Necta inahusika kwa matokeo haya!!!

Necta inahusika kwa matokeo haya!!!

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
24,225
Reaction score
22,632
Wandugu, baada ya kivumbi cha Arusha kutulia, ngoja sasa turejee kwenye mambo ya msingi huku tukisubiri tukio jingine litokee, maana hii nchi kwa matukio haina mfano!
Ni sababu hiyo hiyo ya matukio yasiyoisha iliyotupelekea kusahau kwa haraka matokeo mabaya kabisa ya kidato cha nne, 2012, matokeo ambayo hayajawahi kutokea tangu nchi hii ipate uhuru kutoka kwa wakoloni wa kiingereza mnamo 1961.

Pamoja na sababu nyingi zilizochangia kushuka kwa ufaulu, baraza la mitihani (NECTA) hawawezi kukwepa lawama, hata kama tayari wameishatetewa na watu mbali mbali. Ninasema hili nikiwa na ushahidi ili na mimi nisije nikashurutishwe na Bw Jagonja kuwapelekea polisi ushahidi wangu.

Nimepitia mitihani yote ya kidato cha nne, 2012 nikailinganisha na mitihani iliyotangulia nikagundua kwamba mitihani ya mwaka 2012 ilitungwa kwa mfumo tofauti na mitihani iliyotangulia. Mitihani hii ya mwaka 2012 imetungwa kwa mfumo wa kujieleza zaidi. Maswali karibu yote (hata yale yasiyokuwa ya essay) yanamtaka mwanafunzi kueleza kwa marefu majibu yake. Nyingi ya keywords zilizotumika kuuliza maswali ni kama vile: explain, describe, give a detailed account of, comment on, write an essay on, elaborate, substantiate, evaluate, etc. Keywords za aina hii zinapotumika kuuliza maswali maana yake ni kwamba mtahiniwa anatakiwa kueleza swali lake kwa urefu na kwa upana kweli kweli.

Katika mitihani ya mwaka 2012, kulikuwa na maswali machache sana yanayowataka wanafunzi kuorodhesha (list), kutaja (mention), kueleza kwa ufupi (outline), kufupisha (summarize), kupambanua kwa ufupi (define) na maswali mengine kama hayo. Maswali karibu yote yalikuwa ni ya kujieleza kwa urefu na kwa ufasaha. NECTA walifanya hivi kwa maskusudi huku wakijua kwamba uwezo wa wanafunzi wetu wa shule za sekondari ni mdogo sana. Sasa hii maana yake ni nini kama sio kulenga kuwafelisha watoto kwa makusudi?

Sina shaka mtakuwa mnafahamu kwamba wanafunzi wengi wa shule za kata wanaingia sekondari wakiwa hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu! Kama hali ndiyo hiyo basi, inawezekanaje NECTA iwatungie wanafunzi hawa mitihani ya kujieleza kwa lugha ya kimombo wakati hata Kiswahili chenyewe hawajui kukisoma wala kukiandika? Je, walitegemea wanafunzi wafeli halafu ndipo wanasiasa waingilie kati kuchakachua matokeo?

Ndiyo maana watu wenye busara wakashauri kwamba ingekuwa bora mitihani ikarudiwa kuliko kuchakachua matokeo peke yake. Wanasiasa walitakiwa kuchakachua hadi mfumo na staili iliyotumika kuuliza maswali. Huwezi kuchakachua matokeo tu ukaacha kuchakachua maswali ya mitihani yaliyozaa hayo matokeo. Kama vile wanasiasa walivyojitetea kwamba wanachakachua matokeo ili kwamba “matokeo yalingane na juhudi za kila mwanafunzi”, walipaswa warudi nyuma zaidi hadi kwenye mitihani yenyewe.

