MawazoMatatu
JF-Expert Member
- Sep 6, 2008
- 505
- 63
MtanzaniaLuteni,
Asante kwa masahihisho. Nafikiri kura halali ni zile baada ya kuondoa kura zilizoharibika, hivyo huenda total kwasasa iko sawa.
Kinachoshangaza, ilikuwaje hakuna chama kilicholalamikia matokeo hayo? Nakala na matokeo vituoni kila chama kinakuwa nazo, inaelekea vyama havikuwa makini kuhakikisha wanajumlisha kura zote toka kwa mawakala wao ili kujiridhisha.
Hapo ni tatizo maana kama kuna udhaifu kama huo, mkurugenzi wa uchaguzi anaweza kutangaza matokeo yake ambayo hayaendani na ukweli vituoni na wahusika wasijue ukweli wake.
Tume ya uchaguzi NEC imebadilisha matokeo ya uchaguzi wa ubunge Jimbo la Vunjo baada ya kugundua ilitangaza matokeo tofauti na yale yaliyotangazwa awali na msimamizi wa uchaguzi.
Nec imetangaza matokeo mapya ya Jimbo la Vunjo yanayoonyesha kuwa mgombea wa TLP, Augustine Mrema alipata ushindi wa asilimia 54 na si 50 kama ilivyotangazwa awali.
Mabadiliko ya matokeo ni kama ifuatavyo kura za zamani kwenye mabano
Augustine Mrema TLP 30,810 (29,047)
Chrispin Meela CCM 17,498 (23,870),
John Mrema Chadema 6,558 (6,316)
Lyimo wa NLD kura 811 (118)
Pia idadi halisi ya wapigakura imebadilika kutoka 55,013 iliyotangazwa awali hadi kufikia 55,102 ya sasa huku idadi ya kura halali sasa ikiwa ni 53,914 tofauti na kura halali 53,705 zilizotangazwa awali.
Kutokana na hali hiyo, Mrema ameiomba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza mazingira ya mabadiliko hayo ya kura, akisema kuwa anahisi kulikuwepo na njama za kuchakachua matokeo ambazo ziligonga mwamba.
My take: Kwa sababu kasoro za matokeo zinazidi kuongezeka, ili kuondoa manung'uniko kwa wananchi kuna haja ya kuundwa kwa tume huru kuchunguza uhalali wa matokeo. Serikali zinazoongoza huku wananchi wake wakinung'unika huwa hazifanikiwi na mara nyingi hukumbwa na mikosi mbalimbali kwenye utawala wake.
Mkuu Mtanzania, Swali la Kujiuliza ni nani Aliywashtua NEC kwamba Matokeo waliyotangaza hayakuwa Sahihi? Na Je kama Uchakachuaji huo Ungempa Ushindi jamaa wa CCM je NEC wangekuwa tayari kurekebisha kasoro? Je Nani mwenye Makosa? NEC au Msimamizi wa Uchaguzi?
Je Makosa haya yamefanyika kwenye Majombo mangapi? NEC wakipelekwa majibu sahihi katika majimbo yanayolalamikiwa kama Arumeru Magharibi, Segerea, Kilombero itakuwa tayari kutangaza Takwimu Halisi hata kama hawawezi kutengua Uteuzi wa Mbunge Husika?
Credibility ya NEC Iko wapi?
Kutengua matokeo maana yake nini, hadi aliyekuwa wa kwanza awe wa pili nafikiri hapana, kubadilisha maksi au kura za mtu kutoka A kwenda B ni kutengua hata kama ataendelea kushikilia nafasi ile ile. Hapa tunaona kama hawajatengua kwa vile kura zilizotenguliwa hazikubadili position ya mtu lakini kisheria wametengua matokeo .Luteni,
Sidhani kama NEC kwa kufanya masahihisho wametengua matokeo ya uchaguzi. Ila kama tofauti ya hizo kura ingemfanya mtu mwingine na sio Mrema awe mshindi, hapo ndipo pangelikuwa na kazi kubwa.
Mimi sio mwanasheria, lakini nafikiri ingelitokea hivyo NEC wenyewe wangeliweza kwenda mahakamani kuomba itengue matokeo hayo.
Mtanzania
NEC imesema kura halali kwa sasa baada ya marekebisho ni 53,914 hii ina maana baada ya kutoa zilizoharibika lakini ukijumlisha walizopata wagombea wote total ni 55,677 . Huwezi kutangazwa umeshinda kwa kura fulani halafu waseme hawajatoa zilizoharibika it is nonsense.
Kwa maana yako unataka kutuambia zilizoharibika ambazo siyo halali ziongezwe kwa mgombea yupi? does it make sense. Au kwa lugha nyingine the difference 55,677 - 53,914 = 1,763 ziongezwe wapi wakati wao wameshasema kura halali ni 53,914, ina maana hizo 1,763 walizopewa wagombea hazikuwa halali. Wasitake kutufanya hatujui hesabu.
Tume ya uchaguzi NEC imebadilisha matokeo ya uchaguzi wa ubunge Jimbo la Vunjo baada ya kugundua ilitangaza matokeo tofauti na yale yaliyotangazwa awali na msimamizi wa uchaguzi.
Nec imetangaza matokeo mapya ya Jimbo la Vunjo yanayoonyesha kuwa mgombea wa TLP, Augustine Mrema alipata ushindi wa asilimia 54 na si 50 kama ilivyotangazwa awali.
Mabadiliko ya matokeo ni kama ifuatavyo kura za zamani kwenye mabano
Augustine Mrema TLP 30,810 (29,047)
Chrispin Meela CCM 17,498 (23,870),
John Mrema Chadema 6,558 (6,316)
Lyimo wa NLD kura 811 (118)
Pia idadi halisi ya wapigakura imebadilika kutoka 55,013 iliyotangazwa awali hadi kufikia 55,102 ya sasa huku idadi ya kura halali sasa ikiwa ni 53,914 tofauti na kura halali 53,705 zilizotangazwa awali.
Kutokana na hali hiyo, Mrema ameiomba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuchunguza mazingira ya mabadiliko hayo ya kura, akisema kuwa anahisi kulikuwepo na njama za kuchakachua matokeo ambazo ziligonga mwamba.