NECTA haijafanya madudu upangaji wa matokeo ya ACSEE 2014

let

New Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
3
Reaction score
2
Pointi za Mtihani wa ACSEE zimepangwa kama ifuatavyo:- Division 1 ni kuanzia 3-7, Division 2 kuanzia 8- 9, Division 3 kuanzia 10-13, Division 4 Mtahiniwa anatakiwa angalau awe amepata D mbili au Principal Pass moja isiyopungua C, na Division 0 ni Mtahniwa aliyepata ufaulu chini ya D mbili.

Matokeo ni kuwa mtahiniwa anakokotoa idadi ya pointi zake katika masomo matatu ya tahasusi (combination). Mfano mtahiniwa akiwa na comb. ya PCB/BAM, GS point zake zitapatikana kwenye masomo ya PCB na sio BAM au GS. Point za BAM na GS hazijumuishwi au hazikokotolewi.

Hivyo masomo matatu ya comb. Ndiyo yanayotoa idadi ya point na division na si vinginevyo. Hata hivyo masomo ya Arabic na I/knowledge kwa Z'bar yana comb na yanatumika kujenga idadi ya pointi wakati kwa upande wa Bara hayatumiki wakati wa kupata idadi ya pointi.

Lakiki Arabic mbona ni somo la lugha kama Kiswahili na English au ndo kusema mfumo galatia... Hahahaha
 
Ninachokiona hapa ni mkakati wa serikali kupunguza watu wanaoingia vyuo vikuu.
 
msitake kutufundisha ujinga wenu; haiweezekani matokeo yabadilike kwa kiwango kikubwa hivi ndani ya mwaka mmoja. hii ni njia ya kutaka kutudanganya kwamba BRN inamafanikio.
 
Matokeo ya Somo la Physics Form 6 hakuna A Tanzania nzima,Je ni kweli?
 
Ninachokiona hapa ni mkakati wa serikali kupunguza watu wanaoingia vyuo vikuu.
Nahisi wana mkakati wa kukamatia watu kwenda Ualimu huku wakionekana na jamii kwamba wana sifa za kuingia Ualimu wakati sio!!! Unaweza kukuta mtu amepata III, say ya 13. Mtu kama huyo, kwa zamani angekuwa na IV isiyo na mvuto. Kuna uwezekano TCU wasimchukue huyo wa III ya 13, but akienda Ualimu, kila mmoja ( I mean Watanzania) tutaona walioenda Ualimu wana sifa bora kabisa... wote wamepata III, kwa sababu katika hiyo III ya 13, unaweza kuta ndani yake kuna C na B !!!!!! BRILLIANT...
 
Haya tumekuelewa subirini baada ya miaka minne kupata kazi
 
Vijana wa mwaka huu wana akili maradufu ya wenzao wa mwaka jana ukijumlisha na wa mwaka juzi.
 
Nahisi wana mkakati wa kukamatia watu kwenda Ualimu huku wakionekana na jamii kwamba wana sifa za kuingia Ualimu wakati sio!!! Unaweza kukuta mtu amepata III, say ya 13. Mtu kama huyo, kwa zamani angekuwa na IV isiyo na mvuto. Kuna uwezekano TCU wasimchukue huyo wa III ya 13, but akienda Ualimu, kila mmoja ( I mean Watanzania) tutaona walioenda Ualimu wana sifa bora kabisa... wote wamepata III, kwa sababu katika hiyo III ya 13, unaweza kuta ndani yake kuna C na B !!!!!! BRILLIANT...

Na Upolisi

huku ni kuharibiana muelekeo wa kimaisha kwa kweli.
 
Nahisi wana mkakati wa kukamatia watu kwenda Ualimu huku wakionekana na jamii kwamba wana sifa za kuingia Ualimu wakati sio!!! Unaweza kukuta mtu amepata III, say ya 13. Mtu kama huyo, kwa zamani angekuwa na IV isiyo na mvuto. Kuna uwezekano TCU wasimchukue huyo wa III ya 13, but akienda Ualimu, kila mmoja ( I mean Watanzania) tutaona walioenda Ualimu wana sifa bora kabisa... wote wamepata III, kwa sababu katika hiyo III ya 13, unaweza kuta ndani yake kuna C na B !!!!!! BRILLIANT...

Unaongea kwa ujasili kabisa eti huyo wa III 13 angekua na four mbaya zamani.umefanya uchunguzi au unaandika tuh..kwa mfano mtu mwenye CCD huyo ndo atakua na III13 C ya mwaka huu inaanzia 40-49 na D inaanzia 30-39 sasa hapo kapata C mbili inamaan mwaka jana angekua na D mbili ambazo zingekua point 4 afu hyo D ingekua E ambayo ingekua tano kwa hyo angekua na three nzuri tu.kwa hyo usikurupuke fanya kwanza utafiti ndo uandke humu sawa mkuuu.
 
MAMA JOYCE NDALICHAKO ulistahili kuwepo pale necta, kabisa nina imani na wewe, haa ulowaacha wamefanya nini sasa,
 
Pointi za Mtihani wa ACSEE zimepangwa kama ifuatavyo:- Division 1 ni kuanzia 3-7, Division 2 kuanzia 8- 9, Division 3 kuanzia 10-13, Division 4 Mtahiniwa anatakiwa angalau awe amepata D mbili au Principal Pass moja isiyopungua C, na Division 0 ni Mtahniwa aliyepata ufaulu chini ya D mbili.

Matokeo ni kuwa mtahiniwa anakokotoa idadi ya pointi zake katika masomo matatu ya tahasusi (combination). Mfano mtahiniwa akiwa na comb. ya PCB/BAM, GS point zake zitapatikana kwenye masomo ya PCB na sio BAM au GS. Point za BAM na GS hazijumuishwi au hazikokotolewi.

Hivyo masomo matatu ya comb. Ndiyo yanayotoa idadi ya point na division na si vinginevyo. Hata hivyo masomo ya Arabic na I/knowledge kwa Z'bar yana comb na yanatumika kujenga idadi ya pointi wakati kwa upande wa Bara hayatumiki wakati wa kupata idadi ya pointi.

NONE SENSE
mbona hujasema hayo madaraja na alama zake....
utakuta D ni 15% alafu unajisifu UFAULU UMEPANDAA... NONE SEEEEEEEENSE.
 
serikali ya CCM imeamua kucheza na elimu ambayo n mapigo ya moyo wa taifa hili.
sina shaka huu ni mpango maalumu wa CCM kuzalisha jamii yenye elimu duni ili iwe easy kuwafanyia brain washing kuwatawala.
 
Ukisikia kichwa cha mwendawazimu ndiyo elimu ya Tanzania. Kila mtu anaichezea anavyotaka halafu eti kuanzia Kidato cha 4, 2014 wanatumia GPA. Tatizo siasa imeingia sana NECTA sijui kama Prof Mukandala Mwenyekiti wa bodi ya NECTA anajua maana ya ufaulu wa F6 ambao umetangazwa.

Ukisema ufaulu imeimarika maana yake nini nini wakati mwaka jana aliyepata BBC alikuwa na Div I pt 8 lakini mwaka huu BBC ni div III pt 10. Sasa hapa uimara uko wapi? Mbona vigezo ni tofauti sana kiasi kuwa haikustahili hata kulinganisha ns mwaka jana? Au NECTA hawaoni hilo?
 
Back
Top Bottom