Mimi sijivunii kuona wamafunzi waliofeli wakifaulishwa kwa sababu za kisiasa. Hebu fuatilia mnyororo huu wa namna tunavyoandaa Taifa lisilowajibika kwa kuchukua mfano wa hawa vijana
2002: Walianza darasa la kwanza. Ada ya shule ya msingi ilifutwa: Bahati iliyoje
2005: Wako darasa la nne. Mitihani ya kwenda darasa la tano ilifutwa. Wakapita mpururo
2010: Wakiwa form two. Mitihani ya form two haikuwa kigezo cha kuwapeleka kidato cha tatu
2012: Matokeo yalikarabatiwa ili waonekane wamefaulu
Sasa kama watangulizi wao ambao hawakuwa na "bahati" kama hizi wameweza kujenga maghorofa yakaporomoka, wakafanya makandarasi wa kujenga barabara waazimwe kutoka China/Ujerumani/Japan, wataalam wa fedha waazimwe kutoka Ulaya/Marekani, wakapasua vichwa badala ya miguu na kuwafanya akina Mwandosya, Zito Kabwe na Mwakyembe wakakosa imani nao na kwenda kutibiwa India; hebu tujiulize swali hili kubwa
Watakapofika chuo kikuu na kuendelea na "bahati" hii, hivi hatuoni kwamba itatwezekana sasa tukaandaa madaktari watakaoweka mioyo ya kuku kwa binadamu na kujenga magorofa kwa mabua?
Hebu jamani tuangalie mustakhbar wa Taifa badala ya kufurahi "miteremko" hii inayoletwa na wanasiasa
Inawezekana nikaudhi watu lakini uzalendo umezingatiwa
Chas Mike