Kana kwamba hilo halitoshi, mitihani yenyewe iliyotungwa haieleweki na wala haikutungwa kwa kutumia lugha nyepesi. Lugha iliyotumika katika mitihani ni ngumu sana. Lengo la maswali ya mitihani sio kumkomoa mwanafunzi bali ni kumpima uelewa wake katika mambo aliyojifunza kwa miaka minne. Mitihani haipawsi kupima uwezo wa mwanafunzi kuelewa maswali bali ni kumpima uwezo na kiwango chake cha uelewa wa maarifa aliyojifunza. Ndio maana lugha ya mtihani inatakiwa iwe rahisi na irahisishwe kadri itakavyowezekana ili mtahiniwa aweze kuelewa maswali barabara na kuyajibu kwa ufasaha. Kwa bahati mbaya, watunzi wengi wa mitihani wana tabia ya kutunga maswali ya kimitego, kwa kutumia lugha ngumu na tata ili kuwafanya wanafunzi washindwe kuelewa maswali, hivyo washindwe kuyajibu. Hili ni jambo la kusikitisha sana!

Tukiacha suala la utunzi mbaya wa mitihani, NECTA pia inahusika katika kusababisha ulipuaji kwenye usahihishaji wa mitihani. Baraza la Mitihani hukusanya mamilioni ya shilingi kutoka kwa watahiniwa kwa ajili ya shughuli nzima zinazohusu utungaji, usambazaji, usahihishaji, uchakataji, na uandaaji wa madaraja ya watahiniwa.

Jambo la ajabu ni kwamba, pamoja na mapesa yote wanayokusanya, waliwapangia waalimu wasahihishe mitihani kwa muda wa majuma mawili huku wakiwalipa Tsh 200 kwa kila karatasi (script?) watakayoisahihisha. Katika miaka iliyotangulia, wasahihishaji walikuwa wakilipwa Tsh 400 kwa kila script na usahihishaji ulikuwa ukifanyika kwa muda wa majuma manne (mwezi 1).

Ukitafakari vizuri hapa, utagundua kwamba wasahihishaji walikuwa wanasahihisha kwa haraka na kwa kulipua kwa lengo la kila mmoja kujitahidi kusahihisha scripts nyingi ili apate pesa nyingi! Katika hali ya kawaida, hapa kulikuwa na ulipuaji wa hali ya juu.

USHAHIDI:
Nitatoa maswali machache kama ushahidi wa kile ninachokitetea. Yafuatayo ni baadhi ya maswali yaliyoulizwa katika masomo tofauti kwenye mitihani ya kidato cha nne mwaka 2012:

ENGLISH LANGUAGE:
Question 8.
The following sentences are jumbled. Rearrange them in a logical sequence to make a meaningful paragaraph by writing the corresponding letters in the answer booklet(s) provided.

For example: (i) – H

A. With the aid of television camera, visual images are changed into electrical signals.
B. A television set receives these signals and one can watch them on the screen.
C. However, in order to enable the television set to recieve these signals properly an antenna is needed.
D. These are then combined with radio waves and broadcast in the same way as ordinary sound signals.
E. Television is the system of transmitting moving pictures by radio or cable.

My arguments:
1. Instruction to candidates on how to answer the question is ambiguous and totally ununderstandable.
2. The answer is too technical for an ordinary level student to understand what individual sentences mean so as to be able to combine them to make a meaningful paragraph.

Combining the two difficulties above, it would be hard for the question to be answered correctly by a good number of students, bearing in mind that most of them are very novice at English language and grammar.

BIOLOGY:
Question 5.
Describe the following ecological terms:

(a) (i) Decomposers
(ii) Producers
(iii) Parasites

(b) With example, briefly explain how comparative embryology supports the idea of organic evolution.

CHEMISTRY:
Question 3
(a) With the help of chemical equation, what will be observed when ammonia reacts with:
(i) Hydrogen chloride
(ii) Copper (II) oxide

(b) It is not advisable to sleep inside a house which is not well ventilated with a burning wooden charcoal. Give a reason for that and write the chemical equation to represent your answer.

