Kabende Msakila
JF-Expert Member
- Oct 7, 2020
- 1,809
- 1,692
WanaJf, Salaam!
Naona tume ya uchaguzi nchini Tanzania NEC imepewa meno makali ya kisheria ili kuleta ufanisi ktk uchaguzi mkuu utakaofanyika nchini 28 Oktoba 2020. Hata hivyo nashauri yafuatayo:
Mosi, tume isifanye kazi kama kiranja badala yake iwe kama mzazi (siyo lazima kila jambo linalifanywa na vyama vya siasa linapaswa kuandikiwa barua). Mambo mengine yanahitaji kukaa na kuzungumza;
Pili, amani ya nchi inawaangalia sana ninyi - kwamba kushindwa kwa mgombea yeyote siyo mwisho wa maisha yake (akishindwa) apumzike na wengine waongoze iwe nafasi ya Urais, Ubunge, na Udiwani. Lakini atakayeshinda nafasi yoyote kati ya hizo asijione mjanja na kuanza chokochoko.
Tatu, heshima kwa wapigakura - tume na extended arms yake waheshimu sana utashi wa wananchi wapigakura - kila chama na wagombea wake wamejinadi vya kutosha - aliyejinadi vizuri atapata kura nzuri na aliyejinadi vibaya atapata kura mbaya - hivyo tume isimwonee huruma atakayeshindwa ktk uchaguzi huo;
Nne, vitendo vya uapishaji mawakala - ktk maeneo mengi yapo malalamiko kwamba baadhi ya mawakala wanasumbuliwa kuapishwa na wakurugenzi wa uchaguzi - hiki ni kiashiria kikubwa cha watu kuingia ktk ugomvi na kuhasimiana baina ya makundi - hili likemee ikiwezekana iwapo itagundulika mawakala wasioapishwa basi uongeze muda zaidi ili waapishwe na kusimamia uchaguzi huo kwa kuwa Tanzania ni zaidi ya chama cha siasa;
Tano, kupiga kura, kuhesabu na kutangaza matokeo ya uchaguzi - kwa hakika jinsi ninavyowafahamu watanzania ikiwa kutakuwa na uwazi wa kutosha hakika amani, utulivu, na mshikamano wa kitaifa vitatawala - mashaka yangu ni kwamba iwapo vitu hivi vitafanywa kwa hila basi huenda vikawa kuni ya kulibomoa taifa na ujenzi wake utachukuwa muda mrefu huku tukiwa tumeandika historia mbaya mbele ya jumuiya za kimataifa - sote bila kujali wadhifa wetu tuendelee kuheshimiana - taifa ni zaidi ya chama cha siasa!
Tume ya taifa nawapenda sana na kuwaombea roho ya ujasiri mnapotekeleza majukumu yenu mazito - nasi tutawaunga mkono iwapo mtatekeleza majukumu hayo kwa uzalendo - lkn pia tutatofautiana nanyi iwapo mtachepuka.
Mung ibariki Tanzania,
Mungu ibariki Afrika (nchi salama, mataifa salama).
Msakila M Kabende
Mpiga Kura 2020