Nembo ya Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam na maneno yaliyoko katika logo hiyo ni vitu vya kutazamwa upya kwani viko kisiasa zaidi kuliko kitaaluma

Nembo ya Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam na maneno yaliyoko katika logo hiyo ni vitu vya kutazamwa upya kwani viko kisiasa zaidi kuliko kitaaluma

Kwa Awamu hii TZ haina changamoto yoyote ile. Ole wako hata useme tu daraja limesombwa na mafuriko, ni wao na wewe hadi wahakikishe kucha hazipo
 
Sijui unachobisha ni nini. Vyote unavyosema, knowledge etc, msingi wake wa mwisho ni kumpata mtu aliyestaarabika. Kuhusu Suleman aliyekuambia alikuwa hajaenda shule mdai ada yako. Mfumo wa kiyahudi uliwapitisha vijana kwenye elimu bora sana kuhusu taifa lao na sheria za Mungu. Shida yako ni tafsiri unayoipa elimu, ni finyu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kati ya watu waliokuwa wasomi ni hao wanaoongelewa kwenye biblia na maandiko mengine matakatifu. Sauli au Paulo alikuwa mwanasheria, Luka alikuwa daktari, Mathayo alikuwa mchumi, Petro alikuwa mwanasayansi ya maji - Marine science, akina Shadrack, Meshack, Daniel, etc walikuwa vijana wasomi wa enzi hizo. Shida ya watu wa leo hata imani yao yenyewe hawaijui vizuri, wanaenda kwa mihemko na kutaka miujiza tu badala ya kwenda katika njia, kweli na uzima.
 
Naomba nianzie hapa....
"ELIMU"
"HEKIMA"
"UHURU"
"SIASA"
Tafakari hayo maneno kwa utashi wako,kisha shirikisha mawazo ya wataalamu waliokufundisha/uliopata ujuzi(maarifa n.k),ongezea na Experience za kimaisha ulizo/unazopitia,mwisho TENGANISHA SIASA na SLOGAN UNAZOONA ZINAFAA kutoka VYUO unavyoihisi/kufikiri vinasadifu Slogan zao.
Hiyo hidden mining unayoiongelea bado hainishawashi na ninaamini siasa ndio ilitumika/ ili-influence katika kubuni hiyo logo miaka hiyo ya sisi kupata uhuru.
Habari wakuu,

Binafsi napenda kushauri viongozi wa Chuo hiki kuitazama upya nembo ya chuo kama kweli nembo hiyo inastahili kubaki kama ilivyo au ifanyiwe marekebisho madogo ili iwezeke kusadifu zaidi maswala ya academic kuliko ilivo sasa ambapo,kwa mtazamo wangu,inasadifu zaidi siasa za miaka ya nyuma.

Naposema imekaa kisiasa zaidi simanishi haibebi ujumbe wowote wa kitaaluma, bali ni kwasababu imetoa nafasi kubwa kwa maswala ya kisiasa {mchoro wa Mwenge} kwenye nembo huku mchoro wa kitabu ukipewa nafasi ndogo wakati kazi ya msingi ya chuo ni kuzalisha wataalamu.

Nachojiuliza,mchoro wa Mwenge kwenye nembo ya taasisi inayotoa taaluma inasaidifu nini? Inawezekana nembo ya chuo hiki ni ile ile tangu uhuru hivyo kwa wakati huo, labda kulikuwa na sababu ya kuweka mchoro wa mwenge katika nembo ya chuo ila sidhani kama ni sahihi kuendelea kuwa na mchoro huo kwa wakati tulionao.

Ukiacha mbali swala la mchoro huo wa mwenge,hata maneno yaliyoko katika slogan hiyo nayo sidhani kama yana uhusiano wowote na chuo hicho ambacho kazi yake kubwa ni kuzalisha wataalam(wasomi).

Maneno yaliyoko katika nembo hiyo ni haya:hekima ni uhuru.

Nembo husika ni hii:


Kwa maneno hayo ambayo bila shaka ndio kauli mbiu ya chuo,ni wazi yanaturudisha kule kule kwenye mchoro wa mwenge wa uhuru jambo linalonifanya nijiulize ilitokea tu kama coincedence au ni jambo lililokuwa limekusudiwa?

Nadhani wakati umefika nembo hii itazamwe upya na ifanyiwe marekebisho madogo ingawa jambo hili nalo linaweza kuwa na changamoto zake ingawa sitaki kuamini changamoto hizo ndio zinaweza kuwa kikwazo zaidi tu ya kukosekana dhamira ya kuifanyia mabadiliko nembo hiyo na pengine ni kwakuwa tumeridhika nayo,tumeizoea na hatuoni kasoro yoyote katika hiyo nembo.

Hembu tazameni nembo ya chuo hki kichanga lakini inayosadifu zaidi taaluma kuliko mambo mengine yote katika nembo hiyo bila kusahau uchaguzi mzuri wa maneno yaliyowekwa katika nembo husika.


Jambo hili inawezekana liko hata katika taasisi nyingine lakini haimanishi tukae kimya.

Kama wahusika mpo humu,basi tupeni ufafanuzi wa hiyo logo na hiyo kauli mbiu(moto) labda tunaweza kuelewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
... kwani UDSM wanafundisha "day-to-day experience" au formal education? Day-to-day experience ndiyo inazaa wisdom ambayo huwezi kufundishwa na profesa yeyote.
Imebidi ui-'define' "formal education" ili ionekane kuna aina nyingine za 'education' au bado huelewi?
 
Back
Top Bottom