NEC na ZEC wanaweza kulipasua taifa. Wanaharakati na viongozi wa dini mko kimya? Subirini tatizo

NEC na ZEC wanaweza kulipasua taifa. Wanaharakati na viongozi wa dini mko kimya? Subirini tatizo

Prof Koboko

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2020
Posts
350
Reaction score
2,550
Haiwezekani nchi nzima wanaokosea kujaza forms ni wagombea wa upinzani, haiwezekani wanazijaza forms vizuri ni wagombea wa ccm tu.Wagombea wa CCM wamesomea shule za nchi tofauti? Wakati NEC na NEC zinatoa semina kwa viongozi wa vyama vyote vya siasa, CCM walikua na semina yao ya tofauti?

Liwake jua inyeshe mvua Mkurugenzi wa NEC Dr Mahela kwa historia yake huko nyuma inaonesha alikua mtiifu kwa chama cha mapinduzi, sina historia vixuri na Jaji Kaijage ila kwa huyu Mahela hata mtoto mdogo anaijua. Hawezi kuacha itikadi yake akaenda kutenda haki katika chombo huru kinachopaswa kutenda haki. Kwanza Dr Mahela siyo mwanasheria tuseme anaweza kutafsiri sheria vizuri, huyu binafsi simkubali kabisa na maamuzi yake.

ANGALIZO KWA ZEC NA NEC
Tunaomba wagombea wote walioengiliwa kwa makosa ya kibinadamu ambayo hayana dhamira ya kujinufaisha warudishwe wote sanduku la kura likaamue. Msilazimishe kitu tusichokitaka na msitegemee kulindwa na Dola kuibeba CCM, kamwe wananchi hawatokubaliana na huu uonevu.

Watu waenguliwe kwa makosa dhahiri kama vile Uraia, jinai na na kutokujiandikisha kupiga kura. Hayo ni makosa ya msingi ambayo mtu hana la kujitetea.

Ni ajabu kumuengua mtu kisa ameandikiwa na Hakimu kifupi cha chama chake, kosa ambalo si lake. Hii siyo sawa hata kidogo tuitetee amani ya taifa.

RAI KWA VIONGOZI WA DINI NA WANAHARAKATI
Niwashauri viongozi wa dini mliokalia huu uovu bila ya kuukemea, mnatenda dhambi kubwa sana na hamtokas kuuona ufalme wa mbingu. Kukalia kimya kitu ambacho.
 
TUME ya Uchaguzi imeandikwa Kikatiba katika ibar aya 74 (6) na kuendelea; Madiwani Kukosea kujaza fomu huko kweye KATA, WEOs ndio mikono ya TUME ambayo wanatakiwa kuwasaidia wananchi kujaza vizuri;

Kumlauma DR MAHERA sio sawa kwa sababu maDED ndio Mikono y TUME kwa WILaya na KATA chini ya WEO; sasa kama WEOs wanaipendelea CCM;

NEC huko juu wanatakiwa kuwa macho hasa nyakati za UCHAGUIZI maana mchakato wa uteuzi ulikwisha; TATIZO la TUME yetu sio MTU bali MFUMO/SYSTEM ya upatikanaji wa watendaji wa TUME
 
Wanaccm wanaamini tume itawatangaza kwa lazima.
 
Mmeanza kutafuta Visingizio mapema. JPM tano tena.
 
Viongozi wa dini wanasubiri kuchafuke ndipo waseme, mambo yanayofanywa na tume ni zaidi ya aibu...
 
TUME ya Uchaguzi imeandikwa Kikatiba katika ibar aya 74 (6) na kuendelea; Madiwani Kukosea kujaza fomu huko kweye KATA, WEOs ndio mikono ya TUME ambayo wanatakiwa kuwasaidia wananchi kujaza vizuri; ...
Hao watendaji ndio wawakilishi wa NEC na ZEC, hayo Madudu yao tume zinatakiwa kuyafuta
 
Tulisema sasa basi, iwe kwa vitendo. Hadi leo hii suzan kiwanga hajarudishwa, ila kilichopo ni kelele tu huko twitter. Chadema sisi ni wapumbavu sana
 
Tulisema sasa basi, iwe kwa vitendo. Hadi leo hii suzan kiwanga hajarudishwa, ila kilichopo ni kelele tu huko twitter. Chadema sisi ni wapumbavu sana
Tushasema tatizo ni POMBE. Huyo Mama wanamuogopa sanaa, watarudisha ila watakua wameshampotezea muda sana na atashinda kwa kishindo. Kunambi hawezi siasa za pale pamoja na Kilombero
 
Atarudishwa lini wakati kunambi kishatangazwa na tume??
Tushasema tatizo ni POMBE. Huyo Mama wanamuogopa sanaa, watarudisha ila watakua wameshampotezea muda sana na atashinda kwa kishindo. Kunambi hawezi siasa za pale pamoja na Kilombero
 
TUME ya Uchaguzi imeandikwa Kikatiba katika ibar aya 74 (6) na kuendelea; Madiwani Kukosea kujaza fomu huko kweye KATA, WEOs ndio mikono ya TUME ambayo wanatakiwa kuwasaidia wananchi kujaza vizuri...
Ukiachia mapungufu ya tume., Bado ina maamuzi ya Mwisho ya suala lolote linalohusiana na uchaguzi. Watumie hayo madaraka waliyopewa na Sheria kuwarudisha wagombea wasio na makosa yanayoswihi, uraia, jinai nk. Mbona wamemrudisha mwanyika aliyekiri kisa la jinai kukwepa Kodi na Mambo yanaendelea kawaida? Tume irudishe wagombea tafadhali
 
Wanaccm wanaamini tume itawatangaza kwa lazima.
Mwelekeo uko hivyo. Angalia suala la Mlimba na Susan Kiwanga! Ushahidi wa wazi, lakini wamemtangaza Kunambi kupita bila kupingwa
 
Back
Top Bottom