Nembo ya Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam na maneno yaliyoko katika logo hiyo ni vitu vya kutazamwa upya kwani viko kisiasa zaidi kuliko kitaaluma

Mkuu Salary Slip, mimi si mwanafunzi wala mtumishi wa UDSM; sipo katika nafasi ya kukataa ama kukubali mawazo yako. Maoni yangu ni matokeo ya matumizi ya uhuru na haki zangu za kuwa na maoni na kujieleza.

Hata hivyo, kama mwanafunzi wa zamani wa UDSM, nakumbuka vizuri jinsi logo hiyo, hususani maneno 'hekima ni uhuru' - katika fomu za usajili wa mihula, prospectus, karatasi za mitihani na nyaraka na maeneo mengine muhimu - yalivyokuwa yananikumbusha: umuhimu wa kutafuta, kuwasilisha na kusimamia ukweli; na kudhihirisha hekima kupitia matendo na maneno.

Chuo husika bado kinakabiliwa na vikwazo vingi katika kutoa huduma bora na endelevu kwa wadau wake. Sidhani kama logo ni kikwazo kimojawapo.

Hata hivyo, huenda, hatimaye, wahusika wakatafuta mantiki katikati ya michango yetu.
Pamoja sana mkuu.
 
Hiyo logo ni sawa kabisa. Ni muendelezo ya watu wenye mafungamano ya kisiasa kubeza kila kitu kwa kuona katika mtizamo wa kisiasa.
 
Habari wakuu,

Binafsi napenda kushauri viongozi wa Chuo hiki kuitazama upya nembo ya chuo kama kweli nembo hiyo inastahili kubaki kama ilivyo au ifanyiwe marekebisho madogo ili iwezeke kusadifu zaidi maswala ya academic kuliko ilivo sasa ambapo,kwa mtazamo wangu,inasadifu zaidi siasa za miaka ya nyuma.

Naposema imekaa kisiasa zaidi simanishi haibebi ujumbe wowote wa kitaaluma, bali ni kwasababu imetoa nafasi kubwa kwa maswala ya kisiasa {mchoro wa Mwenge} kwenye nembo huku mchoro wa kitabu ukipewa nafasi ndogo wakati kazi ya msingi ya chuo ni kuzalisha wataalamu.

Nachojiuliza,mchoro wa Mwenge kwenye nembo ya taasisi inayotoa taaluma inasaidifu nini? Inawezekana nembo ya chuo hiki ni ile ile tangu uhuru hivyo kwa wakati huo, labda kulikuwa na sababu ya kuweka mchoro wa mwenge katika nembo ya chuo ila sidhani kama ni sahihi kuendelea kuwa na mchoro huo kwa wakati tulionao.

Ukiacha mbali swala la mchoro huo wa mwenge,hata maneno yaliyoko katika slogan hiyo nayo sidhani kama yana uhusiano wowote na chuo hicho ambacho kazi yake kubwa ni kuzalisha wataalam(wasomi).

Maneno yaliyoko katika nembo hiyo ni haya:hekima ni uhuru.

Nembo husika ni hii:

Kwa maneno hayo ambayo bila shaka ndio kauli mbiu ya chuo,ni wazi yanaturudisha kule kule kwenye mchoro wa mwenge wa uhuru jambo linalonifanya nijiulize ilitokea tu kama coincedence au ni jambo lililokuwa limekusudiwa?

Nadhani wakati umefika nembo hii itazamwe upya na ifanyiwe marekebisho madogo ingawa jambo hili nalo linaweza kuwa na changamoto zake ingawa sitaki kuamini changamoto hizo ndio zinaweza kuwa kikwazo zaidi tu ya kukosekana dhamira ya kuifanyia mabadiliko nembo hiyo na pengine ni kwakuwa tumeridhika nayo,tumeizoea na hatuoni kasoro yoyote katika hiyo nembo.

Hembu tazameni nembo ya chuo hki kichanga lakini inayosadifu zaidi taaluma kuliko mambo mengine yote katika nembo hiyo bila kusahau uchaguzi mzuri wa maneno yaliyowekwa katika nembo husika.

Jambo hili inawezekana liko hata katika taasisi nyingine lakini haimanishi tukae kimya.

