Le professel
JF-Expert Member
- May 14, 2019
- 636
- 960
Kwanini mkuu?Ila wasabato ni habari nyingine
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwanini mkuu?Ila wasabato ni habari nyingine
Hiyo chai haichemshwi!?Wasabato wana maisha magumu sana.
Nakumbuka nilikuwa nawatembelea ndugu zangu fulani wakati niko shule
Chakula kinapikwa ijumaa mchana kinaliwa hadi jumamosi jioni
Jumamosi hawapiki kitu mnakuoa kiporo na chai ya jana[emoji2]
Maisha yao ni magumu kwakweli
Uislam siyo dini ya kivivuMwamedi hakusema chochote kuhusu kupumzika ijumaa
Si ndo chanzo cha wapare kupika kande wanaweka ijumaa mpaka jumapiliWasabato wana maisha magumu sana.
Nakumbuka nilikuwa nawatembelea ndugu zangu fulani wakati niko shule
Chakula kinapikwa ijumaa mchana kinaliwa hadi jumamosi jioni
Jumamosi hawapiki kitu mnakuoa kiporo na chai ya jana[emoji2]
Maisha yao ni magumu kwakweli
Kuna Mtumishi Fulani hapa, Muislam yet akishafika kazini siku ya Ijumaa. Akishamaliza ripoti ya Asubuhi tu, na ndio kazi imeisha Hapo.Mimi si Muislam lakini niliwahi kusikia kuwa dini yao inasema baada ya Swala Ijumaa watu wanaweza kurudi kwenye majukumu yao. All in all Waislamu huwa hawana complications hasa kwa mambo ambayo hayaoneshi kuutweza Uislamu
Haki ya Miaka 8?Hamna kitu cha kupikwa, ushahidi upo wazi kaonewa wakati ni haki yake
Hii itasababisha wasabato wasiajiriwe ktk taasisi ya NMB milele,na taasisi nyingine pia zitawaogopa
Kwahiyo na waislamu wasiwe wanaenda kazini siku ya ijumaa?Kesi ya Neema Akeyo vs- National Microfinance Bank- NMB
HOJA:-
- HAKI YA KUABUDU SIKU YA SABATO
- Kuachishwa kazi kutokana na utoro (siku ya Jumamosi kwa muumini mwadventista) na utovu wa nidhamu
- Ubaguzi wa kutokana na dini/imani ya mtu
Tarehe 01/11/2010 Neema Akeyo aliajiriwa katika Benki ya NMB Arusha kwa nafasi ya Bank Teller hadi alipoachishwa kazi tarehe 05/06/2014 kwa makosa mawili
1. Utoro/absenteeism.
2. Utovu wa nidhamu/insubordination.
Kinyume na NMB Human Resource Manual Policy 2013, Staff Rules, na NMB Code of Good Practice.
Neema hakuridhishwa na uamuzi wa kuachishwa kazi hivyo aliwasilisha madai yake katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi- (Commission for Mediation and Arbitration-CMA) Arusha akipinga uhalali wa kusitishiwa ajira yake na kudai kwamba USITISHWAJI WA AJIRA ULIKUWA BATILI KWANI HAUKUTOKANA NA SABABU ZA MSINGI, NA HAUKUZINGATIA UTARATIBU ULIOWEKWA NA SHERIA. Katika hatua zote Neema alikuwa akiwakilishwa na Wakili Msomi Asubuhi Yoyo.
Uamuzi wa TUME- CMA
Hatimaye tarehe 05/08/2015 kupitia Mhe. Lomayan Stephano- Muamuzi Tume iliamua kwamba usitishwaji kazi ulikuwa batili kwani NMB hakuwa na sababu za msingi wala hakuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria kabla ya kumwachisha kazi Neema Akeyo.
Tume iliamuru NMB kumlipa NEEMA fidia ya mishahara ya miezi 36 kutokana na usitishaji kazi kutokana na ubaguzi wa kidini kwani Neema alinyimwa haki ya kuabudu siku ya Jumamosi kinyume na Katiba ya JMT na mikataba mbalimbali ya kimataifa ambayo Tanzania imeridhia.
Hukumu ya Mahakama Kuu ya Kazi - (High Court Labour Division)-HCLD @ Arusha
Baada ya Uamuzi/Tuzo ya Tume NMB hakuridhika hivyo aliwasilisha maombi ya marejeo katika Mahakama kuu kitengo cha Kazi, na hatimaye tarehe 02/06/2017 kupitia Mhe. Jaji Aisha Nyerere (kama alivyokuwa) Mahakama ilitupilia mbali /dismiss hoja zote za marejeo zilizowasilishwa na NMB, na Mahakama ilithibitisha/confirm Tuzo/Uamuzi wa CMA kwamba usitishaji kazi dhidi ya Neema Akeyo haukuwa halali.
Hukumu ya Mahakama ya Rufaa/ Court of Appeal of Tanzania- CAT iliyoketi Arusha
Baada ya kutoridhishwa tena na Hukumu ya Mahakama Kuu, NMB waliwasilisha Rufaa yao katika Mahakama ya Juu kabisa nchini kuiomba itengue Hukumu ile, na baada ya kusikilizwa kikamilifu tarehe 21/02/2022 Mahakama ilitoa Hukumu yake kupitia waheshimiwa Majaji watatu Mhe. MUGASHA, Mhe. SEHEL, na Mhe. KAIRO ambapo hoja zote za NMB zilitupiliwa mbali na Mahakama ilithibitisha Hukumu ya Mahakama kuu ya Kazi, na Uamuzi wa Tume.
Hukumu hii ni Muhimu kwani imegusa eneo ambalo limekuwa likileta changamoto kwa waumini mara nyingi hususan waumini Waadventista Wasabato.
Hizi ni baadhi ya Hoja zilizotawala katika Shauri hili. Mungu ni mwema na amejidhihirisha kupitia kesi hii. 🙏🏼🙏🏼🙏🏼
- Haki ya kuabudu
- Uhuru wa kuabudu
- Ubaguzi kutokana na dini/imani ya mtu
Nawasilisha kwenu Nakala za Hukumu za Mahakama kuu na Mahakama ya Rufaa.
Kwa muktadha wa makabrasha mengi na zikiwepo kalenda mbalimbali zinaonyesha siku ya kwanza ya juma ni jumapili, ambayo anapaswa kufanya kazi mpaka ijumaa siku ya sita.Kwahiyo wenzie wakifanya kazi siku 6 yeye anafanya kazi siku 5.
Sisi tunatumia calendar ambayo mwanzo wa wiki ni juma3. Shule mwisho ijumaa na baadhi jumamosi na jumapili mapumziko.Kwa muktadha wa makabrasha mengi na zikiwepo kalenda mbalimbali zinaonyesha siku ya kwanza ya juma ni jumapili, ambayo anapaswa kufanya kazi mpaka ijumaa siku ya sita.