Question 13
Describe four common stages for the extraction of metals. Does the extraction of gold follow all four stages? Give reasons.

Maswali ni mengi lakini nimechagua haya machache kama mfano wa kile ninachokisema. Kwa kutumia hayo maswali machache, mtaona jinsi ambavyo Baraza la Mitihani limehusika katika kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha nne, 2012 huku likitetewa na baadhi ya wananchi na wanasiasa kwa manufaa wanayoyajua wenyewe. Tafakari, chukua hatua!
 
vilaza tu hawa watoto wa siku hz mchelemchele tu
 
huwa napatwa na hasira ninaposoma ujinga kama huu sasa wewe ulitaka wawaulize maswali gani??
 
mkuu kwa sasa kuna paradigm shift kutoka content based kwenda competence based education au wenyewe wanaita ni muhamo wa luwaza. ni kweli maswali ya list, mention, name, define, distinguish yanapima uwezo wa mwanafunzi kukariri ufahamu lakini kwa mujibu wa muhamo wa luwaza maswali yanayotakiwa kuulizwa ni ya kujieleza na kufafanua mambo kwa kutumia uelewa wa mwanafunzi mwenyewe sio kama alivyokaririshwa na mwalimu darasani.
bila shaka mkuu wewe taarifa hizi hukuwa nazo na ndio maana umelaumu kwa nini wanafunzi wasiulezwe maswali ya kukariri ya akina mkandawile na nyangwine.
ama kwa hakika hii ni changamoto kubwa kwani vijana wetu walio wengi ambao wanaathiriwa na lugha zao za asili ni vigumu kujieleza(tufanyeje?)
hata mimi naona kama uamuzi wa kuanza kutumia mabadiliko haya ya dira ya mitaala kuhama kutoka ukariri wa ufahamu hadi mwanafunzi kujieleza kwa uelewa weledi binafsi wa mwanafunzi umeanza kutekelezwa kwa haraka mno.
binafsi pia ningependa yale mambo ya enzi zetu za kusolve mapast paper kitu ambacho kwa muhamo wa luwaza si cha kutegemea sana.
nikutahadharishe mkuu kwamba kwa kuwalaumu moja kwa moja baraza necta ambao ni watekelezaji utakuwa hujawatendea haki sana kama ambavyo nimefafanua hapo juu.
 
Mleta mada, maswali yangu kwako ni haya
1. Je hayo maswali yapo nje ya walichofundishwa wanafunzi darasani?
2. Unapolinganisha mitihani ya 90's na sasa je umetafakari mabadiliko mbalimbali yaliyotokea kwenye mfumo wa elimu hadi sasa?
3. Je unajua kuwa wanaotunga maswali ni walimu waliopo mashuleni na NECTA hufanya kuyachagua tu?
4. Je wafahamu kuwa mabadiliko yoyote yafanywayo na NECTA ni lazima wizara husika wataarifiwe na wao ndio wanazitaarifu shule?

Ahsante kwa uungwana wako katika kunijibu haya maswali.
 
Wewe unashangaza kwelikweli hayo maswali yapo within the scope ya waliyofundishwa. Ni umbumbumbu mtu kushindwa kuelezea alichoelewa, no wander ulikuwa mdesaji kwa kuwa ni rahisi kupiga chabo herufi kuliko maelezo.
competence based education lazima itoe fursa ya wanafunzi kuonesha uwezo wao na upana wa somo lilivyoeleweka.
matatizo yetu kama nchi yanahitaji kutatuliwa kwa njia ya kfikiri kwa kina.
 
