Nembo ya Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam na maneno yaliyoko katika logo hiyo ni vitu vya kutazamwa upya kwani viko kisiasa zaidi kuliko kitaaluma

Hivi hii nembo ndiyo inawazuia msiingie Ikulu? By the way kila siku nyie ni mambo ya kupinga tu hapa JF
 
MTOA MADA NI MMOJA KATI YA WAPUMBAVU (BONGOLALA). HIYO LOGOS YA TUMAINI NYOKA ANAMAANISHA NINI?
 
Una tatizo tu na mwenge,halafu nembo haisomeshi wala kukupunguzia akili
Mwenge maana yake ni taa,mwangaza nuru,ukisoma pale utaelimika na kupata mwanga zaidi wa kimaisha
Kiufupi ni kwamba mwenge wa UDSM utakutoa kwenye giza nene la kielimu na kifikra
Sasa wewe unaleta nembo ya tumaini,kwamba inasadifu zaidi taaluma,wasio wafuasi wa kristo watakwambia msalaba kwao ni tatizo,usitegemee chuo cha taifa kikaweka msalaba kwenye logo yake kamanda
Kina Zitto na lissu wametokana na mwenge huo huo
 
Maarifa ya sahihi ya kutosha ndio hiyo inayo itwa HEKIMA.
Unaweza kufanya maamuzi sahihi kama una maarifa sahihi ya kitu unacho taka kufanyia maamuzi.

Ukifanya kitu vibaya unaonekana umefanya jambo bila kutumia hekima. Ukianza kupigna na mtu adharani sababu kakukosea wakati ipo sheria inayoweza kumuadhibu mkosaji wako unanekana hauna hekima.
Hekima hapo ni nini? Ni kukosa maarifa ya namna ya kumuadhibu au kumrekebisha mkosaji wako bila madhara makubwa kwako au kwa jamii.
 
Kwa nini unaamini kwamba huo ni mwenge wa uhuru? Kama ni kweli basi uko sawa.

Lakini pengine huo ni mwanga wa kawaida ukiakisi ukipata elimu umepata mwanga.


Kwa nini maneno yawe na shida.

Hekima ni uhuru. Kwa maana nyingine Elimu bila hekima ni bure.
 
Knowledge is merely having clarity of facts and truths, while wisdom is the practical ability to make consistently good decisions in life.
Jamani....!!! How can you be practically able to make consistent good decisions without having clarity of facts and truths on the situation in hand? "There is no wisdom based on mere intuitions" by TUJITEGEMEE on 17/02/2020.
 
Descartes
“Through wisdom, we hear not only prudence in business, but a perfect knowledge of all things that man can know, both the conduct of his life by preserving his health and the invention of all arts. ”

Aristotle
“The wise man has the knowledge of all things, insofar as possible”

Heraclitus
“Wisdom is one thing. It is to know the thought by which all things are led by all things

Utaona hao wana falsafa wote wanasema wisdom ni maarifa ya vitu vyote.
Na maarifa (knowledge) umesema ndio hupatikana kwenye mojawapo ya kazi za vyuo vikuu.

Jee huyo T.S. Eliot anaweza kuwa challenge hao philosophers?
 
Ukiacha tafsiri iliyojificha, hata tafsiri ya moja kwa moja bado ina mashiko kwa huo moto wa UDSM. Tukumbuke hicho chuo kimeanzishwa mwaka 1961, mwaka tuliopata uhuru. Pia, ni chuo kilichoongoza mijadala ya harakati za uhuru Africa. Kina Walter Rodney hawakuja Tanzania (na kufanya kazi UDSM) kuchoma mahindi, walikuja sababu UDSM ilikuwa tanuru la fikra.

Hata ukichukua maana iliyojificha, bado moto huo una maana kwa taasisi za elimu ya juu. Chuo kikuu hakuna NECTA, wigo wa kujipatia maarifa na hekima umepanuliwa sana tofauti na shule za sekondari. Mtu yuko huru kufikiri tofauti, ili mradi tu awe na hoja za kutetea anachoamini. Elimu ya chuo kikuu inakupa hekima ya kujua baya na jema ktk maisha, kwahiyo unakuwa huru. Hufungwi na danganya toto za watawala wala sheria zao mbaya. Hufungwi na tamaduni zilizopitwa na wakati, uko huru kuwaza na kutenda kinyume na tamaduni maana umepewa hekima ya kujua lililo jema.