Kama wahusika mpo humu,basi tupeni ufafanuzi wa hiyo logo na hiyo kauli mbiu(moto) labda tunaweza kuelewa.
Mkuu ungetoa basi pendekezo la nembo mpya na maneno mapya. Leta mfano wa nembo unayoifikiria tuifanyie kazi
 
Tumaini University is affiliated to religious organization; "Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi. Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi’’.
Mmmmhhh

Uongo wa kuhalalisha Sanamu ili liabudiwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hekima (Utajiri wa maarifa,utambuzi,miiko/moral authority).
Uhuru ( humbleness, utu,Innocently, utii wa sheria bila shuruti,obedience,truth etc)
Mwenge kwenye nembo maana yake ni kumulika maarifa yaliyochini ya bahari/kitabu
na kuyaibua yasambae ulimwenguni kote.
Yote haya yanawezekana tu iwapo mlengwa anayo Hekima/kweli itakayomuweka huru.
 
Habari wakuu,

Binafsi napenda kushauri viongozi wa Chuo hiki kuitazama upya nembo ya chuo kama kweli nembo hiyo inastahili kubaki kama ilivyo au ifanyiwe marekebisho madogo ili iwezeke kusadifu zaidi maswala ya academic kuliko ilivo sasa ambapo,kwa mtazamo wangu,inasadifu zaidi siasa za miaka ya nyuma.

Naposema imekaa kisiasa zaidi simanishi haibebi ujumbe wowote wa kitaaluma, bali ni kwasababu imetoa nafasi kubwa kwa maswala ya kisiasa {mchoro wa Mwenge} kwenye nembo huku mchoro wa kitabu ukipewa nafasi ndogo wakati kazi ya msingi ya chuo ni kuzalisha wataalamu.

Nachojiuliza,mchoro wa Mwenge kwenye nembo ya taasisi inayotoa taaluma inasaidifu nini? Inawezekana nembo ya chuo hiki ni ile ile tangu uhuru hivyo kwa wakati huo, labda kulikuwa na sababu ya kuweka mchoro wa mwenge katika nembo ya chuo ila sidhani kama ni sahihi kuendelea kuwa na mchoro huo kwa wakati tulionao.

Ukiacha mbali swala la mchoro huo wa mwenge,hata maneno yaliyoko katika slogan hiyo nayo sidhani kama yana uhusiano wowote na chuo hicho ambacho kazi yake kubwa ni kuzalisha wataalam(wasomi).

Maneno yaliyoko katika nembo hiyo ni haya:hekima ni uhuru.

Nembo husika ni hii:

Kwa maneno hayo ambayo bila shaka ndio kauli mbiu ya chuo,ni wazi yanaturudisha kule kule kwenye mchoro wa mwenge wa uhuru jambo linalonifanya nijiulize ilitokea tu kama coincedence au ni jambo lililokuwa limekusudiwa?

Nadhani wakati umefika nembo hii itazamwe upya na ifanyiwe marekebisho madogo ingawa jambo hili nalo linaweza kuwa na changamoto zake ingawa sitaki kuamini changamoto hizo ndio zinaweza kuwa kikwazo zaidi tu ya kukosekana dhamira ya kuifanyia mabadiliko nembo hiyo na pengine ni kwakuwa tumeridhika nayo,tumeizoea na hatuoni kasoro yoyote katika hiyo nembo.

Hembu tazameni nembo ya chuo hki kichanga lakini inayosadifu zaidi taaluma kuliko mambo mengine yote katika nembo hiyo bila kusahau uchaguzi mzuri wa maneno yaliyowekwa katika nembo husika.

Jambo hili inawezekana liko hata katika taasisi nyingine lakini haimanishi tukae kimya.

Kama wahusika mpo humu,basi tupeni ufafanuzi wa hiyo logo na hiyo kauli mbiu(moto) labda tunaweza kuelewa.
Tunashukuru kwa mawazo mazuri. Ufafanuzi ni kwamba Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kilianza mwanzoni mwa mwaka 1961 kabla ya mwezi wa 12 tulipopata uhuru. Kilikuwa ni sehemu ya Chuo Kikuu cha London, Uingereza. Hii ni kwa sababu sisi kwa wakati huo tulikuwa chini ya utawala wa Mwingereza. Afrika Mashariki kulikuwa na matawi mengine kama vile Nairobi University na Makerere University.

