Elections 2010 NEC yabadili matokeo ya Vunjo yasema ilikosea

Kwa maana hiyo kama Mrema angekuwa ameshinda kwa chini ya kura 6,372 tungesikia matokeo tofauti na hayo tunayo yajua kwa sasa....dawa ya hawa mafisadi ni kuwa shinda kwa kura nyingi mpka wanachanganyikiwa kuchakachua mtu kaongezwa kura 6,372 lakini bado tu...sijui hawajui mahesabu kweli si uliona zile za spika wa bunge walituambia CCM 74% CMD 16% zilizokuwa zimehalibika 2% sijui kama wamesha fanya malekebisho mpaka sasa au wamepotezea
 
matokeo yote yakianza kupitiwa namna hii tunaweza kujikuta tunaingia matatizoni tu..
wanaweza kuingiza nchi vitani hawa kama walishindwa kuwa makini kabla hawajatangaza ni bora wawajibike, tunajua wametuchangulia viongozi
 
matokeo yote yakianza kupitiwa namna hii tunaweza kujikuta tunaingia matatizoni tu..
Mzee Mwanakijiji, hatuwezi kuingia katika matatizo yoyote kwa sababu hayo matatizo katika matokeo, sio matatizo ya kweli, it was a delibarate move, pre meditated ili kusaidia upande fulani.

Baada ya taarifa rasmi ya juzi kuwa Chadema haiyatambui matokeo, NEC hawalali usingizi, lazima wayatangaze madudu yao yate as 'orninary mistakes' kabla the dossier ya Dr. Slaa haijatoka.

Siku Kiravu anasoma barua ya malalamiko ya Dr. Slaa, alionyesha dharau na dhihaka na ndio maana NEC waliignore kuijibu mpaka leo, hata wakati Kiravu anaadmit walichanganya matokeo ya jimbo moja na jingine, his face was confortable as if nothing happenned, nilitegemea he would have looked sorry!.

Nadhani jamaa wa TISS waliwaruhusu NEC to do whataver they can do na maadam they didi it well, they are protected and safe, nothing will happen anymore, water cannon ziko distributed mikoa yote, there is nothing to worry, Watanzania ni watu wa amani, hawapendi vurugu, you can do them all sort of things na ukimaliza, ni watu wa kusema hewala bwana!.

Ninauhakika wa 100% kwa 100%, Jaji Makame na Kiravu wanastaafu soon, tena wanastaafu kwa heshima badala ya kwa aibu, hii ndio Tanzania yetu.
 

Spot-on. I must say......................
 
Tatizo la historia bwana ni kuwa huwezi kuikimbia wala kuikwepa.. lakini la kutisha zaidi ni kuwa historia ina tabia ya kufunua yaliyofichwa. Hata kama haitatokea wiki hii, hataka sisi sote tuliyoyashuhudia tutakuwa kwenye mavumbi bado historia inaweza ikafunua na kuwaelewa watoto wetu kilichotokea - kwa wema au kwa ubaya.
 
matokeo yote yakianza kupitiwa namna hii tunaweza kujikuta tunaingia matatizoni tu..

...Sahihi. Ila, tuingiie matatizoni mara ya ngapi? Nadhani tu matatizoni tayari.

...Kuna watu wadai wanafahamu matokeo tafauti na haya tunayoyafahamu [rasmi], na idadi yao inaongezeka...sijui wanayapata wapi.

...Kama vile haitoshi, NEC wanatuletea marekebisho yanayotoa picha ya makosa makubwa kabisa. Maji yalianza tuama...wao wanayatibua, kana kwamba hawajui yana tope!
 
Nauliza: Jee, iwapo baada ya masahihisho ingetokea gombea wa Chadema au yuile wa CCM ndiyo kashinda, Nec wangetangaza vilivyo? Yaani kubadilisha mshindi?
 

Aisee! You are damnly right, hii inaleta shida tena kubwa na pengine wanatafuta jinsi ya kumwezesha Meela wa CCM aweze kulalamika na kushinda! Kwa mahesabu haya ulivyojumlisha kura zilizohesabiwa kwa pamoja ni 62,049, ambayo ni tofauti ya kura 6,947. Meela akidai hizi za ziada zinapaswa kuwa ni za kwake, basi atakuwa amepata kura 30,817 na hivyo kumzidi Mzee wa Kiraracha kwa kura saba!!!!!

