Nina wadogo na ndugu zangu watano waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana ambao matokeo yao yametoka mapema mwaka huu.
Kati ya wadogo zangu watano watatu wamepata daraja la kwanza na mmoja wao amepata daraja la kwanza la alama 10 kati ya masomo kumi aliyofanya amepata A's 4 za masomo ya Phys, Maths, Chemis na Bios na masomo mengine 6 amepata B zote, na waliobaki wamepata point 12 na 14 na wote wakiwa na A za Hesabu na Physics. na wengine wakiwa na daraja la pili.
Kwa vile mara nyingi nikipata muda huwa nawafundisha na kuwapa mitihani ya majaribio nilipata ukakasi kidogo na haya matokeo japo nilijua lazima watafaulu ila sio kwa ufaulu wa kiwango hiki, maana enzi za miaka yetu ya 2000 kurudi nyuma ukimkuta kijana amepata one uwezo wake kweli unajieleza bila mashaka.
Hapa ninapokaa nipo karibu na shule ya private na huwa wanatoa tuisheni za masomo ya practical na kwa vile mhusika nafahamiana nae nikamuomba atafute mitihani ya practical ya mwaka jana ya Physics na Chemistry na aandae ratiba ili niwalete wale ndugu zangu wafanye, na pia nikazitafte mitihani ya theory na Physics na Chemistry pia na Mathematics nikaandaa walimu wangu wawili ambao ni marafiki zangu tusimamie ile mitihani na kusahihisha. Hii mitihani ilifanyika kwa siku 3 ina maana wale wadogo zangu walirudia kufanya mitihani waliofanya mwezi November mwaka jana.
Matokeo yake sasa mdogo wangu aliepata one ya 10 na A's 4 za masomo ya sayansi alipata B ya Maths tu halafu mengine yote C, na wote wengine waliobaki walipata alama C katika masomo yote, japo na wao walikuwa na A katika masomo haya.
Hapa nikapata swali, NECTA wao huwa wanasahihishaje, maana binafsi kwa hawa wadogo zangu walipaswa kufaulu ila sio kwa alama hizi za ufaulu walizonazo.
Kuna tofauti kidogo jinsi matokeo ya mwisho ya kidato cha nne yanavyokokotolewa, ukiona mwanao kapata A au B sio kwamba hiyo A kaipata kwa marks za mtihani huo wa siku hiyo ya mwisho tu,hapana! Kuna kitu kinaitwa continued assessment ambapo kuna alama mwanafunzi anachukuliwa kutoka kwenye matokeo ya mock na yale ya mihula rasmi shuleni kisha yanaongezwa kwenye hizi alama alizopata mwishoni then ndio alama ya matokeo ya jumla inapatikana. Kwa hiyo kwa swala la hao watoto ulivyowapima hapo umekosa kuwawekea alama continued assessment zingekuwepo ungekuta huyo aliyepata B ingerudi A na hao wa C ungekuta B au hata A.