ni kwanini mnaogopa sana uwepo wa tume huru ya uchaguzi. Najua hofu yenu inatokana na kutokujiamini kwenu. Mnajua kiuhalisia hamkubaliki hivyo mnajua uwepo wa tume huru isiyofungamana na upande wowote itakuwa ndio mwisho wenu wa kutawala.

Eti unasema tume ipo kwa muujibu wa sheria(so what) Nani alikwambia kitu chochote kinachofanyika kisheria ni chema? Hivi hujui kuna sheria nyingi tu zimetungwa kwa nia ya kuhalalisha nia ovu.

Sent from my A37f using JamiiForums mobile app
 
Ukirejea ya Zanzibar 2015 utagundua ulichoandika hakiakisi hali halisi nchini kwetu!Vyombo vyote vya kimataifa vilijiridhisha kuwa uchaguzi Zanzibar ulikuwa huru na haki na wakatoa report zao kuonesha hivyo!

Lakini katika kutangaza matokeo ZEC wakaona mgombea wa CUF Maalim Seif kamzidi wa CCM,ghafla meza ikapinduliwa na kuamriwa kwamba uchaguzi haukua huru na haki na hao hao ZEC ili kuifaver serikali ya chama cha mapinduzi!

Inaingiaje akilini kituo kimoja,kura zimepigwa za aina 3,ila kura za aina 2 yaani zile za wawakilishi na rais zanzibar tukaambiwa sio huru na za Rais wa JMT zikawa huru?Muda uleule,eneo lilelile na mpiga kura ni yuleyule?

Kwa uchaguzi ule, kama mgombea wa CCM angekuwa anaongoza basi nakuhakikishia uchaguzi usingefutwa!

Hii ndiyo hali ya tume zetu hizi mbili nchini!Haihitaji akili kubwa kujua hizi tume zipo kuwatumia CCM, basi!
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Watumishi wa Serikali wote hulipwa na Serikali ambayo Kiongozi Mkuu ni Rais. Isitoshe watumishi wa Serikali wa ngazi za juu, huteuliwa kwa taratibu zilizowekwa kikatiba na hatimaye kuthibitishwa na kuapishwa na Rais.

Hoja zenu hizo za kitoto.
... hicho ndio hasa kiini cha tatizo - KATIBA/SHERIA! Katiba na sheria havikushushwa kutoka mbinguni; vilitungwa na wanadamu walio na interests zao. KATIBA/SHERIA hurekebishwa kuendana na mahitaji ya wakati. Uteuzi na muundo wa NEC tayari umeonekana kuwa na tatizo kwa mazingira ya sasa ninyi mmekomalia KATIBA, KATIBA, KATIBA kana kwamba imeshushwa na Jibril!

Wanaohoji hawamaanishi Katiba na Sheria havina maana ila pale inapoonekana kuna tatizo virekebishwe ili kuendana na mahitaji ya wakati.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Subirini muondolewe madarakani tena msisubutu kutumia mabavu na kupelekea kuvunja amani. ICC itawahusu.

Kwa hapa Dar unaweza usielewe vizuri ila Zenji likibutuka basi tambua Hata huku bara kuta pamba moto
 
Tume kuwa huru ni kukubali inapotuhumiwa kufanya upendeleo ikubali kukaa pamoja na wadau ili kuwaondolea ,mashaka.
Tume inapokuwa huru inaweza kushitakiwa mahakamani kwa kutangaza mtu ambaye hakupata ushindi kwa wingi wa kura.

Tume inapokuwa huru huwa haipendelei chama tawala kwa namna yoyote ile, wala haitowi vitisho kwa wapinzani, bali husikiliza sauti ya kila mlalamikaji na kuifanyia kazi ipasavyo.

Sasa Tuambie wewe,ZEC imefoji fomu ya Mgombea wa Uraisi na ilipodhihiri wakaishia kumteua na kusema wasamehewe .
Ninani aliyefoji ile fomu mulendani ya tume? Kachukuliwa haua gani?

ZEC imebainika kuwa pingamizi zote za wawakilishi zimeandikwa na mtu mmoja kwa muandiko unaofanana.
 
Back
Top Bottom