Kuhusu nembo. Kwanza ifahamike kuwa kabla nembo hiyo haijaanza kutumika kwenye siasa kama unavyosema, ilitumika kwenye taaluma ikimaanisha elimu ni mwanga, humuongoza mwanadamu kulifukuza giza na hivyo kuona njia nayoiendea, kuona suluhisho la matatizo katika jamii,n.k. Hivyo hiyo alama ya mwanga, ilikuja kutumika baadaye kwenye shughuli za nchi, ikiwemo siasa wakimaanisha kile walichomaanisha wasomi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam. Kumbuka miaka ya nyuma enzi za Nyerere, mambo mengi walijifunza kutoka kwa wana taaluma.

Pili kuhusu maneno ya "Hekima ni uhuru" maana yake ni hii: Hekima ni neno la kifalsafa ya kisomi linalomaanisha Maarifa, busara, nk. Kwa Kiingereza ni Knowledge and/or Wisdom. Na neno uhuru halina ile maana ya kisiasa bali hapa neno uhuru lina maanisha kutokuwa mtumwa wa ujinga. Yaani kufumbuka au kufunguka kiakili, Yaani kwa Kiingereza ni Liberation. Yaani kuondokana na mzigo wa ujinga. Maana yake kwa Kiingereza tungeweza kusema kitu kama vile "Knowledge is Liberation" or "Knowledge sets you free" " Knowledge is light", etc. Bahati mbaya au nzuri uzuri huo na alama hizo zikachukuliwa na serikali na wanasiasa wakaziingiza kwenye shughuli zao. Ni jambo la mjadala kama maana ya mwanzo haipo tena au haina umuhimu tena. bali wahusika wanaweza kuboresha. Ukizingatia chuo hiki ni mali ya umma. Pia kumbuka siku hizo ilikuwa ni wakati wa chama kimoja, hivyo wakienda kuomba kutumia kile kinachotumika na taasisi ya serikali haikuwa rahisi kukizuia. Chuo kilikuwa ni sehemu ya seikali. Lakini pia wadau ukiwemo mtoa hoja tunaweza kukubaliana kwamba wale wanaotumia sasa nembo au maneno hayo basi wayaache yatumike na Chuo maana kazi zake zote zina lengo la kuwapa watu mwanga wa kitaaluma na kuwaweka huru mbali na zigo la ujinga. Kumbuka ujinga ulitangazwa ni adui wa nchi na maendeleo.

Asante.
Naamini umepata mwanga hata kama itakuwa ni kwa sehemu.

NB: Ila kwa mfano huu wa nembo ya Chuo cha Tumaini ukiangalia vizuri kuna alama zinazosadifu mmiliki wake ambaye ni Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) au kwa kiingereza ELCT-The Evangerical Lutheran Church in Tanzania. Kuna Msalaba, na alama zingine za Kanisa. Kwa mantiki hiyo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwa na maneno au nembo inayofanana na shughuli za serikali yaweza kuwa ni sahii maana chuo chenyewe ni mali ya serikali.
 
Hekima haifundishwi popote! Kazi ya msingi ya chuo kikuu chochote ni kufundisha, tafiti, na ushauri. Nani duniani humu amewahi kufikia "Hekima ya Sulemani"? Alisomea chuo kikuu kipi kuipata hekima ile? UDSM ijikite kwenye majukumu yake ya msingi badala ya kuambatana na siasa uchwara!
Naona kama vile una jazba isiyo na msingi. Kumbuka yote yafanywayo na Chuo Kikuu msingi wake Falsafa (Philosophy) ambayo ni ngumu sana kuielewa kwa mtu wa kawaida. Na ndi maana nchi zilizoendelea zimewekeza kwenye elimu ili watu wawe na maarifa ya kupambanua mambo. Falsafa ni fikra pevu kwa kila jambo. Hivyo hata katika nyanja zote za kitaaluma, iwe ni uhandisi, utabibu/afya, kilimo, elimu, urubani, sheria, dini, n.k kuna PhD yake. na PhD maana yake ni Doctor of Philosophy. Kwa hiyo Philosophy siyo somo la sanaa au Arts. it cuts across all the disciplines. Yaani ni maarifa ya ngazi ya juu kabisa kwenye eneo husika na husomewa. Wengi huwa wanafikiri mtu akiwa professor ndiye msomi kuliko daktari wa falsafa (PhD). Hapana, kwanza uprofessa hausomewi bali mtu anapandishwa cheo tu kwa kazi anazozifanya akiwa kwa mfano tayari amesomea PhD. Kuna kazi za kuandika vitabu, kufanya utafiti, kutoa ushauri, nk. hizo ndizo humpandisha mtu akafikia ngazi ya professa. Kwa hiyo maneno "Hekima" "Uhuru" kwenye taaluma yana maana zaidi ya yanavyotumika kwenye vitabu vya dini na kwenye siasa. Kwenye taaluma hekima ni maarifa, akili, ufahamu, nk. Neno uhuru kwenye taaluma ni liberation, liberty, set free, be out of ignorance, etc.
 
