NEC, Wakati huu wa Corona uandikishaji wa wapiga kura uangaliwe vizuri

NEC, Wakati huu wa Corona uandikishaji wa wapiga kura uangaliwe vizuri

kindikwili

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2016
Posts
1,862
Reaction score
2,876
Wakuu habari za asubuhi!

Napenda kuwaomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuangalia namna bora zaidi ya kuboresha daftari la wapiga kura wakati huu wa corona bila kuleta athari kwa jamii. Kama ugonjwa huu utaingia vijijini hali yetu itakuwa mbaya sana kama taifa hivyo napendekeza yafuatayo kwa Tume ya Uchaguzi ya Taifa.

1. Huu si muda wa kutumia watu kutoka nje ya eneo husika kuandikisha wapiga kura- Ingekuwa vyema wanaoandikisha wananchi wakawa ni watu wa eneo husika. Hii ya watu kutoka wilaya nyingine halafu hao hao wanazunguka sehemu tofauti ni hatari kubwa wakati huu.

2. Tume iombe Jeshi la polisi kusimamia mchakato mzima wa uandikishaji -yaani askari polisi ahakikishe mwananchi moja ndiye anayeingia ndani tena baadaa ya kunawa kwa maji tiririka na sabuni.

3. Tume ihakikishe kuna sanitizer kwenye chumba cha kuandikishia na kila baada ya mtu moja kalamu ya kusainia kitambulisho kile kinatakaswa vyema kabla ya kutumika tena na mtu mwingine.

4. Wahakikishe uwepo wa barakoa kwenye kila kituo cha kuandikishia na maji safi ya kunawa.

5. Siku za kuboresha daftari zinaweza kuongezwa kama watu ni wengi kuepusha msongamano.

Luhaga Mpina.JPG

Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Lubiga Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu, Buyamba Duba akiangalia kwa makini namna Mbunge wa Jimbo la Kisesa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akihakiki taarifa zake kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura katika Ofisi ya Kata ya Lubiga. Aprili 22, 2020

Mwisho serikali isipate taabu kuweka kijiji kizima quarantine ikibidi endapo itabainika kuna mtumishi wa tume yeyote kafariki kwa ugonjwa wenye dalili za COVID 19 badala ya kuwafuata watumishi hao huku wananchi wakibaki wamepigwa na butwaa wasijue nini ni shida.

Nimeshauri kwa moyo wa uzalendo mimi siyo nabii ila common sense inanituma kuamini zoezi hili lisipoangaliwa vyema inaweza kuleta balaa huko vijijini.
 
Vyema wahakikishe kila mtu anayefika kituoni kujiandikisha amechukua tahadhari ya kujikinga, especially mask, na hili litategemea upatikanaji wa hivyo vifaa vijijini, vinginevyo wanaenda kutengeneza tatizo jingine kubwa zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Denooj mpaka nimeandika uzi huu ujue sijakurupuka umakini unatakiwa uongozwe maradufu na hali ikiendelea hivi wasisite kusitisha kwa muda zoezi lenyewe.

Ombi langu kwa Mungu siku zote ni huu ugonjwa usije ukaenea sana nchini maana hali itakuwa mbaya sana
 
Mkuu Denooj mpaka nimeandika uzi huu ujue sijakurupuka umakini unatakiwa uongozwe maradufu na hali ikiendelea hivi wasisite kusitisha kwa muda zoezi lenyewe. Ombi langu kwa Mungu siku zote ni huu ugonjwa usije ukaenea sana nchini maana hali itakuwa mbaya sana
Zoezi likisitishwa kuna uwezekano uchaguzi nao kusogezwa mbele, au usifanyike kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zoezi likisitishwa kuna uwezekano uchaguzi nao kusogezwa mbele, au usifanyike kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwani uchaguzi na maisha ya watanzania nini bora, uchaguzi upo tu unaweza hata kufanyika january mwakani ila maisha ya watanzania waliokufa hayawezi kurudi tena
 
Mkuu Denooj mpaka nimeandika uzi huu ujue sijakurupuka umakini unatakiwa uongozwe maradufu na hali ikiendelea hivi wasisite kusitisha kwa muda zoezi lenyewe.

Ombi langu kwa Mungu siku zote ni huu ugonjwa usije ukaenea sana nchini maana hali itakuwa mbaya sana

Mkuu wala usipate, toka iingie awamu yake hii madarakani, uchaguzi unanajisiwa vibaya sana, hivyo wananchi wanaojitambua hawajitokezi kujiandikisha kupiga kura. Hivyo wanaojitokeza ni wachache sana na hawana hamasa yoyote. Kwa sababu hiyo hakuna hatari yoyote kama ilivyo kwenye vyombo vya usafiri ambapo watu wanabanana, na kondakta ndio anayekusanya nauli kwa watu wote ndani ya chombo cha usafiri.
 
Back
Top Bottom