NECTA huwa wanasahihishaje mitihani yao? Nimepata mashaka ya alama za ufaulu wa wadogo zangu

Paploman

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2019
Posts
1,759
Reaction score
3,452
Nina wadogo na ndugu zangu watano waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana ambao matokeo yao yametoka mapema mwaka huu.

Kati ya wadogo zangu watano watatu wamepata daraja la kwanza na mmoja wao amepata daraja la kwanza la alama 10 kati ya masomo kumi aliyofanya amepata A's 4 za masomo ya Phys, Maths, Chemis na Bios na masomo mengine 6 amepata B zote, na waliobaki wamepata point 12 na 14 na wote wakiwa na A za Hesabu na Physics. na wengine wakiwa na daraja la pili.

Kwa vile mara nyingi nikipata muda huwa nawafundisha na kuwapa mitihani ya majaribio nilipata ukakasi kidogo na haya matokeo japo nilijua lazima watafaulu ila sio kwa ufaulu wa kiwango hiki, maana enzi za miaka yetu ya 2000 kurudi nyuma ukimkuta kijana amepata one uwezo wake kweli unajieleza bila mashaka.

Hapa ninapokaa nipo karibu na shule ya private na huwa wanatoa tuisheni za masomo ya practical na kwa vile mhusika nafahamiana nae nikamuomba atafute mitihani ya practical ya mwaka jana ya Physics na Chemistry na aandae ratiba ili niwalete wale ndugu zangu wafanye, na pia nikazitafte mitihani ya theory na Physics na Chemistry pia na Mathematics nikaandaa walimu wangu wawili ambao ni marafiki zangu tusimamie ile mitihani na kusahihisha. Hii mitihani ilifanyika kwa siku 3 ina maana wale wadogo zangu walirudia kufanya mitihani waliofanya mwezi November mwaka jana.

Matokeo yake sasa mdogo wangu aliepata one ya 10 na A's 4 za masomo ya sayansi alipata B ya Maths tu halafu mengine yote C, na wote wengine waliobaki walipata alama C katika masomo yote, japo na wao walikuwa na A katika masomo haya.

Hapa nikapata swali, NECTA wao huwa wanasahihishaje, maana binafsi kwa hawa wadogo zangu walipaswa kufaulu ila sio kwa alama hizi za ufaulu walizonazo.
 
Inawezekana sio NECTA ila walipigwa boost na shule, husikiagi shule zinatangazwa redioni zinafaulisha, mbinu wanazotumia wanajua wenyewe, ila kikubwa wanafaulisha, hata vilivyoshindikana kufaulu zitafaulishwa.😂😂😂😂😂😂
Mkuu hawa walikuwa shule za Kata
 
Vipi wamevunja record yako? Mimi kijana wangu amekosa moja afikie record yangu. Nimechukua sana maana mazingira yake ya kusoma ni rafiki zaidi kuliko niliyosomea mimi; yeye ni seminari boarding mimi nilisoma day
 
Huyu wa one ya 10 amevunja mkuu lakini uwezo wake na ufaulu wak

Huyu wa point 10 kavunja mkuu, tatzo ni ufauli na upeo wake haviendani
 
".. Tatizo ni ufaulu na upeo wake haviendani"
Hapa huwa kuna equations zinatumika mwenye uelewa anakatwa maana ataweza kuishi bila maganda na asiye atapita maana hatoweza kuishi bila maganda.

Hiyo ndio Ndalichako's Law
 
Ulifanya yote hayo ili ugundue nini? Alafu ukishagundua?

Basi usiwapeleke form five. Watafutie vitu vingine vya kufanya kwa sababu hawakufaulu form fooo. Wafundishe cherehani
 
Nina wadogo na ndugu zangu watano waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana ambao matokeo yao yametoka mapema mwaka huu.

Kati ya wadogo zangu watano watatu wamepata daraja la kwanza na mmoja wao amepata daraja la kwanza la alama 10 kati ya masomo kumi aliyofanya amepata A's 4 za masomo ya Phys, Maths, Chemis na Bios na masomo mengine 6 amepata B zote, na waliobaki wamepata point 12 na 14 na wote wakiwa na A za Hesabu na Physics. na wengine wakiwa na daraja la pili.

Kwa vile mara nyingi nikipata muda huwa nawafundisha na kuwapa mitihani ya majaribio nilipata ukakasi kidogo na haya matokeo japo nilijua lazima watafaulu ila sio kwa ufaulu wa kiwango hiki, maana enzi za miaka yetu ya 2000 kurudi nyuma ukimkuta kijana amepata one uwezo wake kweli unajieleza bila mashaka.

Hapa ninapokaa nipo karibu na shule ya private na huwa wanatoa tuisheni za masomo ya practical na kwa vile mhusika nafahamiana nae nikamuomba atafute mitihani ya practical ya mwaka jana ya Physics na Chemistry na aandae ratiba ili niwalete wale ndugu zangu wafanye, na pia nikazitafte mitihani ya theory na Physics na Chemistry pia na Mathematics nikaandaa walimu wangu wawili ambao ni marafiki zangu tusimamie ile mitihani na kusahihisha. Hii mitihani ilifanyika kwa siku 3 ina maana wale wadogo zangu walirudia kufanya mitihani waliofanya mwezi November mwaka jana.

