Necta wako sahihi csee 2012

K2S7J3

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
449
Reaction score
332
Sijaona kosa la NECTA kuhusiana na failure ya CSEE 2012 kwa sababu zifuatazo;

1. Mtihani ulikuwa standard

2. Usahihishaji ulifanywa na walimu wenyewe

3. Necta waligrade matokeo kwa viwango vya kawaida

4. Baada ya kuridhishwa na mwenendo mzima huo wa uandaaji wa matokeo, waziri aliyatangaza kwa watanzania

Nashindwa kuelewa kwa nini lawama zinatupiwa NECTA wakati wizara ndo wanahusika na uandaaji wa wanafunz hivyo kufeli ni kwa sabab ya mandaalizi mabovu na sio kulalamikia grading

Hebu tujiulize;
1. Kwa nini wizara wanawarushia mpira NECTA wakat waziri ndo alitangaza matokeo?

2. Mwanafunzi kaenda form 1 kisiasa hajui kusoma na kuandika, halaf form 2 hakuna mtihani. Je, huyu naye tustandardize ili apate division IV?

3. Kwa staili hii tunaipeleka wapi nchi yetu?

Fikra pevu zinahitajika sana

nawasilisha mada wana JF
 
Hoja zote ulizotoa ni za kweli kabisa lakini zimemezwa na grade ambazo serikali imetangazia umma kuwa zilitumika wakati wadau hawakuandaliwa.Binafsi sio mwalimu lkn baada ya walimu kutoka kusahihisha walirudi na taarifa kuwa vijana wengi hawajafanya vizuri.Alama za kufaulu kwenye karatasi za kujibia zilikuwa za kutafuta sana.Kauli ya serikali yaweza kuwa kweli lakini sio sababu pekee ya anguko hilo la ufaulu
 
hapana mkuu uko sawa sawia haijawahi kutokea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…