Nembo Mpya ya Kigoma Region Tanzania | Jumuiya ya watu wa Kigoma

Nembo Mpya ya Kigoma Region Tanzania | Jumuiya ya watu wa Kigoma

Kigoma Region Tanzania

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2021
Posts
230
Reaction score
611
Imeundwa August 25/ 2024 na kufanyiwa maboresho August 26-27/2024
LOGO Imeundwa na Kamati yetu ya Ubunifu kwa kushirikiana na kampuni ya Strain Org inayomilikiwa na MwanaKigoma.

Imeundwa Kwa Gharama ya Tsh 110'000 + 30'000 za usajili. Nembo imeshakabishiwa BRELA kwa ajili ya usajili.

1725066360369.png


NEMBO imebeba vielelezo 14 vinafafauliwa hapo chini.
UFAFANUZI WA NEMBO MPYA

1-Duara nyembemba la mwanzo (Ring ya juu kabisa):
Inawakilisha muunganiko wa watu wa Kigoma ambao hawaishi Kigoma wapo Mbali na Kigoma lakini wanafuatilia na kutamani yale yanayoendelea Kigoma. Na hii inaleta taswira kwamba Jumuiya yetu itafanya kazi kitaifa zaidi kuunganisha watu wote wa mkoa wa Kigoma.

1725066521855.png


2-Duara Nene la pili (Ring iliyobeba maneno):
Inawakilisha Wanajamii wa Mkoa wa Kigoma wanaoishi ndani ya mkoa wa Kigoma, hii inajumuisha wazawa ambao hadi sasa wanaishi mkoani Kigoma. Ni kwa mwanakigoma yeyote yule anayeishi mkoani Kigoma.

1725066564984.png


3-Maneno JUMUIYA YA WATU WA KIGOMA:
Jamii ya watu wa Kigoma ni JUMUIYA> Hivyo sisi ni JUMUIYA YA WATU WA KIGOMA (Mkusanyiko wa watu wa Kigoma) wenye malengo maalumu katika kusukuma kurudumu la maendeleo ndani ya mkoa wetu.

1725066602152.png


4-Duara Nyembemba la Ndani.
Inawakilisha wale ambao sio wazawa pia hawana asili ya Kigoma lakini wanaipenda Kigoma na wanaishi Kigoma au kuja kutembelea mara kwa mara, ikiwemo wale walio olewa na kuoa ndani ya Jamii ya Kigoma. Ni kwa yeyote yule anayeishi mkoani Kigoma ima kwa ajira, biashara, utalii, kazi au makazi.

1725066685798.png


5-Jengo la kituo cha gari moshi:
Ni Kituo cha Reli cha Kigoma ambacho ni kivutio cha Watalii, kilichojengwa wakati wa Ukoloni wa Ujerumani mwaka 1912. Wajerumani walijenga kituo hicho na majengo kadhaa mkoani Kigoma kuanzia miaka ya 1902.

1725066723715.png


6-Mawimbi ya Ziwa Tanganyika nyuma ya Station:
Inawakilisha msongamano na uthabiti wa mawimbi ndani ya Ziwa Tanganyika.

1725066776288.png


7-Samaki Mgebuka akichupa kwenye mawimbi ya maji:
Mgebuka ni samaki maarufu zaidi katika Ziwa Tanganyika. Samaki huyu wa maji baridi hupikika mapishi yote na akasalia na ladha. Maisha yake ni kwenye maji ya lindi la kati na huzaliana hasa majira ya masika.

1725066862808.png


8-Ramani ya Ziwa Tanganyika:
Ni ziwa kubwa zaidi la ufa barani Afrika na ziwa la pili kwa ukubwa duniani kwa ujazo. Ziwa Tanganyika liko ndani ya Ufa wa Albertine, tawi la magharibi la Ufa wa Afrika Mashariki, na limezuiliwa na kuta za milima za bonde la ufa. Ni ziwa kubwa zaidi la ufa barani Afrika na ziwa la pili kwa ukubwa duniani kwa ujazo.

1725066973411.png


9-Ramani ya mkoa wa Kigoma:
Kigoma inapatikana Magharibi mwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mkoa una wilaya 6 ambazo ni Wilaya ya Kasulu‎, Wilaya ya Kibondo‎, Wilaya ya Kigoma Mjini‎, Wilaya ya Uvinza, Wilaya ya Kakonko na Wilaya ya Buhigwe.

1725067008630.png


10-Zao la mgazi (Chikichi) katika Ramani:
Michikichi ni zao mojawapo ya mazao ya mafuta ambalo hulimwa kwa wingi katika mkoa wa Kigoma, hapa nchini Tanzania. Kwa mwaka huzalisha zaidi ya tani 2,000 za mawese na zaidi ya tani 450 za mafuta ya mise. Zao la mchikichi limekuwa mkombozi kwa wakulima wengi wa Mkoa wa Kigoma.

1725067044983.png


11-RANGI YA DARK BLUE:
Inawakilisha muonekano wa maji ya mbali (gezi) ndani ya Ziwa Tanganyika, lakini pia ni rangi ya kuvutia katika muonekano wa Nembo. Mzimu wa ziwa Tanganyika unaitwa 'Mwanzalulu' kwa kimanyema, kwa kiha unaitwa 'Mganzaruguru' na kwa kibembe huitwa 'mkangialukulu'

1725067090231.png


12-RANGI YA BLUE SKY:
Inawakilisha muonekano wa maji ya Ziwa Tanganyika na mito na mabwawa mbalimbali ndani ya mkoa wa Kigoma.

1725067125945.png


13-RANGI YA KIJANI:
Kijani inawakilisha uoto wa asili wa aridhi yetu ya KIGOMA pamoja na muonekano wa milima yake.

1725067164392.png


14-RANGI NYEUPE:
Nyeupe inawakilisha matumaini yetu yajayo kwa umoja wetu na dhamira yetu watu wa KIGOMA.

1725067195252.png




NB:
Nembo hii ni ruksa kutumika kwa mwanakigoma yeyote yule anaruhusiwa kuitumia kwa maslahi ya mkoa na kwa wanakigoma, nasio kwa maslahi binafsi.
T-shirt zake na kofia zipo mbioni na zitatangazwa mitandaoni.

Ahsanteni sana.
 
Sababu kwanini haijawekwa picha ya sokwe kwenye NEMBO ya Kigoma, haijadhihirishwa kwasababu SOKWE inawakilishwa na makamanda wetu, Timu yetu ya Mkoa MASHUJAA FC.

Tizama Video
 

Attachments

  • An8-vdNxWsCP-eKQ4nr8AMVA4GkvecKaKRKkAC2pI5GccOLqbRJwVovMLH8PTv5ixufm0dr9-UKGQDjJ02XN7OE.mp4
    3.9 MB
Back
Top Bottom