Alichoongea Neema ni sahihi sema ulimi ulishindwa kutamka vizuri. Alikuwa anamaanisha kumbe ndio maana wanaokuwa Wabunge unapofika wakati wa uchaguzi wanatamani kuwatoa roho washindani wao kwa Kuwa Bungeni ni kuzuri. Ikumbukwe Neema aligombea 2015 alifanyiwa figisu hakupita. Mwaka 2020 aligombea tena watesi wake wakaungana kumshughulikia ili asipite. Na alishughulikiwa kwelikweli ikiwepo kutengenezewa kesi kibao. Kama mtakumbuka mpaka siku moja kabla ya uchaguzi alikuwa akizungushwa polisi kuwa ametoa rushwa lakini wakawa hawamuonyeshi ushahidi. Asubuhi aliporuhusiwa kwenda kuomba kura kwa maagizo ya viongozi wakuu mtakumbuka alipiga magoti aka za kulia na kutoa machozi kwa alichokuwa anafanyiwa na watesi wake. Pamoja na figisu alipata kura nyingi. Baada ya kupata kura nyingi bado watesi wake waliendelea kumuundama na kufanya lobbying ya vikao vya huko chini Kuwa wamuandike vibaya. Lakini JPM na timu yake walipoona zilikuwa ni figisu wakaamua kumpendekeza ateuliwe.
Neema ameteswa na watesi, anapomshukuru Mungu kufika hapo anakosa maneno ya kusema. Hivyo alimaanisha watesi wanatamani kutoa roho na si yeye.