NECTA haijafanya madudu upangaji wa matokeo ya ACSEE 2014

Hivi kwa nini marobot ya CCM hapa JF hayajadili habari kama hizi?
 
Subirini 2015 tutakapo pata Katiba mpya na Serikali makini yenye viongozi makini....Huu uozo ambao Serikali ya MAPEPO CCM inatufanyia katika Elimu yetu sasa unakaribia ukomo...Serikali ya Kishetani ipo radhi kuangamiza Taifa ili mapepo yendelee kutawala....

NAsubiria kwa hamu Daftari jipya la Kura...
 
serikali ya CCM imeamua kucheza na elimu ambayo n mapigo ya moyo wa taifa hili.
sina shaka huu ni mpango maalumu wa CCM kuazalisha jamii yenye elimu duni ili iwe easy kuwafanyia brain wash kuwatawala.

Nina hasira kali sana na hii Serikali ya MAPEPO ya CCM.... Hivi kwanini Mungu anaangalia haya yanotokea...? Kwann aliruhusu kutupa Shetani JK...Kwanini kwanini kwanini????
 
Kwanini Watanzania tunarusu MAPEPO yachezee Elimu yetu...? Tutaruhusu haya mpaka lini..? Je! Ni nani aliyetuloga na kutupumbaza kiasi hiki...?
 
Vasco Da Gama anazeeka vizuri,mwacheni weee ...mwakani hawa failure watamwadhibu na chama chake kwenye kura,badala alete wanasayansi na academicians wengine analete wahuni wa Marekani waje kufundisha muziki kwa Akina diamond wasiolipa kodi kwa shoo zao huku walala hoi wakilipishwa,mswahili kumpa nchi imekuwa kazi kweli kweli
 
acha porojo wewe!
A ya kipindi chetu ilikuwa 81-100
A ya sasa 71-100
 
Toa ushahidi wa hayo unayoongea... mimi nakupa Barua ya Wizara 2013; nanukuu "Katika mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012 Baraza lilitumia mfumohuu wa alama mgando ambapo: A = 80 – 100, B = 65 – 79, C = 50 – 64, D = 35 – 49, F = 0 – 34. Kwa upande wa Kidato cha Sita Baraza lilitumia mfumo wa A = 80 – 100; B = 75 - 79; C = 65 – 74; D = 55 – 64; E = 45 – 54; S = 40 – 44 na F = 0 – 39". Kisha hapa tena:"Muundo huu mpya wa alama utatumika kwa mzunguko wa miaka minne kabla haujahuishwa tena ili kuupa muda wa kutosha kuona aina ya changamoto zinazojitokeza na jinsi ya kuzishughulikia..." Kwa mantiki hii, viwango vya alama na ufaulu ni kama inavyooneshwa kwenye jedwali la 1 hapa chini: A=75 - 100, B+ 60 - 74 B=50- 59 10, C=40 - 49 10, D=30 - 39, E=20 - 29 , F=0 - 19. Source: http://www.moe.go.tz/index.php?option=com_docman&task=doc_download&gid=305&Itemid=622. Kama device unayotumia haiwezi ku-download PDF document, basi soma hapa: TAARIFA MUHIMU: SERIKALI YATANGAZA VIWANGO VIPYA VYA ALAMA ZA UFAULU ELIMU YA SEKONDARI‏ | EDDY BLOG .


Sasa basi, tumchukue huyo wa CCD ambae umetolea mfano. Huyo amepata C na range ya ufaulu wake ni 40-49 kama ulivyosema. Sasa basi, angalia hiyo 40-49 kwa mwaka 2012 inaingia wapi... kwa kuangalia barua ya wizara. Sidhani kama panahitaji utaalamu kufahamu kwamba hiyo 40-49 ambayo ni C (2014), inaangukia ama kati ya S = 40 – 44 au kwenye E = 45 – 54 bHivyo basi, kwa kutumia grading za 2012, hiyo C ingekuwa ama E or S! Una lingine?
 

Kwa Hiyo Wewe Ulitaka Wafeli Kama Mwaka Jana Au Sio..Kufeli Kwa Watu Sio Kupanda Kwa Elimu..Mbona 2012 Watu Walifaulu sana tu. Na Grade Zilizotumika Ni A 75-100 B 65-74 C 55-64 D 45-54 E 35-44 S. 25-34 F 0-24....
Kufeli Kwa Mwaka Jana Usiwahukumu wa mwaka huu na kumbuka form6 wa mwaka huu walifaulu vizuri form4 2011 tofauti na form6 wa mwaka jana waliofanya mtihani wa form4 2010
 
We vipi?????!!! Mie nimeleta suala lingine kabisa, wewe ukaniambia naongea bila utafiti... nakupa reference ya wizara, unageuka unasema nilitaka wafeli... hoyaaa, we vipi???!!! Kama umeshau, hoja yako hii hapa:
kwa hyo usikurupuke fanya kwanza utafiti ndo uandke humu sawa mkuuu.
Sasa je, naandika kwa kurupuka, au?
 
We vipi?????!!! Mie nimeleta suala lingine kabisa, wewe ukaniambia naongea bila utafiti... nakupa reference ya wizara, unageuka unasema nilitaka wafeli... hoyaaa, we vipi???!!! Kama umeshau, hoja yako hii hapa: Sasa je, naandika kwa kurupuka, au?

Basi Hapo Kosa Walifanya Mwaka Jana Kuwafelisha Lakini Kwa Mwaka Huu Wapo Sawa Na Miaka Mingine Kutokea 2012....
 
Nimeangalia Tabora Boys, hakuna A ya Phisics kabisa,ina maana Tanzania nzima hakuna
 
Sijakuelewa una maana gani ukisema hawa ni sawa na 2012. Mwaka 2012 hapakuwa na B+ na Div I ilianzia pointi 3-9 lakini mwaka huu inaanzia 3-7, vitu vingi ni tofauti sasa huo usawa ni upi hapo. Unajitesa bure kutetea u....zi wakati kila aliye na akili timamu anaona kabisa kuwa NECTA imechakachua matokeo kwa kivuli cha viwango vipya vya upangaji wa madaraja

Basi Hapo Kosa Walifanya Mwaka Jana Kuwafelisha Lakini Kwa Mwaka Huu Wapo Sawa Na Miaka Mingine Kutokea 2012....
 

Kwa iyo Unataka kusemaje?? wa mwaka huu hawajafaulu kiualali au?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…