Haya mleta mada, tutaacha kutunga maswali MAGUMU ili wanafunzi WAFAULU, na ili KUBORESHA kiwango cha elimu kilichoshuka tutajipanga na MULUGO na hivi karibuni tutaleta maswali kama

1. The highest mountain in Africa is KILIMA.....
a. njeru
b. njoro
c.njaro
d. njiro

2.The first President of the United Republic o Tanzania was Julius Kambarage Nye......
a. rara
b. rire
c.rere
d.roro

With this kind of examinations we are sure that all our students will pass with flying colours hence improving the level of PERFORMANCE of our schools. ridiculous
 
Naunga mkono hoja kwa sababu zifuatazo:
1.kujituma kwa walimu kumepungua tofauti na zamani.
2.kutoa maswali nje ya silabasi,eg.hakuna kitabu cha wizara ya elimu kilichoelezea extraction of gold na pia maswali mengi yanatoka ktk vitabu vya kenya hususani masomo ya biology,chemistry na physics.
3.elimu kuingiliwa na siasa.
4.kutokuwa na ukaguzi au ufuatiliaji wa vipindi vya walimu madarasani.
 
vilaza tu hawa watoto wa siku hz mchelemchele tu
punguani tu ndo mwenye mawazo kama hayo,hauwez ukajiona wewe ni bora kuliko mwingine.....!sasa hao mchelemchele wana tofauti gani na wewe nganongano
 
Mtaala wa miaka ya nyuma na mwaka huu ni tofauti! Katafute vitabu pia uone (navyo ni vya kumpa mtoto uwezo wa kujieleza hivo hivo) tukubaliane na ukweli kuwa kufutwa kwa mtihani wa form two, na uvivu wa watoto wenyewe ni tatizo sana! kweli mtu hajui hata' grandchilren', aunt, sister na mengine madogo madogo! Wafaulu waende wapi?
 
Wandugu, baada ya kivumbi cha Arusha kutulia, ngoja sasa turejee kwenye mambo ya msingi huku tukisubiri tukio jingine litokee, maana hii nchi kwa matukio haina mfano!
Ni sababu hiyo hiyo ya matukio yasiyoisha iliyotupelekea kusahau kwa haraka matokeo mabaya kabisa ya kidato cha nne, 2012, matokeo ambayo hayajawahi kutokea tangu nchi hii ipate uhuru kutoka kwa wakoloni wa kiingereza mnamo 1961.

Pamoja na sababu nyingi zilizochangia kushuka kwa ufaulu, baraza la mitihani (NECTA) hawawezi kukwepa lawama, hata kama tayari wameishatetewa na watu mbali mbali. Ninasema hili nikiwa na ushahidi ili na mimi nisije nikashurutishwe na Bw Jagonja kuwapelekea polisi ushahidi wangu.

Nimepitia mitihani yote ya kidato cha nne, 2012 nikailinganisha na mitihani iliyotangulia nikagundua kwamba mitihani ya mwaka 2012 ilitungwa kwa mfumo tofauti na mitihani iliyotangulia. Mitihani hii ya mwaka 2012 imetungwa kwa mfumo wa kujieleza zaidi. Maswali karibu yote (hata yale yasiyokuwa ya essay) yanamtaka mwanafunzi kueleza kwa marefu majibu yake. Nyingi ya keywords zilizotumika kuuliza maswali ni kama vile: explain, describe, give a detailed account of, comment on, write an essay on, elaborate, substantiate, evaluate, etc. Keywords za aina hii zinapotumika kuuliza maswali maana yake ni kwamba mtahiniwa anatakiwa kueleza swali lake kwa urefu na kwa upana kweli kweli.

Katika mitihani ya mwaka 2012, kulikuwa na maswali machache sana yanayowataka wanafunzi kuorodhesha (list), kutaja (mention), kueleza kwa ufupi (outline), kufupisha (summarize), kupambanua kwa ufupi (define) na maswali mengine kama hayo. Maswali karibu yote yalikuwa ni ya kujieleza kwa urefu na kwa ufasaha. NECTA walifanya hivi kwa maskusudi huku wakijua kwamba uwezo wa wanafunzi wetu wa shule za sekondari ni mdogo sana. Sasa hii maana yake ni nini kama sio kulenga kuwafelisha watoto kwa makusudi?