Matokeo yake sasa mdogo wangu aliepata one ya 10 na A's 4 za masomo ya sayansi alipata B ya Maths tu halafu mengine yote C, na wote wengine waliobaki walipata alama C katika masomo yote, japo na wao walikuwa na A katika masomo haya.

Hapa nikapata swali, NECTA wao huwa wanasahihishaje, maana binafsi kwa hawa wadogo zangu walipaswa kufaulu ila sio kwa alama hizi za ufaulu walizonazo.
Usiwachukulie poa madogo wapo bright na material siku hizi nje nje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vijana wamejituma vyema na wamevunja rekodi yako na sasa unaikasirikia necta! Mitihani yenyewe unayosema division one zilikua adimu si ndio ile ya swali la hesabu linakua na vipengele viwili, vifupi na vilivyo wazi? Ifike pahali tukubali tu kwamba vijana wetu wa sasa wanajituma sana katika masomo.
 
Ni kweli unayoongea. Kuna Dogo hata Mimi nilikua najua anapata zero, lakini kapata 3 ya 25 na huku uwezo wake ni Mdogo.

Kiufupi matokeo ya siku hizi yapo kisiasa, hata ukiongea na wanaosahihisha necta watakuambia.
 
Hakuna kujituma. Goli limepanuliwa utashindwaje kufunga? We mugoli huo macho yako yanashindwa kulenga? Unafuatilia aina ya Maswali wanayopewa? Unajua mpangilio wa alama Kwa madaraja A-F? Kila kitu cha zamani ni classic! Aliyemaliza darasa la nne ya Mkoloni/ beberu mweupe ataendelea kuwa juu kuliko aliye na Degree ya sasa.
Vijana wamejituma vyema na wamevunja rekodi yako na sasa unaikasirikia necta! Mitihani yenyewe unayosema division one zilikua adimu si ndio ile ya swali la hesabu linakua na vipengele viwili, vifupi na vilivyo wazi? Ifike pahali tukubali tu kwamba vijana wetu wa sasa wanajituma sana katika masomo.
 
Hakuna kujituma. Goli limepanuliwa utashindwaje kufunga? We mugoli huo macho yako yanashindwa kulenga? Unafuatilia aina ya Maswali wanayopewa? Unajua mpangilio wa alama Kwa madaraja A-F? Kila kitu cha zamani ni classic! Aliyemaliza darasa la nne ya Mkoloni/ beberu mweupe ataendelea kuwa juu kuliko aliye na Degree ya sasa.
Mindset za kikapuku kama hizi ndizo zinazowachelewesha! Madaraja ya sasa yanafahamika na madaraja ya kale yanafahamika. Kama hiyo haitoshi, past paper za kale zipo hata leo na za sasa zipo pia. Tukubali tu kwamba vijana wanajituma na ndio maana dunia inazidi kua bora kisayansi na kiteknolojia kadri siku zinavyo songa. Vijana wameibua chachu ya ushindani kwa kila nyanja kwa sasa kuliko ilivyokua hapo kale. Kama ushindani huu umekushinda, ondoka duniani uwapishe wanaoweza kushindana na kuhimili mikiki mikiki ya kileo. Wape kongole vijana. Usiwe kama wale wapuuzi wanaolinganisha vi credit vyao vitatu na na misonge 7 ya vijana. Jumapili njema.
 
Mkuu unakuwa kama hujawahi kuwa mwanafunzi (samahani kama nitakukwaza). Kwanza tambua kuwa mfumo wetu elimu umejikita kwenye kukariri zaidi hivyo basi mitihani inapokaribia wanafunzi wanakuwa kwenye higher alert ya kukariri material ili wayabwage kwenye mtihani. Kwa wanafunzi wale ambao ni wazuri wa kukariri wakikaribia mtihani huwa ni wanafunzi ambao kama wanakosa furaha hivi. Hiyo husabishwa na ubongo wao kuko ncetrate zaidi na kukariri material hivyo kuupunguzia ubongo kubeba vitu ambavyo havinatija kwa wakati huo maana material yao huwa yametunzwa kwenye short memory hivyo usumbufu wowote utakaojitokeza ndani ya muda huo utamharibia sana. Na hii ni kwa sababu huwa wanasoma sana wanapokaribia kufanya mtihani maana hawana uwezo wa kutunza material yao kwa muda mrefu kwenye ubongo wao. Sasa hawa watu wa namna hiyo mtihani ukiisha tu huwa wanasahau haraka sana.

Lakini naomba tu nikwambia kuwa kila mtu anambinu zake za kusoma, madogo wameonesha juhudi wamefaulu vizuri na ninaamini kabisa kufaulu kwao vizuri ni kitu ulichokihitaji sana. Kwa hiyo waandalie ada waende kidato cha tano na mwisho wa siku kidato cha sita wakushangaze zaidi.
 
Back
Top Bottom