Uchaguzi 2020 NEC yahimiza wananchi kujitokeza kupiga kura, yahakikisha usalama, usawa na uwazi

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2019
Posts
305
Reaction score
728
1601631459196.png

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa uchaguzi mkuu wa Oktoba 28 utakuwa wa huru, haki na wenye kufuata katiba na hiyo ni pamoja na kuruhusu watazamaji wa ndani na nje ya nchi ambapo hadi sasa Tume imetoa vibali kwa Asasi za kiraia na Taasisi 97 za ndani ya nchi na makundi 16 ya watazamaji kutoka nje ya nchi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano maalumu uliowakutanisha na wadau wa uchaguzi kutoka makundi mbalimbali ndani ya Mkoa huo zikiwemo Asasi za kiraia, viongozi wa dini, wawakilishi wa wanawake, vijana, waandishi wa habari na wazee wa kimila Mkurugenzi wa Ofisi ya Tume Zanzibar, Hamidu Mwanga amesema kuwa Tume imejipanga katika kusimamia uchaguzi wa mwaka huu kwa kufuata katiba ya nchi, sheria, kanuni na miongozo mbalimbali na inaamini kuwa kila mdau akitimiza wajibu wake kwa kufuata taratibu watanzania watapiga kura kwa amani siku hiyo ya uchaguzi mkuu.

"Tume inatumia nafasi hii pia kuwatoa hofu wapiga kura wote wenye mahitaji maalumu kwa kuwa maelekezo yote yametolewa kwa watendaji wa uchaguzi... maelekezo yamewataka kutoa vipaumbele kwa watu, wenye ulemavu, wajawazito, wanaonyonyesha, watakaokwenda na watoto vituoni, Wazee na wagonjwa" ameeleza.

Aidha amesema kuwa Tume imeweka mazingira bora kwa wenye ulemavu wakiwemo wa viungo ambao watatumia vituturi, wasioona watatumia kifaa cha maandishi cha nukta nundu na wasiojua kutumia kifaa hicho na wale wasiojua kusoma na kuandika wanaoruhusiwa kwenda na watu wanaowaamini kwa ajili ya kuwasaidia kupiga kura.

Amesema kuwa katika kipindi hiki cha kampeni Tume imekuwa ikisisitiza vyama vya siasa na wagombea kuzingatia maadili ya uchaguzi katika kampeni zao ikiwemo kuepuka lugha za kashfa, maneno ya uchochezi yanayotishia usalama na amani ya nchi pamoja na kufanya kampeni zinazoashiria ubaguzi katika misingi ya jinsi, ulemavu, ukabila, udini, maumbile au rangi.

Kwa upande wake Mkurugenzi msaidizi wa Elimu ya mpiga kura Monica Mnanka amesema kuwa daftari lina wapiga kura 29,188,347 ambapo wapiga kura 29,059,507 wapo Tanzania bara na 128, 840 wapo Tanzania, Zanzibar na tayari Tume imeshatoa orodha ya wapiga kura kwa wasimamizi wa uchaguzi na vyama vya siasa kwa uhakiki na rejea wakati wa uchaguzi.

Vilevile amesema kuwa Tume inawahikikishia usalama wananchi wote na wajitokeze kwa wingi siku ya Oktoba 28 na kuchagua wawakilishi wao na kurejea majumbani na kusubiri matokeo.
 
View attachment 1587965

Tume ya uchaguzi ya CCM hatuiamini kamwe.
 
Mbona neno HAKI ni dogo sana ila limekuwa gumu sana kutamkika badala yake yanatajwa matunda ya Haki tu😂😂😂😂kwanini wasiuhakikishie Umma kuwa haki itatendeka pasipo na shaka na atakaeshinda ndio atatangazwa kwa Haki kabisa
 
Tunataka tume iwakemee na kuwakamata wanaonunua shahada za kupigia kura! Pia kama kweli tume inakusudia kuendesha uchaguzi kwa haki ihakikishe mawakala wote wa vyama vya upinzani hawafanyiwi figisu za kutowemo ndani ya kituo cha kupigia kura na pia isikataze wananchi kulinda kura zao!
 
View attachment 1587965

Kwa upande wake Mkurugenzi msaidizi wa Elimu ya mpiga kura Monica Mnanka amesema kuwa daftari lina wapiga kura 29,188,347 ambapo wapiga kura 29,059,507 wapo Tanzania bara na 128, 840 wapo Tanzania, Zanzibar na tayari Tume imeshatoa orodha ya wapiga kura kwa wasimamizi wa uchaguzi na vyama vya siasa kwa uhakiki na rejea wakati wa uchaguzi.

Vilevile amesema kuwa Tume inawahikikishia usalama wananchi wote na wajitokeze kwa wingi siku ya Oktoba 28 na kuchagua wawakilishi wao na kurejea majumbani na kusubiri matokeo.

Watu 29Mil wanwezaje kupiga kuwa kwa siku moja kwenye vituo 80K ?? Huu ni wizi wa wazi.
 
Back
Top Bottom