Mwisho, sio haki kukiweka UDSM na Tumaini Makumira ktk sentensi moja. Huo utakuwa ukoo wa Kambale, mtoto, mama na baba wote wana ndevu. Makumira kuwa na moto wa Teaching, Research and Service ni sawa na kusema kazi ya mama mzazi ni kuzaa-stating the obvious.
 
Hiyo hidden mining unayoiongelea bado hainishawashi na ninaamini siasa ndio ilitumika/ ili-influence katika kubuni hiyo logo miaka hiyo ya sisi kupata uhuru.
 
Kama alivyobainisha kwa usahihi ndugu Sooth hapo juu, UDSM ilianzishwa katika mazingira mahususi ya kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiutamaduni.

Miaka ya mwanzoni mwa 1960, waasisi, pamoja na mambo mengine, waliichukulia elimu ya Chuo Kikuu kama nyenzo muhimu katika kuandaa rasilimali watu bora - yenye ujuzi, maarifa na uzoefu - katika fani mbalimbali, kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu.

Watu walioelimika vyema, ni dhahiri, wangeonyesha kiwango cha juu cha hekima na wangekuwa huru dhidi ya ujinga, maradhi, umaskini na hatimaye kuchangia katika kupiga vita vitisho vya ukoloni mamboleo vya ndani na nje ya nchi.

Kwa sababu hiyo, logo ya UDSM imeakisi, inaendelea kuakisi na hapana shaka itaendelea kuakisi ndoto na matarajio ya waanzilishi wake.
 
Ni kawaida ya watu wavivu wanapokuwa kwenye hali ngumu (kwa ajili ya uvivu wao) hujaribu kutafuta visingizio vya kila aina ili tu ionekana tatizo siyo wao bali linaletwa na kitu kingine. Hata ungekuwa na nembo ya aina gani kama hufanyi kazi kwa bidii na maarifa ni bure tu.
 
Huu utumbo mpelekeo mkeo akakupikie sio kutuletea hapa mtandaoni.
 
Bado nasisitiza mjitafakari kuhusu hiyo logo yenu.
 
Mkuu Salary Slip, mimi si mwanafunzi wala mtumishi wa UDSM; sipo katika nafasi ya kukataa ama kukubali mawazo yako. Maoni yangu ni matokeo ya matumizi ya uhuru na haki zangu za kuwa na maoni na kujieleza.

Hata hivyo, kama mwanafunzi wa zamani wa UDSM, nakumbuka vizuri jinsi logo hiyo, hususani maneno 'hekima ni uhuru' - katika fomu za usajili wa mihula, prospectus, karatasi za mitihani na nyaraka na maeneo mengine muhimu - yalivyokuwa yananikumbusha: umuhimu wa kutafuta, kuwasilisha na kusimamia ukweli; na kudhihirisha hekima kupitia matendo na maneno.

Chuo husika bado kinakabiliwa na vikwazo vingi katika kutoa huduma bora na endelevu kwa wadau wake. Sidhani kama logo ni kikwazo kimojawapo.

Hata hivyo, huenda, hatimaye, wahusika wakatafuta mantiki katikati ya michango yetu.
 
Watu wanasema Tanzania tunatumia mwenge, mwenge ni agano la kishetani na ndio maana nchi yetu maskini.
Naomba niwaulize mbona Marekani wanatumia hiyo alama ya mwenge kwenye ile sanamu kubwa inayoitwa The Statue of Liberty kwanini wao hawajalaaniwa na kubaki maskini.

Pia naomba niulize wale wanao jinadi kupigania Uhuru na Demokrasia huku wakipinga mwenge kwa vigezo vya kidini, kwanini wanafungwa na imani za kidini?
Kwanini serikali ilazimishwe kuamini mambo ya kidini? Uhuru na haki viko wapi hapo kwa maana kuna watu wasio amini ktk mambo ya dini zinazo sema mwenge ni laana au agano na shetani.

Uhuru kamili wa taifa lolote huja kwa kuzingatia kutenganisha dola na dini (Separation of religion and state) na hiyo ndio demokrasia na kutenda haki kwa makundi yote..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…