NECTA yatikiswa; yacharuka

NECTA yatikiswa; yacharuka

Wakuu mbona mtu unaweza uka-appeal unatoa pesa mtihani wako unasahihishwa upya.., (Ila tahadhari...) wakisahihisha upya wanakuwa na hasira kweli kweli unaweza ukawa ulipata II ukajikuta wakirudia unapata IV
Ndugu yangu, mwanafunzi wa shule ya kata aliyeko kijijini atapata wapi fursa ya kukata rufaa hata kama anajua wazi kuwa matokeo aliyopewa siyo sahihi
 
Imethibitishwa kutoka NECTA kwamba mkuu wa shule wa Green acres aliitwa NECTA ili kuprove kile ambacho kimesema na mkurugenzi wake, kwa kupitia matokeo ya mwanafunzi mmoja baada ya mwingine, na imebainika kwamba mkurugenzi huyo alitoa taarifa za kutungwa. Kwa hiyo NECTA imewaagiza wanasheria wake waandae kesi, tayari kwa kumpeleka mahakamani mkurugenzi wa Green acres.

Mkuu taarifa za kweli hizi?
 
anapitia matokeo ya wanafunzi wake kichwani kuna viroba vitatu unategemea nini?

Ha ha aha mkuu siku hizi elimu ni biashara kwa hiyo lazima ailinde kwa gharama yoyote ile!
 
Mkuu taarifa za kweli hizi?
100% nilikuwa baraza leo mchana na nikapewa taarifa hizi na baadhi ya jamaa zangu hapo baraza. So naamini ni za kweli, vinginevyo hawa rafiki zangu wawe wameamua kunidanganya.
 
Siku moja wakati Professor mmoja anatufundisha (Masters) akasema eti Dr. Kawambwa tangu aingie Coet hajawahi kuandika paper hata moja.....
 
Hapo ndipo patamu. Ikiwa Mkurugenzi kasema uongo, ajutie uchochezi wake, na kama itathibitika kuwa kasema kweli, basi NECTA iwajibike!!!!!!! Tunaomba haya yasiyeyuke kama upepo unaopita, bali jamii tupate ukweli na uhakika wa jambo hili. Walioathiriwa na matokeo hayo, nao wapewe haki yao kwa kupitia (kusahihisha upya) mitihani hiyo. Naamini, mitihani yao bado iko intact.

Kama ikithibitika ni kweli mtaamini madai ya kuchakachuliwa mitihani ya wanafunzi wa Kiislamu mwaka jana?
na kwanini sasa mnataka uchunguzi ufanyike na sio kabla!
 
necta kumbe ndio wapumbavu kiasi hiki, naanza kuamin kuwa waislamu walikuwa sawa kabisa kwa madai yao.
 
Hebu chukua muda kidogo ufuate link hii na kuangalia namba s.1197/0173 uone kama kuna Bookkeeping au commerce.

https://www.jamiiforums.com/matokeo2012/data/s1197.htm

Tanzania tumeona mengi kiasi hatushangai tena ila -Penye ukweli uongo hujitenga. Mara nyingi kama anavyoweza kuwa huyu mwalimu amekurupuka pia viongozi wetu tumezoea kuwaona wakikurupuka KUKANUSHA hata pale ambapo mambo yako wazi hivi ni mara ngapi umesikia kiaongozi akiongea tena kwenye tv na kesho akakanusha bila aibu akijua wazi record ipo. kama wew kinachokufanya uone mwalimu kadanganya ni hii link uliyotoa mbona hutuambii kuhusu mwanfunzi mwingine aliyetajwa (Humphrey Sanga, mwenye namba 01197/148) na kwa mujibu wa link hii madai ya mwalimu yako sawa?

[TD="width: 6%"] S1197/0148
[/TD]
[TD="width: 4%"] M
[/TD]
[TD="width: 6%"] 24
[/TD]
[TD="width: 4%"] III
[/TD]
[TD="width: 58%"] CIV-D HIST-D GEO-C KISW-D ENGL-C PHY-D CHEM-C BIO-C B/MATH-D
[/TD]

Mbona hukumalizia utafiti wako? [yasije yakawa yale ya Jairo ambayo tuhuma zilikuwa za uongo kwani idadi ya mashirika hayakuwa sawa(20) wala kiasi cha pesa hakikuwa mil 50 kama tuhuma zilivyodai]
Naamini hapa yawezakana kabisa kuna kaujanja mahali -and time will tell. na huenda hataenda mtu mahakamani - hivi umesahau vitisho vya list of shame kuwa wangeenda mahakamani - mapaka leo kimya, hajaeenda mtu mahakamani ..
 
