NECTA yatikiswa; yacharuka

Kwani mwanzo walisahihisha kwa gharama za nani mkuu?

Kawaida unapo appeal ili usahihishiwe upya, unalipia gharama za appeal yako, ndiyo maana katika hili, nimetoa maoni kuwa NECTA warudie kusahihisha upya kwa wote, bila kudai gharama za appeal (Kwa gharama zao), ili wajisafishe na kashfa hii. Vinginevyo, kashfa hii ni nzito kwao. (Sijui kama umenielewa)
 

Sitegemei kama NECTA wale wale wakisahihisha tena kutakuwa na kitu tofauti mkuu
 

Mkuu nadhani unaweza kuchukua muda kidogo kuangalia ukweli wa madai
Mimi nimekwenda kwenye link ya shule hiyo na nimeangalia namba hiyo 0173 nimeona Bwana Bujugo alikosea walau kwa namba hiyo aliyoitaja. https://www.jamiiforums.com/matokeo2012/data/s1197.htm
 
Mambo ya kukurupuka wakati mwingine sio mazuri pengine aliambiwa na mke wake :A S shade:
Mchwechwele mwalimu alishakula pesa ya mzazi na kumhakikishia lazina anapasua; sasa hivi anaweweseka kwa hofu ya kudaiwa pesa na kukimbiwa na wanafunzi
 
Last edited by a moderator:

Si wamebadilisha tu kwenye system!!!! haichukui hata dakika mbili kuyarekebisha mara baada ya tuhuma kutolewa.
 
kama kayeyusha huyo hedimasita, anyang'anywe shule.....anatuharibia watoto!
 
Safi sana. Nilisema kuwa huyu jamaa kachemka hata matokeo ya wanafunzi wake anashindwa kuyasoma.
anapitia matokeo ya wanafunzi wake kichwani kuna viroba vitatu unategemea nini?
 

Mkuu nakupata, na hii issue ni sensitive, We can not judge him from only one factor, I think Director is not crazy, kwa hali hiyo, anazo sababu za kuthibitishia umma kuwa hajakurupuka, na anaweza ku-defend hoja zake. Huyu ni mtu wa msaada hasa pale atakapo toa ushirikiano kwa jamii. alitakiwa pamoja na hilo kosa ambalo umeliona, (na ki ukweli liko wazi, amekosea) aendelee kutoa ushirikiano, hasa kwa wale watoto ambao ana uhakika hawakufanya mtihani, na bado matokeo yao yakatoka na wakawa wamefaulu.
Kama kasema uongo, Huu ni uchochezi wa maksudi kwa nia ya kuchafua vyombo husika, achukuliwe hatua kali, na kama kasema kweli, basi, jamii haitakuwa na imani tena na NECTA, ivunjwe, na wahusika wachukuliwe hatua stahiki.
 
Na mimi sijazuia wafanye uchunguzi.

Nilichofanya ni fact checking.
 
Hapa napo vipi?

Alisema hivi: Alitaja mfano wa mwanafunzi, Humphrey Sanga, mwenye namba 01197/148, ambaye hakufanya mitihani hiyo lakini matokeo yanaonesha amefaulu kwa kupata alama nzuri.

"Huyu mwanafunzi tulimsimamisha na hakufanya mitihani, lakini matokeo yake yanaonekana amepata hivi; Civics D, Historia D, Jiografia C, Kiswahili D, English C, Physics D, Chemistry C, Biology C, Basic Mathematics D, ambapo amepata daraja la tatu pointi 24," alisema Bujugo.


Matokeo ya mtandaoni haya:

[TD="width: 6%"]
S1197/0148​
[/TD]
[TD="width: 4%"]
M​
[/TD]
[TD="width: 6%"]
24​
[/TD]
[TD="width: 4%"]
III​
[/TD]
[TD="width: 58%"]
CIV-D HIST-D GEO-C KISW-D ENGL-C PHY-D CHEM-C BIO-C B/MATH-D​
[/TD]
 
WAKATI mjadala wa matokeo mabaya ya kidato cha nne ukiendelea kulitikisa taifa, kashfa mpya ya matokeo hayo imeibuliwa.

Kashfa hiyo mpya imeibuliwa na Mkurugenzi wa Shule ya Green Acres, Julian Bujugo, kwamba matokeo ya baadhi ya shule nchini ikiwamo yake yamechakachuliwa.

Akizungumza na gazeti hili jana, Bujugo alisema kuwa baadhi ya wanafunzi kwenye shule yake hawakufanya mitihani ya kidato cha nne, lakini matokeo yanaonesha wamefaulu kwa kupata alama za juu.

Alitaja mfano wa mwanafunzi, Humphrey Sanga, mwenye namba 01197/148, ambaye hakufanya mitihani hiyo lakini matokeo yanaonesha amefaulu kwa kupata alama nzuri.