Tunashukuru kwa mawazo mazuri. Ufafanuzi ni kwamba Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kilianza mwanzoni mwa mwaka 1961 kabla ya mwezi wa 12 tulipopata uhuru. Kilikuwa ni sehemu ya Chuo Kikuu cha London, Uingereza. Hii ni kwa sababu sisi kwa wakati huo tulikuwa chini ya utawala wa Mwingereza. Afrika Mashariki kulikuwa na matawi mengine kama vile Nairobi University na Makerere University.

Kuhusu nembo. Kwanza ifahamike kuwa kabla nembo hiyo haijaanza kutumika kwenye siasa kama unavyosema, ilitumika kwenye taaluma ikimaanisha elimu ni mwanga, humuongoza mwanadamu kulifukuza giza na hivyo kuona njia nayoiendea, kuona suluhisho la matatizo katika jamii,n.k. Hivyo hiyo alama ya mwanga, ilikuja kutumika baadaye kwenye shughuli za nchi, ikiwemo siasa wakimaanisha kile walichomaanisha wasomi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam. Kumbuka miaka ya nyuma enzi za Nyerere, mambo mengi walijifunza kutoka kwa wana taaluma.

Pili kuhusu maneno ya "Hekima ni uhuru" maana yake ni hii: Hekima ni neno la kifalsafa ya kisomi linalomaanisha Maarifa, busara, nk. Kwa Kiingereza ni Knowledge and/or Wisdom. Na neno uhuru halina ile maana ya kisiasa bali hapa neno uhuru lina maanisha kutokuwa mtumwa wa ujinga. Yaani kufumbuka au kufunguka kiakili, Yaani kwa Kiingereza ni Liberation. Yaani kuondokana na mzigo wa ujinga. Maana yake kwa Kiingereza tungeweza kusema kitu kama vile "Knowledge is Liberation" or "Knowledge sets you free" " Knowledge is light", etc. Bahati mbaya au nzuri uzuri huo na alama hizo zikachukuliwa na serikali na wanasiasa wakaziingiza kwenye shughuli zao. Ni jambo la mjadala kama maana ya mwanzo haipo tena au haina umuhimu tena. bali wahusika wanaweza kuboresha. Ukizingatia chuo hiki ni mali ya umma. Pia kumbuka siku hizo ilikuwa ni wakati wa chama kimoja, hivyo wakienda kuomba kutumia kile kinachotumika na taasisi ya serikali haikuwa rahisi kukizuia. Chuo kilikuwa ni sehemu ya seikali. Lakini pia wadau ukiwemo mtoa hoja tunaweza kukubaliana kwamba wale wanaotumia sasa nembo au maneno hayo basi wayaache yatumike na Chuo maana kazi zake zote zina lengo la kuwapa watu mwanga wa kitaaluma na kuwaweka huru mbali na zigo la ujinga. Kumbuka ujinga ulitangazwa ni adui wa nchi na maendeleo.

Asante.
Naamini umepata mwanga hata kama itakuwa ni kwa sehemu.

NB: Ila kwa mfano huu wa nembo ya Chuo cha Tumaini ukiangalia vizuri kuna alama zinazosadifu mmiliki wake ambaye ni Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) au kwa kiingereza ELCT-The Evangerical Lutheran Church in Tanzania. Kuna Msalaba, na alama zingine za Kanisa. Kwa mantiki hiyo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwa na maneno au nembo inayofanana na shughuli za serikali yaweza kuwa ni sahii maana chuo chenyewe ni mali ya serikali.
Nashukuru kwa maelezo yako mazuri ingawa sijui usahihi wake.Hata hivyo,hata wewe bado unaonekana kukiri kuwa kuna umuhimu wa kuitaza upya nembo hiyo hivyo tuwaachie wahusika.
 
