NECTA Tulipeni pesa zetu!

Sango Ochwera

Member
Joined
Mar 20, 2013
Posts
98
Reaction score
26
Ikiwa ni siku mbili tangu kidato cha nne kuanza mitihani yao ya Taifa, wilayani Rorya malipo ya wasimamizi wa mitihani hiyo bado ni kitendawili.Akifunga semina elekezi ya wasimamizi wa mitihani hiyo Novemba 2, 2013 katika ukumbi wa CCM Utegi,Afisa Elimu Sekondari wilaya ya Rorya aliwaahidi walimu kuwalipa fedha zao kati ya Jumatatu na Jumanne ambapo hadi sasa hakuna taarifa yoyote juu ya malipo hayo ya wasimamizi.

Natambua wazi umahiri wa serikali katika kulimbikiza kwa makusudi madeni ya walimu,lakini kwa hili tunaiomba serkali kupitia NECTA itulipe pesa zetu! Hii si kazi ya kujitolea.Tambueni kuwa kazi hii ni ya risk kubwa,hivyo kuendelea kukalia haki zetu huku mkitutaka kuendelea na kazi ni manyanyaso yasiyoweza kuvumiliwa hata kidogo!
 
Maskini Walimu,hata kwenye suala nyeti kama usimamizi wa mitihani pia wanakopwa na serikali? Serikali ya nchi hii sasa inaelekea siko! Big Results Now na manyanyaso kwa walimu!
 
Kama hulipwi unaweza kuacha kaz, c iko nje ya ajira
 
Waliosimamia mitihani ya form two wilaya ya mkuranga nao hadi leo bado hawajalipwa,so huko tu.
 
Ndalichako kaondoka yamebaki mazombie... Hakuna kitakacho endelea hapo eti BIG RESULTS NOW wakati secta nyeti katika elimu wameendelea kuwepo mapepo yasiyo mjua hata Mungu
 
Ni big results now ama better resign now (brn)?
 

Inaonekana hufahamu hata unayepaswa kumdai. NECTA hawahusiki hapo mlipaji wenu ni TAMISEMI.
Aione MotoYaMbongo.
 
Inaonekana hufahamu hata unayepaswa kumdai. NECTA hawahusiki hapo mlipaji wenu ni TAMISEMI.
Aione MotoYaMbongo.
wewe ndo ujui bajeti ya uendeshaji mitihan inatoka nectaTAMISEMI inahusikaje.necta ni taasisi chini ya moevt wanafungu lao
 
wewe ndo ujui bajeti ya uendeshaji mitihan inatoka nectaTAMISEMI inahusikaje.necta ni taasisi chini ya moevt wanafungu lao

Watu wengine bana!
Endelea kujidanganya ila usidanganye wenzio na kama hujui kitu uliza utafahamishwa tu.
Hilo swala lilisharudi TAMISEMI siku nyingi. Tangu wasimamizi walipoanza kulipwa half Per Diem.
TAMISEMI isihusike kwani shule za sekondari na walimu kwa ujumla wapo wizara gani?
 
Wilaya ya kasulu na buhigwe mpaka leo tar 13.11.2013 hawajalipwa fedha ya semina ya mtihani wala ya usimamizi na mitihani shule zilizo nyingi zimememaliza, walimu wamebaki bila msaada hata nauli hawana za kuwarudisha vituo vyao vya kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…