Sina shaka mtakuwa mnafahamu kwamba wanafunzi wengi wa shule za kata wanaingia sekondari wakiwa hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu! Kama hali ndiyo hiyo basi, inawezekanaje NECTA iwatungie wanafunzi hawa mitihani ya kujieleza kwa lugha ya kimombo wakati hata Kiswahili chenyewe hawajui kukisoma wala kukiandika? Je, walitegemea wanafunzi wafeli halafu ndipo wanasiasa waingilie kati kuchakachua matokeo?

Ndiyo maana watu wenye busara wakashauri kwamba ingekuwa bora mitihani ikarudiwa kuliko kuchakachua matokeo peke yake. Wanasiasa walitakiwa kuchakachua hadi mfumo na staili iliyotumika kuuliza maswali. Huwezi kuchakachua matokeo tu ukaacha kuchakachua maswali ya mitihani yaliyozaa hayo matokeo. Kama vile wanasiasa walivyojitetea kwamba wanachakachua matokeo ili kwamba "matokeo yalingane na juhudi za kila mwanafunzi", walipaswa warudi nyuma zaidi hadi kwenye mitihani yenyewe.

Kana kwamba hilo halitoshi, mitihani yenyewe iliyotungwa haieleweki na wala haikutungwa kwa kutumia lugha nyepesi. Lugha iliyotumika katika mitihani ni ngumu sana. Lengo la maswali ya mitihani sio kumkomoa mwanafunzi bali ni kumpima uelewa wake katika mambo aliyojifunza kwa miaka minne. Mitihani haipawsi kupima uwezo wa mwanafunzi kuelewa maswali bali ni kumpima uwezo na kiwango chake cha uelewa wa maarifa aliyojifunza. Ndio maana lugha ya mtihani inatakiwa iwe rahisi na irahisishwe kadri itakavyowezekana ili mtahiniwa aweze kuelewa maswali barabara na kuyajibu kwa ufasaha. Kwa bahati mbaya, watunzi wengi wa mitihani wana tabia ya kutunga maswali ya kimitego, kwa kutumia lugha ngumu na tata ili kuwafanya wanafunzi washindwe kuelewa maswali, hivyo washindwe kuyajibu. Hili ni jambo la kusikitisha sana!

Tukiacha suala la utunzi mbaya wa mitihani, NECTA pia inahusika katika kusababisha ulipuaji kwenye usahihishaji wa mitihani. Baraza la Mitihani hukusanya mamilioni ya shilingi kutoka kwa watahiniwa kwa ajili ya shughuli nzima zinazohusu utungaji, usambazaji, usahihishaji, uchakataji, na uandaaji wa madaraja ya watahiniwa.

Jambo la ajabu ni kwamba, pamoja na mapesa yote wanayokusanya, waliwapangia waalimu wasahihishe mitihani kwa muda wa majuma mawili huku wakiwalipa Tsh 200 kwa kila karatasi (script?) watakayoisahihisha. Katika miaka iliyotangulia, wasahihishaji walikuwa wakilipwa Tsh 400 kwa kila script na usahihishaji ulikuwa ukifanyika kwa muda wa majuma manne (mwezi 1).

Ukitafakari vizuri hapa, utagundua kwamba wasahihishaji walikuwa wanasahihisha kwa haraka na kwa kulipua kwa lengo la kila mmoja kujitahidi kusahihisha scripts nyingi ili apate pesa nyingi! Katika hali ya kawaida, hapa kulikuwa na ulipuaji wa hali ya juu.

USHAHIDI:
Nitatoa maswali machache kama ushahidi wa kile ninachokitetea. Yafuatayo ni baadhi ya maswali yaliyoulizwa katika masomo tofauti kwenye mitihani ya kidato cha nne mwaka 2012:

ENGLISH LANGUAGE:
Question 8.
The following sentences are jumbled. Rearrange them in a logical sequence to make a meaningful paragaraph by writing the corresponding letters in the answer booklet(s) provided.