Kweli wazungu walileta mfumo wa vyama vingi kutugawa hasa hiki kizazi cha sasa ambacho hakina misingi ni shida, alafu wamedakwa kule Ufipa ndiyo balaa kwenye GPA za 32.
Nembo hii inashida gani jamani maneno ya uhuru, mwenge wa uhuru, maji. Nakama tukiwasikiliza hawa wapumbafu walah tutakosa hata historia yetu hatutaijua.
Na ukishindwa kujiharalisha kisiasa utajiharalisha kwa nembo ya chuo, kweli kifo cha mende kimekaribia tutasikia mengi mara nembo ya taifa ina siasa na ukabila, kesho utasikia bendera ya taifa ina siasa za CCM rangi ya kijani ibadirishwe iwekwe ya nyekundu ya ufipa.
Ni upumbafu na ulofa katika ubora wake (Ben William Mkapa hakukosea)
 
Habari wakuu,

Binafsi napenda kushauri viongozi wa Chuo hiki kuitazama upya nembo ya chuo kama kweli nembo hiyo inastahili kubaki kama ilivyo au ifanyiwe marekebisho madogo ili iwezeke kusadifu zaidi maswala ya academic kuliko ilivo sasa ambapo,kwa mtazamo wangu,inasadifu zaidi siasa za miaka ya nyuma.

Naposema imekaa kisiasa zaidi simanishi haibebi ujumbe wowote wa kitaaluma, bali ni kwasababu imetoa nafasi kubwa kwa maswala ya kisiasa {mchoro wa Mwenge} kwenye nembo huku mchoro wa kitabu ukipewa nafasi ndogo wakati kazi ya msingi ya chuo ni kuzalisha wataalamu.

Nachojiuliza,mchoro wa Mwenge kwenye nembo ya taasisi inayotoa taaluma inasaidifu nini? Inawezekana nembo ya chuo hiki ni ile ile tangu uhuru hivyo kwa wakati huo, labda kulikuwa na sababu ya kuweka mchoro wa mwenge katika nembo ya chuo ila sidhani kama ni sahihi kuendelea kuwa na mchoro huo kwa wakati tulionao.

Ukiacha mbali swala la mchoro huo wa mwenge,hata maneno yaliyoko katika slogan hiyo nayo sidhani kama yana uhusiano wowote na chuo hicho ambacho kazi yake kubwa ni kuzalisha wataalam(wasomi).

Maneno yaliyoko katika nembo hiyo ni haya:hekima ni uhuru.

Nembo husika ni hii:

Kwa maneno hayo ambayo bila shaka ndio kauli mbiu ya chuo,ni wazi yanaturudisha kule kule kwenye mchoro wa mwenge wa uhuru jambo linalonifanya nijiulize ilitokea tu kama coincedence au ni jambo lililokuwa limekusudiwa?

Nadhani wakati umefika nembo hii itazamwe upya na ifanyiwe marekebisho madogo ingawa jambo hili nalo linaweza kuwa na changamoto zake ingawa sitaki kuamini changamoto hizo ndio zinaweza kuwa kikwazo zaidi tu ya kukosekana dhamira ya kuifanyia mabadiliko nembo hiyo na pengine ni kwakuwa tumeridhika nayo,tumeizoea na hatuoni kasoro yoyote katika hiyo nembo.

Hembu tazameni nembo ya chuo hki kichanga lakini inayosadifu zaidi taaluma kuliko mambo mengine yote katika nembo hiyo bila kusahau uchaguzi mzuri wa maneno yaliyowekwa katika nembo husika.

Jambo hili inawezekana liko hata katika taasisi nyingine lakini haimanishi tukae kimya.

Kama wahusika mpo humu,basi tupeni ufafanuzi wa hiyo logo na hiyo kauli mbiu(moto) labda tunaweza kuelewa.

Mkuu. Uko na mind so negative. Unamka. Unalala. Unakula. Huku unaweza kitu gani negative cha kusema na kuandika. It’s bad for your Health.
 
