NEC yajipanga uchaguzi ujao kuaminiwa dunia nzima

NEC yajipanga uchaguzi ujao kuaminiwa dunia nzima

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
MKURUGENZI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dk Wilson Mahera ametoa wito kwa viongozi, wadau wote wa uchaguzi kuendelea kujipanga kikamilifu kuhakikisha uchaguzi ujao unakuwa bora, mzuri na kuaminika katika jamii na ulimwenguni kote.

Alisema hayo juzi wakati akifungua kikao cha wadau wa uchaguzi kujadili na kuchangia taarifa ya uchaguzi 2020, kilichoandaliwa na Kituo cha Amani Haki na Msaada wa Kisheria Tanzania (PLAJC). "Tanzania ni nchi yenye misingi ya demokrasia inayozingatia sheria, ni imani yangu mapendekezo yatakayotokana na kikao hiki yatajielekeza katika kuboresha na kuimarisha demokrasia nchini na hatimaye kukuza na kudumisha umoja na mshikamano wa kitaifa," alisema.

Alisema uchaguzi ni muhimu katika nchi kwani unaashiria kukua na kukomaa kwa demokrasia katika nchi, kupitia uchaguzi wananchi hupata fursa na kuchagua viongozi wanaowataka kwa hiari.

“Kwa upande mwingine uchaguzi unawafanya viongozi waliochaguliwa kufanya kazi kwa kujiamini kwa kuwa wana ridhaa ya wananchi wanaowaongoza.
Pamoja na ukweli huo ili uchaguzi ukidhi malengo hayo ni lazima usimamiwe vizuri na kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na haki,” alisema.

Mwenyekiti wa PLAJC, Leatitia Petro alisema kikao hicho ni kwa ajili ya kujadili na kuchambua taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 ya NEC pamoja na taarifa mbalimbali za wadau wa ndani na nje waliopewa vibali na tume kuangalia uchaguzi mkuu 2020.

Alipongeza serikali kwa kugharamia shughuli za uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kwa asilimia 100.

Pia alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kujenga mazingira wezeshi kwa taasisi zisizo za kiserikali kuendelea kufanya kazi za kuleta maendeleo kwa wananchi.
 
Huyo Mahera ni mnafiki mkubwa. Ndiye kwa kushirikiana na marehemu wakaweka huu uchafu wotebtulio nao leo huko Bungeni na kwenye halmashauri.

Jambazi tangu lini akawa mshauri wa kuzuia ujambazi? Mahera nibtakataka katika dunia ya wastaarabu.
 
MKURUGENZI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dk Wilson Mahera ametoa wito kwa viongozi, wadau wote wa uchaguzi kuendelea kujipanga kikamilifu kuhakikisha uchaguzi ujao unakuwa bora, mzuri na kuaminika katika jamii na ulimwenguni kote.
Huyu huyu aliyekuwa anampigia debe jpm wazi wazi eti "watu wanataka kusikia utalindaje rasilimali" na siyo blabla as if ameshikilia mawazo ya watu. Sijui yeye aliwatembelea watu saa ngapi akajua watu wanataka kusikia Nini. Hili li mahela mama alitoe linaharibu uchaguzi makusudi kisa ni li ccm
 
MKURUGENZI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dk Wilson Mahera ametoa wito kwa viongozi, wadau wote wa uchaguzi kuendelea kujipanga kikamilifu kuhakikisha uchaguzi ujao unakuwa bora, mzuri na kuaminika katika jamii na ulimwenguni kote.

Alisema hayo juzi wakati akifungua kikao cha wadau wa uchaguzi kujadili na kuchangia taarifa ya uchaguzi 2020, kilichoandaliwa na Kituo cha Amani
Huyu mjinga kwa kweli hana hata aibu kuongea mbele ya watu .... Sasa hapo inajaribu kukubali kuwa uchaguzi uliopita haukuaminiwa duniani.
 
K
Tangulini wakaheshimu chaguo la wananchi?? Au anajipendekeza Kwa Hangaya??
MKURUGENZI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dk Wilson Mahera ametoa wito kwa viongozi, wadau wote wa uchaguzi kuendelea kujipanga kikamilifu kuhakikisha uchaguzi ujao unakuwa bora, mzuri na kuaminika katika jamii na ulimwenguni kote.

Alisema hayo juzi wakati akifungua kikao cha wadau wa uchaguzi kujadili na kuchangia taarifa ya uchaguzi 2020, kilichoandaliwa na Kituo cha Amani
Kwa uchafuzi wa 2019/2020 kujiosha labda watumie bleach, ili hata Dunia iwaone wasafi
 
Sisi tutazidisha maombi kwa watesi wetu nayo yatajibiwa kadri ya mapenzi yake
 
Huyo Mahera ni mnafiki mkubwa. Ndiye kwa kushirikiana na marehemu wakaweka huu uchafu wotebtulio nao leo huko Bungeni na kwenye halmashauri.

Jambazi tangu lini akawa mshauri wa kuzuia ujambazi? Mahera nibtakataka katika dunia ya wastaarabu.
Kila aliyeshiriki kuhujumu maamuzi ya Watanzania kwenye uchafuzi wa 2020 ni lazima Mungu atamchapa hapahapa duniani.

Huyu siku si nyingi mtasikia tunkama siyo stroke, basi lolote baya na liwe juu yake Amen.
 
Ngoja waendelee tu kuchezea akili za watu. Ipo siku watatafuta mahali pa kwenda kujificha baada ya watu kuchoshwa na uonevu wao.
 
Back
Top Bottom