For example: (i) – H

A. With the aid of television camera, visual images are changed into electrical signals.
B. A television set receives these signals and one can watch them on the screen.
C. However, in order to enable the television set to recieve these signals properly an antenna is needed.
D. These are then combined with radio waves and broadcast in the same way as ordinary sound signals.
E. Television is the system of transmitting moving pictures by radio or cable.

My arguments:
1. Instruction to candidates on how to answer the question is ambiguous and totally ununderstandable.
2. The answer is too technical for an ordinary level student to understand what individual sentences mean so as to be able to combine them to make a meaningful paragraph.

Combining the two difficulties above, it would be hard for the question to be answered correctly by a good number of students, bearing in mind that most of them are very novice at English language and grammar.

BIOLOGY:
Question 5.
Describe the following ecological terms:

(a) (i) Decomposers
(ii) Producers
(iii) Parasites

(b) With example, briefly explain how comparative embryology supports the idea of organic evolution.

CHEMISTRY:
Question 3
(a) With the help of chemical equation, what will be observed when ammonia reacts with:
(i) Hydrogen chloride
(ii) Copper (II) oxide

(b) It is not advisable to sleep inside a house which is not well ventilated with a burning wooden charcoal. Give a reason for that and write the chemical equation to represent your answer.

Question 13
Describe four common stages for the extraction of metals. Does the extraction of gold follow all four stages? Give reasons.

Maswali ni mengi lakini nimechagua haya machache kama mfano wa kile ninachokisema. Kwa kutumia hayo maswali machache, mtaona jinsi ambavyo Baraza la Mitihani limehusika katika kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha nne, 2012 huku likitetewa na baadhi ya wananchi na wanasiasa kwa manufaa wanayoyajua wenyewe. Tafakari, chukua hatua!

Nashukuru kwa uchambuzi ulioweza kuuweka humu ndani kuonesha kwamba unajali elimu yetu ya Tanzania badala ya kuwa kama sisi wengine tuliomo humu kupinga tu bila kutoa maoni.Siwezi kusema kwamba kila ulichoandika kipo sawa na pia siwez kusema kama umekosea ila naweza kuchangia sehemu chache kulingana na nilivyoiona mitihani.

Hapo kwenye blue cwezi kukubaliana napo kwa maana sio sababu ya msingi ya kufanya mitihani itungwe kwa kiswahili.Kutokujua kusoma na kuandika kwa wanafunzi wanaojiunga kidato cha kwanza sio sababu ya kuwalaumu necta kutunga mitihan ya kujieleza kwa kimombo wakati unajua wazi kwamba hata mitihan ya miaka ya nyuma ilitungwa kwa lugha hiyo.Kufanya ivyo ni kushusha elimu ya yetu.
Hao watu unaowaita wenye busara inawezekana siku hiyo walikuwa wana mawazo yanayowasumbua ndio maana wakatoa mapendekezo kama hayo.Pia upande mwingine unaweza ukasema mtu anabusara kwasababu tu wewe binafsi unamuheshimu,haiwezekani mtu akatoka shule oktoba then mei unakuja kumuambia arudie mtihani,hapo unadhan atafanyaje mtihan utakaompa au ndio utampa mwezi mmoja wa kujiandaa ukidhan atafaulu zaidi ya mara ya kwanza.

Binafsi naweza kukuunga mkono hapo kwenye malipo ya walimu maana nadhan ndipo matatizo yalipo.Ni wazi walimu wanafanya kazi yao ili waweze kujiingizia chochote cha kulisha familia zao na itakuwa ni kazi ngumu kwa mwalimu kupoteza mda na karatasi moja yenye malipo kidogo.Pia madai ya walimu yalikuwa hayajashughulukiwa kipindi walimu wanasahihisha mitihani ivyo inaweza ikawa moja ya sababu zilizochangia matokeo mabaya.

