NEC na ZEC ni Tume Huru kwa mujibu wa Sheria, nongwa inatoka wapi?

 
Unaelewa kabisa unafanya siasa za matumboni huku tume huru ya uchaguzi ikiwa mfukoni mwa ccm, kweli wasomi wa Tanzania mpo tayari kuua watu milioni 1 kwa ajili ya kupata TSh 1 million, ulaaniwe kwa ushenzi huu.
 
Kwa vile zina masilahi upande wako utaziona za kitoto.

CCM, chama kikongwe na inayokubalika, inaghwaya nini TUME HURU YA UCHAGUZI?!. Hofu ya nini?!
Unaona kuwa zina maslahi upande wangu kwa kuwa umeamua kutokuona na kukubali ukweli kwamba watumishi wa Tume (ambao ni wachache sana) siyo wote wanaipenda CCM. Hata kama wote wataipenda CCM siyo wapiga kura.

Uchaguzi ni mchakato kama ifuatavyo:-
1) Kujiandikisha kwa kila Mtanzania mwenye sifa za kupiga kura. Hatua ya kwanza iliyo huru kabisa. Je, kuna Mtanzania aliyenyimwa haki hiyo?
2) Kuhakiki daftari la wapiga kura ili kuondoa makosa yoyote yatakayo yamejitokeza kwenyr uandikishaji.
3) Kila chama kuteua watu wenye sifa za kuwakilisha chama kwenye kinyang'iro cha kupigiwa kura. Huu nao ni mchakato ulio uhuru wenye sifa za kugombea haki yao.
4) Wateuliwa wa chama kuthibitishwa na Tume kama wametimiza masharti yote yaliyowekwa. Mchakato huu unang'unikiwa kuwa unatoa nafasi ya wagombea halali kuenguliwa. Kuna uwezekano, lakini ni vyema kujua kuwa ni yule aliyeenguliwa anao uhuru na haki ya kukata rufaa kama ilivyo kisheria. Bahati mbaya, ama kwa makusudi, viongozi wa vyama badala ya kulikuchukulia suala hilo kwa uzito unaostahili, huamua kutanguliza lawama. Ni bahati mbaya pia kilichotokea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuenguliwa kwa wagombea na kusabibisha kususia uchaguzi, halijawa funzo kwa viongozi wa vyama husika.
5) Wagombea waliopitishwa wako huru kutumia haki yao ya kufanya kampeni. Ni zoezi ambalo zinaendelea kwa sasa. Bila shaka uhuru na haki hiyo wagombea wanatumia kwa mujibu wa sheria.
6) Vituo vya kupigia kura hutangazwa mapema na majina ya wapiga kura kubandikwa. Mpiga kura anao uhuru na haki ya kwenda kuthibitisha kuwa jina lake lipo.
7) Siku ya kupiga kura, waliojiandikisha wana uhuru na haki ya kwenda kupiga kura.
8) Wakati wa kupiga kura mpiga kura anao uhuru na haki ya kumchagua mgombea anayempenda.
9) Vyama vinavyoshiriki kwenye Uchaguzi wana uhuru na haki ya kuweka Wakala kila kituo kuhakikisha uhuru na haki ya kila mpiga kura inaheshimika.
10) Baada ya zoezi la kupiga kura, uhesabuji wa kura ufanyika kwa ushiriki wa Mawakala wa vyama. Hawa wanayo haki na uhuru wa kushiriki.
11) Baada ya hesabu ya kura kukamilika, Mawakala wa vyama wanao haki na uhuru wa kuthibitisha ukweli huo kwa kusaini karatasi za matokeo hayo. Lakini, kuna ukweli kwamba Mawakala wa vyama vilivyofanya vibaya kwenye kituo hukataa kusaini, si kwa sababu matokeo siyo sahihi, bali aibu.
12) Matokeo ya vituo hujumuishwa na Tume kisha kutangazwa mshindi.
13) Mgombea yeyote anao uhuru na haki ya kukata rufaa kama hakuridhika na matokeo hayo. Km kama haridhiki na matokeo ya kituo chochote, anao uhuru na haki ya kuona matokeo hayo ili ajiridhishe.

LAWAMA KWA TUME NI UNAFIKI MTUPU. Acheni VIOJA, JENGENI HOJA.
 
K Hongera kwa Uchambuzi makini Sana ! Uchambuzi uliojaa Elimu pana !
 
Noise!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…