Hivi kweli with all the IT guys na nawaona wanaoingia pale Tume na vimikoba vya Laptop, inakuwa vigumu kiasi hiki kujumlisha hesabu kidogo! Taifa hili! Lakini nafahamu hakuna kazi kubwa kama kudanganya. Ukichakachua vinamba, ni lazima uwe na akili za ziada za kuweza ku-maintain consistency katika tarakimu zote! TUME inapaswa kujiuzulu SASA! AIBU KUBWA KWA TAIFA
 
Hayo ni ya mbunge tu walijichanganya je ya President???bora tu wangekaa kimya maana hapa saa ndo wanatufanya tuamini ya kuwa hawakuwa makini na kazi yao.
 
Wanasheria nisaidieni,
Kwenye sakata la Segerea Makame alisikika akisema NEC ikishatangaza matokeo chombo cha kutengua ni Mahakama pekee, je kwa wao kutengua matokeo ya Vunjo NEC wameingilia kazi ya mahakama? na je kama wana uwezo wa kutengua ni kwa kipindi gani baada ya matokeo kutangazwa wiki, miezi 2 miaka 3?
 
Augustine Mrema TLP 30,810 (29,047)=====> -1763
Chrispin Meela CCM 17,498 (23,870)======> +6372
John Mrema Chadema 6,558 (6,316)======> -242
Lyimo wa NLD kura 811 (118) ==========> -693

Hawa wa tofauti na sisiemu walikumbwa na -ve error lkn wa sisiemu alikumbwa na +ve error. Naungana tena na dr. siyatambui matokeo
 

Luteni,

Asante kwa masahihisho. Nafikiri kura halali ni zile baada ya kuondoa kura zilizoharibika, hivyo huenda total kwasasa iko sawa.

Kinachoshangaza, ilikuwaje hakuna chama kilicholalamikia matokeo hayo? Nakala na matokeo vituoni kila chama kinakuwa nazo, inaelekea vyama havikuwa makini kuhakikisha wanajumlisha kura zote toka kwa mawakala wao ili kujiridhisha.

Hapo ni tatizo maana kama kuna udhaifu kama huo, mkurugenzi wa uchaguzi anaweza kutangaza matokeo yake ambayo hayaendani na ukweli vituoni na wahusika wasijue ukweli wake.
 

Luteni,

Sidhani kama NEC kwa kufanya masahihisho wametengua matokeo ya uchaguzi. Ila kama tofauti ya hizo kura ingemfanya mtu mwingine na sio Mrema awe mshindi, hapo ndipo pangelikuwa na kazi kubwa.

Mimi sio mwanasheria, lakini nafikiri ingelitokea hivyo NEC wenyewe wangeliweza kwenda mahakamani kuomba itengue matokeo hayo.
 

Shikamoo Mama Mdogo,

I love you. Nimependa kilemba chako na kapointi hako nilikokakoleza.

Tuimbe pamoja wimbo huu wa taarabu. Wengine, si wanaume, magumegume, timbwili timbwili la Asha Ngedere, dereva wa kipanya, pole pole mkono na paja, ....na upenda sana wimbo huu.
 


Mkuu Mtanzania, Swali la Kujiuliza ni nani Aliywashtua NEC kwamba Matokeo waliyotangaza hayakuwa Sahihi? Na Je kama Uchakachuaji huo Ungempa Ushindi jamaa wa CCM je NEC wangekuwa tayari kurekebisha kasoro? Je Nani mwenye Makosa? NEC au Msimamizi wa Uchaguzi?

Je Makosa haya yamefanyika kwenye Majombo mangapi? NEC wakipelekwa majibu sahihi katika majimbo yanayolalamikiwa kama Arumeru Magharibi, Segerea, Kilombero itakuwa tayari kutangaza Takwimu Halisi hata kama hawawezi kutengua Uteuzi wa Mbunge Husika?

Credibility ya NEC Iko wapi?
 

Hii iliyoongezwa tayari imetumika kukokotoa idadi ya viti maalum!!!
 
NEC wameanza kuangalia huko Vunjo. Vipi wana ubavu wa kupitia tena matokeo ya urais? kama watakuta kasoro watafanya nini? Naona hawa jamaa walichukuliwa mambumbumbu wamezoea kuhesabu kutumia vidole na vijiti mara wakaletewa tekinolojia ya kompyuta. Piga, ua, garagaza hawana capacity. wamechaguana kindugu na wala siyo kwa mwenye utaalam
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…