NECTA yatangaza matokeo ya darasa la nne na kidato cha pili, 2017, 51,807 wakwama kuendelea kidato cha 3

NECTA yatangaza matokeo ya darasa la nne na kidato cha pili, 2017, 51,807 wakwama kuendelea kidato cha 3

Mkuu [HASHTAG]#Hajto[/HASHTAG] ingia kwenye hii link itakupeleka direct shulen kwako.

ukifanikiwa utujuze
Damdeok na mm nipatie link yakucheki moja kwa moja matokeo ya MZUMBE secondary school..
 
we ndo mshamba ukifungua shule control +f andika jina then enter
Hiyo command naijua sana na ndio ya kwanza kuitumia lakini kanapokuja kale ka box cha kuandika ukianza kuandika herufi yoyote , inatokea rangi nyekundu ikiwa na maana hakuna herufi ya namna hiyo . Labda kitu ambacho sasa naweza kukubali kama wewe imekubali komand hiyo basi tatizo ni brawzer ya maxthon ninayoitumia . Yamkini ningeyafungua kwa mozila, crome au internet explorer ingekubali hiyo command
 
mi natumia mozilla imekubali aiseee may be browser
 
Attachments

  • kweli.jpg
    kweli.jpg
    154.9 KB · Views: 188
Haka kawebsite ka necta mbona ni chenga? tz hamna hata kimoja tunachoweza?
 
Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mitihani ya upimaji wa darasa nne na kidato cha pili iliyofanyika Novemba 22 na 23 mwaka jana, huku idadi kubwa ya wanafunzi wakifanya vyema katika mitihani hiyo.

Akitangaza matokeo hayo leo Jumatatu Januari 8, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema jumla ya wanafunzi 1,086,156 waliofanya mtihani wa darasa la nne wamefaulu kati ya 1,158,444 waliofanya upimaji huo.

Amesema wanafunzi hao wamefaulu kwa kupata alama zenye madaraja ya A,B,C na D wakati wanafunzi 72,288 sawa na asilimilia 6.24 wamepata alama za daraja E, ambao ni ufaulu usioridhisha.

Kuhusu matokea ya upimaji wa kidato cha pili, Dk Msonde amesema jumla ya wanafunzi 433,453 sawa na asilimia 82.32 kati ya 486,742 waliosajiliwa kufanya mtihani huo wamepata ujuzi wa maarifa ya kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu.

Dk Msonde alisema wanafunzi wa kidato cha pili 51,807 sawa na asilimia 10.68 wameshindwa kupata alama za kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu.

Chanzo: Mwananchi

Kwa matokeo ya kidato cha pili, bofya link hapo chini
MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2017

Kwa matokeo ya darasa la nne, bofya link hapo chini
MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2017
Naweza kupata matokeo kujua ni shule zipi zimekuwa za kwanza mpaka kumi kitaifa.Please mwenye hiyo list naimba aiweke hapa tuone.
 
Back
Top Bottom