Nelson OKWA: Sivunji mkataba wangu bila mil. 800/=

Nelson OKWA: Sivunji mkataba wangu bila mil. 800/=

Baada ya kutamatika kwa safari ya Simba SC kwenye michuano ya Mapinduzi Cup 2023 huko Zanzibar, viongozi wa Simba hawakutaka kulaza damu mara moja wakawasiliana na wakawa (agent) wa mchezaji Nelson Okwa aitwaye Adeniji Jubril Awofe ili waanze mazungumzo ya kuvunja mkataba.

Simba SC wakafanya mazungumzo na kutoa maapenzekezo yao kuhusu kuvunja mkataba. Bwana Awofe akawasiliana na mchezaji wake kumuelezea taarifa kuhusu mapendekezo ya waajili wake.

Majibilu ya Nelson Okwa kwa Bwana yalikuwa "Siko tayari kuvunja mkataba kwa sasa ukizingatia mkaataba wangu unatamatika 2024, hata hivyo kama suala la kuvunja mkataba kwa sasa ni lazima basi kiasi cha USD 380,000/= kitafaa kubadili maamuzi yangu".

Viongozi wa Simba watakaa kikao siku ya jumatatu asubuhi kujadili zaidi suala la wachezaji wa kuachwa ili kutengeneza nafasi kwa ajili ya wengine.

View attachment 2470366
Taarifa imekaa kidakubdaku kutoka utopoloni...
 
Wakome kusajili magarasa
Kisa tu eti alionekana kukinukisha kwenye mechi 2 alizocheza dhidi ya Yanga alipokuwa Rivers United! Wazee wa kukurupuka wakampa mkataba!! Huku wakimpamba kwa kila aina ya mapambio.

Ngoja tuone mwisho wa hili sekeseke! Milioni 800 usawa huu, si mchezo.
 
Apelekwe tu kwa mkopo Yanga.
Hapo nina uhakika atapata namba ya kudumu.
 
Mi ni mpenzi wa Simba,ila wachezaji wanaoingia kwa mchongo,hata kutoka wanapewa mbinu za kuzidi kuikamua club.

Kama mtu aliyehusika kumleta anajulikana,Simba isimchekee,maana ni wazi kuna maksudi

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
Watu pale wanaishi au wanaongeza pesa kwenye akaunti zao kupitia 10% za haya magarasa.
 
Kisa tu eti alionekana kukinukisha kwenye mechi 2 alizocheza dhidi ya Yanga alipokuwa Rivers United! Wazee wa kukurupuka wakampa mkataba!! Huku wakimpamba kwa kila aina ya mapambio.

Ngoja tuone mwisho wa hili sekeseke! Milioni 800 usawa huu, si mchezo.
Kama kambole na biriganya mlivyoingia kichwa kichwa
Kweli uto(nyani) haoni kundule
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Mi ni mpenzi wa Simba,ila wachezaji wanaoingia kwa mchongo,hata kutoka wanapewa mbinu za kuzidi kuikamua club.

Kama mtu aliyehusika kumleta anajulikana,Simba isimchekee,maana ni wazi kuna maksudi

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
Hicho ulichokisema ni kweli kuna baadhi ya viongozi wanakula kupitiw mikataba ya wachezaji na haya ndio yanatesa sana timu zetu hakuna uadilifu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo Simba na Yanga tunachemka kwenye scouting na kuwa fuatilia wachezaji sometimes viongozi wetu ambao hawa hujui mpira wanafanya maamuzi kwa kuangalia mechi moja.
 
Usitutoe kwenye reli suala lililopo mezani ni ishu ya FEI TOO ngja iishe kwanza 😎 😎
 
Kamati ya Usajiri ya Simba ina dhana bado kuwa kila mchezaji mfupi ni Miquissone.
Utailamu Kamati ya Usajili, lakini mimi naungana na Magori kuwa mtu anayepaswa kusajili wachezaji na viongozi wa klabu na sio kocha. Kocha sio mpenzi wala mwanachama wa klabu, ukimpa madaraka ya kusajili mchezaji kwa mkataba wa miaka mitatu wakati yeye hana uhakika wa kudumu kwa hata miezi sita, unafanya makosa. Kocha ndiye aliyependekeza wasajiliwe Okwa na Ouatara, halafu yeye akapata ofa nene sehemu nyingine akawaacha Simba!
 
Back
Top Bottom