beneli
Member
- May 1, 2013
- 86
- 7
Japo kwa chini chini lakini wote twajua kuwa wanafunzi wa kidato cha nne wanaosubiri matokeo mioyo na roho zao zipo juu pindi wasikiapo neno 'matokeo'hata kama ni ya mpira, roho huruka.Binafsi nilishapitia hatua hii miaka zaidi ya mitano iliyopita, swala linalonitatiza ni kweli matokeo ya NECTA huwa kweli ndo kilichopandwa ?
Tunawajua watu wengi mitaani kwa mashuleni ,waliokuwa na bidii za dhati katika elimu walioangukia pua , je hawakuwa na juhudi ? Swala la ufaulu kwa ujumla huwa linawaacha hata walimu na vitendawili visivyotegulika vya hata flan ! Na flani !? Nini kiliwakuta ? Tunashukuru Mungu tuliopita huko ,lakini wengi hatukupenda 'mavuno' haba tuliyopata, ila tukasonga mbele.
Ninachojaribu kusema kwa wadogo zangu ni kutoweka matarajio makubwa sana usije ukaghafilika na matokeo..na ushukuru Mungu kwa kile utakachokipata.
Niwatakie Matokeo mema