Kwa upande wa maswali uliyoyaweka hapo sijaona tatizo lolote kwa maana ni vitu ambavyo vinafundishwa darasani labda inawezekana kipindi wewe unasoma hayakuwepo ila ni maswali wanafunzi wameyapitia na hata mitihani ya miaka ya nyuma baadhi yalikuwepo.Tafuta vitabu vinavyotumika mashuleni uchunguze kama hautapata majibu ya maswali uliyoyaweka hapo.

Kwa upande wangu nadhani njia bora ilikuwa ni kurudia kusahihisha upya na sio kupeana marks za bure.

mkuu kwa sasa kuna paradigm shift kutoka content based kwenda competence based education au wenyewe wanaita ni muhamo wa luwaza. ni kweli maswali ya list, mention, name, define, distinguish yanapima uwezo wa mwanafunzi kukariri ufahamu lakini kwa mujibu wa muhamo wa luwaza maswali yanayotakiwa kuulizwa ni ya kujieleza na kufafanua mambo kwa kutumia uelewa wa mwanafunzi mwenyewe sio kama alivyokaririshwa na mwalimu darasani.
bila shaka mkuu wewe taarifa hizi hukuwa nazo na ndio maana umelaumu kwa nini wanafunzi wasiulezwe maswali ya kukariri ya akina mkandawile na nyangwine.
ama kwa hakika hii ni changamoto kubwa kwani vijana wetu walio wengi ambao wanaathiriwa na lugha zao za asili ni vigumu kujieleza(tufanyeje?)
hata mimi naona kama uamuzi wa kuanza kutumia mabadiliko haya ya dira ya mitaala kuhama kutoka ukariri wa ufahamu hadi mwanafunzi kujieleza kwa uelewa weledi binafsi wa mwanafunzi umeanza kutekelezwa kwa haraka mno.
binafsi pia ningependa yale mambo ya enzi zetu za kusolve mapast paper kitu ambacho kwa muhamo wa luwaza si cha kutegemea sana.
nikutahadharishe mkuu kwamba kwa kuwalaumu moja kwa moja baraza necta ambao ni watekelezaji utakuwa hujawatendea haki sana kama ambavyo nimefafanua hapo juu.

Ndugu yangu, pamoja na huo mhamo wa ruwaza, hivi unadhani kwamba wanafunzi wanaoingia sekondari huku hawajui kusoma na kuandika wana uwezo wa kujieleza kweli? Pili, kumbuka kwamba Waziri Kawambwa alisema matokeo yanachakachuliwa ili "yalingane na juhudi za wanafunzi" na mazingira wanayosomea. Unadhani kwamba mazingira ya sasa ya kutolea elimu yanafanana na yale ya shule za miaka ya 80s au 90s?
 
Ni vema ripoti iwekwe hadharani kwani haiwezekani serikali ione uozo mwote huo halafu ikae kimya tu huku mitihani ya Kidato cha Nne 2013 ikitarajiwa kuanza tarehe 4/11/2013. Pamoja na kuwa inawezekana kuna huo uozo NECTA lakini makosa kama hayo ya usahihishaji ni vema mifano halisi ikatolewa kwani nimeshafanya kazi ya marking najua jinsi uhakiki unavyofanyika. Uzuri ni kuwea karatasi za watahiniwa haziteketezwi mapema. Ingependeza udhaifu huo ungewekwa bayana ili kama kweli kulikuwa na madudu hayo basi yasijirudie tena mwaka huu.

Kwa nini hiyo ripoti iwe siri sana? Kwa nini Dr Ndalichako apewe likizo ya muda mrefu. Watanzania tunataka majibu.

Na jee Mkuu wa kaya ya elimu, kama kumekuwa na udhaifu mkubwa kwenye nyumba yake mpaka Kiranja wake ameunda tume ndiyo imeanika uozo, bado Kawambwa ana sifa ya kuwa Waziri wa Elimu?

TUNATAKA MAJIBU TUMECHOSHWA NA UBABAISHAJI
 
Back
Top Bottom