Uchaguzi 2020 NEC: Wagombea muwe makini, tusilaumiane

Yaani uingie kwenye chumba cha mtihani halafu utake msimizi wa mitihani akusomee na kutafasiri mahitaji ya swali.Wewe hutakiwi hata kujipigia kura mwenyewe, unastahiri kupata ZERO
Mfano wako mzuri sana. Nchi zilizoendelea mwalimu anahakikisha wanafunzi wana vifaa vya kuandikia. Na anakueleza mahitaji ya swali kwa sababu lengo la mtihani sio kukufelisha bali kupima uelewa wako.

Ndio maana mara nyingi unaruhusiwa kuingia na vitabu na calculator kwenye mtihani. Kwenye uchaguzi hatutafuti bingwa wa kujaza fomu bali mtu ambae wananchi wataona anafaa kuwawakilisha na kuwapigania.

Kumtoa mgombea kwa sababu ameandika Fundi Mchundo badala ya F Mchundo sio haki.

Amandla...
 
Kwani Kuna wagombea vichaa?
Kama mgombea kiti cha urais hawezi kujaza fomu kwa usahihi, hafai
Wangekuwa vichaa, hata kuwaelekeza ingekuwa bure. Tatizo la hali iliyopo ni kuwa inatoa nafasi kwa wasimamizi kuwasaidia tu wale wanaowapenda na hata kwa baadhi kuingiza dosari ( herufi katika jina) katika fomu ya yule wasiemtaka. Hii inawezekana isiwe kweli lakini ndivyo watu watakavyoamini hasa inapotokea kuwa ni wagombea wa vyama fulani tu ndio wanaokosea.

Amandla...
 
Ngoja wamtumikie shetani , tutaona mwisho wao ni UPI Rip Mkapa.
 
Nani atakuruhusu kupiga picha fomu yako? Ingekuwa vyema kama msimamizi angekuwa anasaini nakala ya fomu iliyowasilishwa kuthibitisha kuwa amepokea.

Na pale inapoonekana imekosewa mgombea arudishiwe fomu aliyowasilisha ikionyesha dosari zilizoonekana. Lakini sidhani kama inakuwa hivyo.

Amandla...
 
Hawa washenz wa akili hawawez kukuelewa
 
Kujaza fomu ni njia tu ya kupata taarifa sahihi za mgombea. Nia ovu za kipuuzi zimeanza kutumika kupitia fomu kuwaondoa wagombea, hii siyo sawa hata kidogo (rejea uchaguzi wa serikali za mitaa).

Watu wenye hila mbaya hawatakiwi kuwa waamuzi katika jamii au taifa. Uovu unaweza kuhalalishwa kwa kutumia sheria na kanuni pale tu kwenye waamuzi wabaya.
 
Ukianza kula nyama ya mtu huachi!

CCM mlishaonyesha umafia wenu chaguzi za mitaa!
 
Tume ipo sahihi sema kuna wagombea husubiri siku ya mwisho ndio wanarudisha fomu. Tabia hiyo ibadilike.
 
Yaani uingie kwenye chumba cha mtihani halafu utake msimizi wa mitihani akusomee na kutafasiri mahitaji ya swali.Wewe hutakiwi hata kujipigia kura mwenyewe, unastahiri kupata ZERO
Hahahaaaaaaaa kukosea ndio moja ya kuonesha huwezi kazi.
 
Naomba ufafanuzi: Kama mgombea au mtia nia asipojiandikisha kwenye daftari la mpiga kura bado atakuwa na sifa ya kugombea Urais, Ubunge au Udiwani. Kuuliza si ujinga.
 
Baada ya utawala wa JPM hakuna tena mtu atakayeheshimika kwa title yake....sijui Dkt (PhD), Profesa, Jaji n.k

Wote wamekuwa wapuuzi puuzi tu
 
Kuna mtu alikwishawahi kujiuliza swali hili?? Inakuwa mgombea wa chama kimoja anaweka pingamizi kuwa fomu ya mgombea wa chama kingine sio sahihi wakati mgombea huyo hakukabidhiwa fomu hiyo???

Ukweli ni huu - NEC huchukua fomu za wagombea na kuzikabidhi kwa chama fulani ili wagombea wake waweke pingamizi. Tume haijawahi kuweka pingamizi kwa mgombea!!

Kwa sasa tume ingeita wagombea wote pamoja na kuzikagua na kuzirekebisha. Mapingamizi mengine ambayo sio makosa ya jinai au madai hayana maana lakini Tume imekuwa ikiyakubali kwa faida ya chama kimoja!
 
Hii tume sio rafiki kabisa kwa wadau wa uchaguzi pia haina ushirikiano kabisaaaa yaaani mi siamini kwa tume hii kama kutakuwepo na uchaguzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…