“Huyu mwanafunzi tulimsimamisha na hakufanya mitihani, lakini matokeo yake yanaonekana amepata hivi; Civics D, Historia D, Jiografia C, Kiswahili D, English C, Physics D, Chemistry C, Biology C, Basic Mathematics D, ambapo amepata daraja la tatu pointi 24,” alisema Bujugo.

Alimtaja mwanafunzi mwingine, Martin Rushaigwa, namba 01197/0173, ambaye alifanya masomo ya ‘Arts’.

Alisema matokeo ya mwanafunzi huyo yanaonesha kuwa ameongezewa alama za masomo ya biashara ya Bookeeping na Commerce, ambayo hakuyafanya kabisa.

Alimtaja mwanafunzi mwingine aliyefanya mtihani huo lakini matokeo yake yanaonesha amewekewa ‘absent’ na mwanafunzi mwingine, Mbazi Volta, hakufanya mitihani lakini amepewa alama za ufaulu.

“Matokeo hayo yananipa wasiwasi kwamba yanaweza kuwa yamechakachuliwa,” alisema Bujugo.

Mkurugenzi huyo anaiomba Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kurudia kusahihisha mitihani hiyo ili kuondoa ukungu ulioligubika taifa kwa sasa kuhusu matokeo ya kidato cha nne.

“Naomba usahihishaji urudiwe, maana huu ni ubabaishaji mkubwa…matokeo hayo yamewaathiri watoto kisaikolojia na sijui watakwenda wapi?,” alihoji.

Alisisitiza kuwa usahihishaji urudiwe kwani katika shule hiyo wanafunzi wenye uwezo mkubwa tangu walipoanza kidato cha kwanza ndio waliofanya vibaya wakati waliokuwa wakifanya vibaya, wameibuka na alama za juu.

Mkurugenzi huyo alisema wazazi wa watoto hao wanatarajiwa kukutana mwishoni mwa wiki hii kujadiliana kuhusu matokeo hayo na hatua za kuchukua.

Akitolea ufafanuzi suala hilo, Msemaji wa Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), John Nchimbi, alisema si kweli kuwa matokeo hayo yamechakachuliwa bali ni matokeo halisi ya shule hiyo.

Alisema iwapo mkurugenzi wa shule hiyo ana shaka na matokeo hayo, alitakiwa kufika katika ofisi za baraza hilo ili apatiwe taarifa sahihi kabla ya kutoa taarifa katika vyombo vya habari.

“Mi nimeangalia hayo majina, naona yapo sawa na hata huyo mwanafunzi ambaye anasemekana hakufanya mitihani na akapewa alama…napenda kusema kuwa alama alizopewa si zake na hata katika orodha yetu anaonekana kuwa hakufanya mitihani,” alisema.

Katika hatua nyingine, Waziri wa wizara hiyo, Dk. Shukuru Kawambwa na wenzake, wamekuwa bubu kueleza endapo wako tayari kujiuzulu au la.

Tanzania Daima ilifika wizarani hapo jana kutaka kuonana na Waziri Kawambwa ili atoe msimamo wake, mwandishi alijibiwa kuwa waziri huyo alikuwa kikaoni na asingeweza kutoka.

Hata waziri alipopigiwa simu pamoja na kutumiwa ujumbe mfupi wa maneno, hakupokea wala kujibu ujumbe huo.

Kwa upande wake, katibu mkuu wa wizara hiyo naye hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo kwa madai kuwa alikuwa kikaoni.

Naye Naibu Waziri, Philipo Mulugo, alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi kueleza msimamo wake, simu yake iliita bila kupokewa na hata hakuwa tayari kujibu meseji ya ujumbe mfupi.

Source :Tanzania Daima
 

Namba S1197/0148 SIO YA Humphrey Sanga. Huyo kilaza na mwalimu wake watakuwa wamesahau namba ya mtihani.
 
Si wamebadilisha tu kwenye system!!!! haichukui hata dakika mbili kuyarekebisha mara baada ya tuhuma kutolewa.

We kichwa maji. Nakala nyingine ya matokeo ipo Jamiii Forum. Wamebadilishaje huko?. Invisible nae ni NECTA?
 
Je kama ulikuwa na Div. 0, utapata ngapi?????? Kwa kashfa hii, nashauri NECTA wasahihishe mitihani yote upya kwa gharama zao!!!!!!

NECTA hawana gharama zao ni pesa ya watu waliochangia (pesa ya mitihani) au Kodi zetu (NECTA sio wafanya biashara..) all in all uzembe upo na huwa unatokea, nilikuwa ninawashauri watu kwamba kuna njia ya kufahamu matokeo nayo ni ku-appeal na kulipia gharama, nadhani kama kweli unajiamini gharama hio ni ndogo kuliko kukaa mtaani au kukosa cheti.., wangefanya bure nani angecover cost ?, pia hii ingefungua a can of worms kila mwenye zero na four angekuwa ana-appeal
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…