Uchaguzi 2020 NEC yataka vyama vya siasa viwe na subira

Uchaguzi 2020 NEC yataka vyama vya siasa viwe na subira

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imevitaka vyama vya siasa nchini viwe na subira na viiache tume hiyo itekeleze majukumu yake kwa mujibu wa taratibu za uendeshaji wa uchaguzi.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk Wilson Mahera, ilisema orodha ya vituo vya kupigia kura itatolewa kwa vyama siasa siku 14 kabla ya siku ya kupiga kura.

Alisema kwa kuzingatia masharti ya kanuni ya 50 (1) ya uchaguzi wa Rais na wabunge ya mwaka 2020, wasimamizi wa uchaguzi watavipatia vyama vya siasa orodha ya vituo vya kupigia kura ili vyama vipange mawakala na kuwasilisha majina ya mawakala hao kwa kila kituo ndani ya siku saba kabla ya siku ya kupiga kura.

Dk Mahera pia alieleza kanuni ya 37 ya kanuni za uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura za mwaka 2018 zinaelekeza kuwa, tume inaweza kuvipatia vyama vya siasa nakala ya daftari hilo kwa ajili ya utambuzi wa wapigakura wanaoingia katika kituo cha kupigakura.

“Ifahamike bayana kuwa muda ulioainishwa kikanuni wa kuvipatia vyama nakala ya daftari na orodha ya vituo vya kupigia kura bado haujafika,” alisema.

Dk Mahera alieleza kuwa kalenda ya utekelezaji wa shughuli za uchaguzi inaonesha kuwa siku 14 kabla ya uchaguzi ni jana Oktoba 14, 2020.
 
Bwana Manoti - kwa mustakabala mwema wa nchi yetu, ungejiuzulu jombi.

Kuwepo kwako katika tume hii kunaipaka sana tume matope kama si mali kabisa!
 
Sasa yeye mwenyewe anakiri kuwa kwa mujibu wa sheria ni jana, alafu anasema tena wawe na subira
 
Back
Top Bottom