Mkuu Salary Slip, hoja yako ina mantiki kubwa sana, lakini ni vyema tukapata pengine maana ya jumla yaliyopo katika "logo" hii na ni pengine ilikuwa ni sababu ya kihistoria na kimazingira iliyopelekea ikalembwa na maandishi hayo. Kwa maana yangu mwenyewe ambayo si rasmi, tunaweza kuyapambanua maneno haya kama ifuatavyo;

Hekima ni hali ya mtu kutambua mambo muhimu ya mahusiano juu yake yeye mwenyewe na wanadamu wengine, vitu, matukio na mazingira ambayo humuwezesha kufanya uamuzi bora wa kuenenda nayo kwa kila kimoja kati ya hivyo ama kwa baadhi ama pia ujumla wake.

Uhuru ni uamuzi wa kuchagua kuwaza, kunena, kutenda ama kutimiza wajibu pasipo kuvunja sheria, kanuni na utaratibu maalum unaokubalika.

Kwa hiyo basi, kwa muktadha na maudhui ya kihistoria ya chuo hiki, tena kwa kuzingatia kuwa ndicho pekee kilichokuwa cha kwanza hapa nchini baada ya sisi kuwa taifa huru, inawezekana ikawa ndiyo sababu ya kuhusisha neno "Uhuru" ndani yake. Kwa maana ya uwepo wa neno "Hekima" sioni ukakasi wowote juu yake. Kwa maana hiyo "combination" ya maneno haya mawili si ya kubeza, isipokuwa ni kuyapa "due weight"
tapatalk_1581958213820.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumaini University is affiliated to religious organization; "Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi. Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi’’.
Hapana huyo nyoka ndio yule yupo kwenye kilichokuwa kitivo Cha UDSM muhimbili
 
Hekima inasomewa darasani?
Ngoja tuweke kwa kizungu huenda utaelewa na tutajua kama kuna siasa au ni abstract message imewafanya musielewe ujumbe mzito katika hiyo motto sijui tuite Slogan.

HEKIMA NI UHURU = "WISDOM IS FREEDOM".
Jiulize lengo la kutafuta elimu au maarifa pale chuo kikuu ni nini?
Jiulize hekima inapatikananje kama haujazaliwa nayo?
Jiulize hekima inaleta uhuru wa nini au kwa namna ipi?

Huo ni ujumbe mzito sana kuliko akili ya kawaida. Ni Abstract art, ni philosophical message.

Kwa kuanzia tu kujibu hayo maswali nakuambieni mnaodhani hiyo ni siasa.
Hekima huleta uhuru wa fikra.
Hizo fikra ndio hutumika kwenye hizo tafiti, kutoa huduma,kutoa elimu yenye manufaa kwa jamiii, n.k.
Kwa hivyo utaona ujumbe wa kwenye nembo ya Tumaini University upo ndani ya Ujumbe wa nembo ya UDSM.
Ni sehemu moja tu ya ujumbe mkubwa uliopo ktk nembo ya UDSM.

Hekima huleta uhuru wa kujieleza, uhuru wa kuhoji, uhuru kufanya chochote bila kuvunja sheria, Uhuru wa kuchagua kitu unacho amini, uhuru wa kutafuta ukweli(tafiti), uhuru wa serikali kutoingiliwa na dini, n.k.

Mwenge ni alama ya uhuru(a torch is a universal symbol of freedom), kwa kesi hii ya chuo kikuu ni uhuru wa kifikra.
Tunaona uhuru wa kifikra huleta uhuru wa kila kitu kuanzia wa maoni , udadisi, uhuru wa kutafuta maarifa, uhuru wa kutafuta ukweli sio kwa hisia bali kwa kuegemea majibu ya tafiti(facts based in research ), uhuru wa kiuchumi, kutenganisha dola na dini, n.k.

Ni kama vile wamarekani walivyo tumia alama ya mwenge kwenye sanamu la uhuru ile sanamu yao inaitwa kwa kimombo The Liberty Statue.
Lile sanamu limeshika mwenge.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Salary Slip huwa nakuheshim Sana na ofcourse niliona nyuzi yako, lazima niifungue. Lakin kama utaendelea kuwa unapandisha nyuzi Level one kama hizi,nitakushusha kwenye orodha ya watu wa JF ambao nasoma nyuzi zao kwa umakini.
 
Back
Top Bottom