warumi
R I P
- May 6, 2013
- 16,218
- 18,440
Staa wa Bongo Fleva ambaye kwa sasa anafanya kweli kimataifa, Nasibu Abdul ' Diamond Platnumz ' ameandika historia kwenye Tuzo za Black Entertainment Television ( BET) 2014 huku akiwatia kiwewe mastaa wakubwa kama Cornell Iral Haynes ' Nelly ' , Christopher Maurice ' Chris Brown' na wengine kibao.
Tukio hilo lilijiri usiku wa kuamkia Jumatatu wiki hii kwenye Ukumbi wa Nokia Theatre jijini Los Angeles , Marekani ambapo Diamond alikuwa ameteuliwa kuwania Kipengele cha Mwanamuziki Bora kutoka Afrika akiwa sambamba na mwanamuziki Davido ( Nigeria ) , Mafikizolo ( Afrika Kusini) , Tiwa Savage ( Nigeria ) , Toofan ( Togo ) na Sarkodie ( Ghana) .
TUZO YAENDA KWA DAVIDO
Tuzo hiyo haikuwa bahati kwa Diamond kwani ilikwenda kwa Davido . Licha ya kukosa tuzo hiyo , yapo mengi ambayo Diamond ameweka historia au rekodi katika ' event' huku kuunganishwa na mastaa hao ikiwa topiki muhimu.
MCHUMBA WA CHRISS BROWN AMSHOBOKEA
Katika hali ya kushangaza, mwanamitindo maarufu Marekani ambaye ni mchumba wa Chris Brown, Karrueche Tran alionekana kumshobokea Diamond mara alipokutana naye uso kwa uso.
Karrueche alijikuta hajiwezi alipokuwa akimhoji Diamond ambapo moja kwa moja alimvutia kipaza sauti na kuanza kumpiga maswali huku akionesha kuvutiwa naye kwa muonekano aliokuwa nao .
Akihojiwa na demu wa Chris Brown. Karrueche alikuwa akijichekeshachekesha huku akimhoji kuhusiana na mwanamuziki ambaye Diamond anamkubali ambapo alijibu ni Chris Brown, wote wakajikuta wakiangua kicheko.
Kana kwamba hiyo haitoshi , Karrueche muda wote aliendelea kumshangaa na mwisho wa siku wakabadilishana namba za simu.
MASTAA MACHO JUU
Ulipofika wakati wa utoaji tuzo katika kategori ya Mwanamuziki Bora kutoka Afrika, lilipotajwa tu jina la Diamond kutoka Tanzania na wimbo wake wa Number One RMX , mastaa kibao walionesha kushangaa na ndipo macho yote yakahamia eneo aliokuwa amekaa.
Wengi walionekana kutoa maneno ya chinichini sambamba na kumuoneshea vidole wakionesha kumkubali kwa kutinga mjengoni hapo.
NELLY, CHRIS BROWN WAINGIWA KIWEWE
Wakati Diamond anaingia ukumbini , mastaa mbalimbali duniani walionekana kumshangaa na kati yao alikuwa ni Nelly ambaye aliushikilia mkono wa Diamond kwa sekunde kadhaa akitaka waendelee kupiga stori. Diamond akiwa kwenye pozi Wakiwa katika zulia maalum jekundu , Nelly aliyewahi kutamba na wimbo wake maarufu wa Dilemma alionekana na kutaka kumfahamu zaidi Diamond .
Kila sehemu aliyokuwa akienda , Nelly hakutaka kumuacha na alionekana kuambatana naye kwa kumng'ang'ania mkono kila kona akipiga naye picha na kuzunguka eneo lote wakiwa pamoja.
Naye Chris Brown ambaye aliangusha bonge la shoo alionekana kumshangaa Diamond huku akitamani kuendelea kukaa naye.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu ukumbini humo , maswali mengi yaliibuka kuwa iweje , kwa Mtanzania kama yule kukanyaga katika mjengo mmoja na mstaa wa dunia.
TYSON , MAYWEATHER WADUWAA
Mabondia maarufu duniani akiwemo Floyd Mayweather na Mike Tyson walijikuta wakiduwaa kwa kumshangaa kwa kila hatua aliyokuwa anapiga.Macho yao hayakuwa mbali naye na hata katika zulia jekundu , Maywearher , baada ya kumaliza kupiga picha akiwa na mkewe alimfuata.
MASTAA KIBAO WAGOMBEA NAMBA
Wakati shoo hiyo ikiendelea baadhi ya msataa waliokuwa pembeni na Diamond walionekana kumfagilia na hata wengine kuomba namba za simu kwa malengo tofauti ikiwa ni pamoja na kutaka kufanya naye kolabo katika siku za usoni.