Nembo ya Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam na maneno yaliyoko katika logo hiyo ni vitu vya kutazamwa upya kwani viko kisiasa zaidi kuliko kitaaluma

Kwa Awamu hii TZ haina changamoto yoyote ile. Ole wako hata useme tu daraja limesombwa na mafuriko, ni wao na wewe hadi wahakikishe kucha hazipo
 
Kati ya watu waliokuwa wasomi ni hao wanaoongelewa kwenye biblia na maandiko mengine matakatifu. Sauli au Paulo alikuwa mwanasheria, Luka alikuwa daktari, Mathayo alikuwa mchumi, Petro alikuwa mwanasayansi ya maji - Marine science, akina Shadrack, Meshack, Daniel, etc walikuwa vijana wasomi wa enzi hizo. Shida ya watu wa leo hata imani yao yenyewe hawaijui vizuri, wanaenda kwa mihemko na kutaka miujiza tu badala ya kwenda katika njia, kweli na uzima.
 
Naomba nianzie hapa....
"ELIMU"
"HEKIMA"
"UHURU"
"SIASA"
Tafakari hayo maneno kwa utashi wako,kisha shirikisha mawazo ya wataalamu waliokufundisha/uliopata ujuzi(maarifa n.k),ongezea na Experience za kimaisha ulizo/unazopitia,mwisho TENGANISHA SIASA na SLOGAN UNAZOONA ZINAFAA kutoka VYUO unavyoihisi/kufikiri vinasadifu Slogan zao.
Hiyo hidden mining unayoiongelea bado hainishawashi na ninaamini siasa ndio ilitumika/ ili-influence katika kubuni hiyo logo miaka hiyo ya sisi kupata uhuru.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
... kwani UDSM wanafundisha "day-to-day experience" au formal education? Day-to-day experience ndiyo inazaa wisdom ambayo huwezi kufundishwa na profesa yeyote.
Imebidi ui-'define' "formal education" ili ionekane kuna aina nyingine za 'education' au bado huelewi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…