Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,931
- 24,816
Tumeona kwa macho yetu baadhi ya watu wanaojiita wana CCM wakijaribu kuhujumu uchaguzi huu. Tumeona ambavyo wanaonekana wakiwa na kura fake ambazo wanataka kuzichanganya na halisi.
Hawa ni wahujumu, wahujumu na wafitini ambao wanataka kuonesha kuwa Mh. Rais hatakiwi na hawezi shinda hivi hivi mpaka kura ziibwe au zichakachuriwe.
Hawa wana nia ya kumfitinisha Mh. Magufuli na Polepole ambaye aliwahi sema bila kuiba kura CCM haiwezi shinda. Sisi tunataka uchaguzi huru na wa haki ili Dunia nzima ione kuwa Magufuli anapendwa.
Sasa inapoonekana kuna kura za maruhani ni kuonesha kuwa Rais Maguful hapendwi ila anaiba kura. Hili ni jambo la kulikataa kata kata.
NEC toeni tamko na wahusika wafunguliwe kesi za Uhujumu uchumi. ZEC toeni Tamko mkemee jambo hili.
Tunategemea CCM iseme kuwa hizo kura haizitaki na haizikubali yale maeneo yenye ukengeufu yarudiwe ili chama chetu kishinde kwa uhalali.
Anayehujumu uchaguzi kwa kura huyo ni mfitini na mhujumu. Huyo anampaka matope Magufuli. Akamatwe ashtakiwe. CCM tusikubali kura za wizi. Kwani hatuwezi shinda bila hizo?