We kichwa maji. Nakala nyingine ya matokeo ipo Jamiii Forum. Wamebadilishaje huko?. Invisible nae ni NECTA?

To the best of my knowledge JF ipo link, unless moderators saved the original web page ukibofya link you are directed to necta site.
 
Wakuu mbona mtu unaweza uka-appeal unatoa pesa mtihani wako unasahihishwa upya.., (Ila tahadhari...) wakisahihisha upya wanakuwa na hasira kweli kweli unaweza ukawa ulipata II ukajikuta wakirudia unapata IV
Mkuu hoja yako kama inafurahisha lakini ndani yake kuna ujumbe mzito sana. Unajua unaposahihisha karatasi laki nne, asilimia ya kuwa makini makini inaweza kabisa kupungua kutokana tu na uchovu, lakini inapotokea mtu/watu wachache wame-appeal basi asilimia ya umakini inakuwa kubwa zaidi, hivyo inawezekana kabisa hata pale ambapo walikubeba awali wakaangalia upya na vise versa.
 
Ndugu yangu, mwanafunzi wa shule ya kata aliyeko kijijini atapata wapi fursa ya kukata rufaa hata kama anajua wazi kuwa matokeo aliyopewa siyo sahihi
Mkuu usihofu NECTA ya sasa imeweka kila kitu wazi sio kama zamani, unaweza kupata fomu ya ku-appeal kwenye tovuti ya NECTA (The National Examinations Council of Tanzania) pakua jaza kwa usahihi, lipia na kisha itume NECTA kwa huduma. Maelekezo yote ya malipo yapo kwenye fomu hiyo.
Hii ni NECTA ya uwazi na Ukweli ya kwanza kutokea Tanzania.
 
Si wamebadilisha tu kwenye system!!!! haichukui hata dakika mbili kuyarekebisha mara baada ya tuhuma kutolewa.

Ivi wakibadilisha kwenye system na sisi tuliopewa CD zenye matokeo hayo na wengine walio download wakasevu kwenye kompyuta zao na flash nk huwa yanabadilika sio? Aiseee...na Press Release yao yenye ufafanuzi umeiona?? Ngoja nitafute scanner niwawekee hapa tumalize ubishi.
 
Na ikugundulika ni kweli na wao waburuzwe mahakamani kwa kuchakachua!
 
Na ikugundulika ni kweli na wao waburuzwe mahakamani kwa kuchakachua!
Na leo mzazi wa mwanafunzi asiyefanya mitihani lakini akapata daraja la 3 amethibitisha kuwa mwanaye alifukuzwa shule na hakufanya mtihani wa Taifa
 
Kama ikithibitika ni kweli mtaamini madai ya kuchakachuliwa mitihani ya wanafunzi wa Kiislamu mwaka jana?
na kwanini sasa mnataka uchunguzi ufanyike na sio kabla!

(Re:-Hiyo red) Kwa kuwa uchunguzi hufanyika baada ya tatizo kutokea, na siyo kabla ya tatizo. Kwa kuwa Tatizo limetokea, basi uchunguzi ufanyike (Re:-Hiyo blue) Dhana ya kuwa wanafunzi wanaweza kuchakachuliwa kwa misingi ya dini, hainiingii akilini, na wala haiwezekani kwa sasa. Labda mpaka hapo misingi ya ubaguzi wa kidini itakapokomaa. Kwa sasa bado sana, wala kwa watanzania wengi bado hatujashawishika kiasi hicho, na bado undugu mchanganyiko wa kidini tunao. "TUSIENDEKEZE UBAGUZI WA KIDINI, KWA KUWA MWISHO WA SIKU, SI MIMI WALA WEWE, ATAKAYENUFAIKA NA UDINI. SOTE TUTAJUTIA"
 
Back
Top Bottom