Nembo ya Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam na maneno yaliyoko katika logo hiyo ni vitu vya kutazamwa upya kwani viko kisiasa zaidi kuliko kitaaluma

Nembo ya Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam na maneno yaliyoko katika logo hiyo ni vitu vya kutazamwa upya kwani viko kisiasa zaidi kuliko kitaaluma

Hakuna mwanadamu anayezaliwa na hekima.Hata sulemani hakuzaliwa na hekima.Ndio maana hata Mungu kwenye biblia amesema wazi "mtu akipungukiwa na hekima na aombe" kwa hiyo hekima inapatikana baada ya kuzaliwa na wala si kuzaliwa nayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
... na wala hekima haifundishwi darasani. Tuko pamoja.
Niliuliza kule juu kama hekima hujazaliwa nayo unawezaje kupata hekima?
Swali kubwa sana hili kama wewe ni great thinker na hauendeshwi na siasa au na hisia za kidini.
Simaanishi usifuate imani za kidini, lakini lazima utambue wakati gani kwa muktadha upi usiegemee kiimani za kidini unapotafuta ukweli wa kitu au unapofanya mjadala.

Hekima(widom) huja kwa kujifunza na kufunzwa maarifa(knowledge) flani, kwa msisitizo tunasema ukiwa na maarifa ya vitu vingi sana ndipo unakuwa na hekima.
Na University ni sehemu wanayokuza fundisha na kukuza maarifa kwa uhuru na kiwango cha juu kabisa.
At the university is where the true enlightenment is practiced if and only if that institute is operated fully autonomous, free from religious and state interference.
 
hakuna haja ya kubadili slogani Ya hekima ni uhuru.Ni kweli kuwa hekima haifundishwi popote lakin Hekima inapatikana kutokana na mambo mbalimbali kwa pamoja.Mojawapo ni elimu,malezi ya wazazi na jamii inayotuzunguka.Miaka ya 2010 kurudi nyuma chuo hiki kilikuwa mstari wa mbele kufanya hekima itamalaki.Lakini siasa za majitaka zikajitungia sheria za kuwabana wanaUDSM kuendesha tena ile midahalo ya wazi ambayo ilikuwa inachochea maarifa ndio maana hata serikali kwa kutambua hilo katika sh.Mia5 noti wakaweka ukumbi wa Nkurumah kutokana na hekima iliyokuwako pale.Watu walitoa maoni kwa uhuru kabisa.
Cha kufanya ni rais ajaye kurusisha tena midaharo vyuoni ili wajadili changamoto zinazoikabili nchi ili zipatiwe fumbuzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Miaka ya leo akitokea professa au msomi mwingine yeyote anachambua changamoto za nchi yetu huyo ni adui wa nchi na msaliti mkubwa na anapaswa kupigwa risasi mchana kweupe! Hata ukionekana umepiga picha ya shimo lililopo katikati ya barabara unasakwa na polisi usiku na mchana.
 
mbona hii logo ya Tumaini ni kama Nembo ya kanisa tuu
 
Kuna watu hawana elimu lakini wana busara hasa.
Mkuu samahani kwa kauli hii, ningependa kujua elimu yako ni kiwango gani?
Kama umefikia elimu ya shahada ya kwanza kuna kitu hakiko sawa ktk mfumo wako wa kujifunza ukiwa shuleni na vyuoni.

The wisdom in philosophy
From the Latin sapientia, it relates to intelligence, in the opinion, common sense, prudence, knowledge, science, philosophy. Wisdom is commonly used to describe the character of that which is reasonable, or to exercise moderation in desires.
Source: What is Wisdom ? Philosophical Definition

Ukisoma hapo kwenye nini maana ya wisdom(hekima) utaona inahusiana na vitu vingi ikiwemo na knowledge, science na phylosophy.

Je elimu ya chuo kikuu lengo lake sio kukupatia knowledge?
Je kazi ya chuo kikuu sio kukupa mbinu za kisayansi na kutambua asili ya vitu kisayansi?
Au kutafuta majibu ya vitu mbalimbali au changamoto mabalimbali zinazo ikabili jamii au dunia kwa njia za kisayansi kupitia hizo tafiti (research) unazo sema?

Go back to the college mkuu wangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui unachobisha ni nini. Vyote unavyosema, knowledge etc, msingi wake wa mwisho ni kumpata mtu aliyestaarabika. Kuhusu Suleman aliyekuambia alikuwa hajaenda shule mdai ada yako. Mfumo wa kiyahudi uliwapitisha vijana kwenye elimu bora sana kuhusu taifa lao na sheria za Mungu. Shida yako ni tafsiri unayoipa elimu, ni finyu sana.
Naomba nitofautiane na wewe; lengo la msingi la chuo kikuu ni kupata KNOWLEDGE not WISDOM! Ni kupata MAARIFA sio HEKIMA! Hakuna mahali popote darasani uliwahi kukaa ili ufundishwe HEKIMA; tunaingia darasani kupata MAARIFA. Huwezi kuniambia wote ambao hawajafikia elimu ya chuo kikuu au ambao hawajasoma (darasani) kabisa hawana HEKIMA!

"Where is the wisdom we have lost in knowledge? Where is the knowledge we have lost in information?" —T.S. Eliot. Knowledge is gathered from learning and education, while most say that wisdom is gathered from day-to-day experiences and is a state of being wise. Knowledge is merely having clarity of facts and truths, while wisdom is the practical ability to make consistently good decisions in life.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
As it is to wisdom, learning is a change in behavior resulting from experiences and esposure. A change in behaviors after passages of years, yields what we call wisdom.
Naomba nitofautiane na wewe; lengo la msingi la chuo kikuu ni kupata KNOWLEDGE not WISDOM! Ni kupata MAARIFA sio HEKIMA! Hakuna mahali popote darasani uliwahi kukaa ili ufundishwe HEKIMA; tunaingia darasani kupata MAARIFA. Huwezi kuniambia wote ambao hawajafikia elimu ya chuo kikuu au ambao hawajasoma (darasani) kabisa hawana HEKIMA!

"Where is the wisdom we have lost in knowledge? Where is the knowledge we have lost in information?" —T.S. Eliot. Knowledge is gathered from learning and education, while most say that wisdom is gathered from day-to-day experiences and is a state of being wise. Knowledge is merely having clarity of facts and truths, while wisdom is the practical ability to make consistently good decisions in life.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu hawana elimu lakini wana busara hasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hivyo hii inaondoa ukweli kwamba maarifa (knowledge) itokanayo na taasisi za elimu humuongezea hekima msomi?
Hata hao wasio soma wamejifunza maarifa yanayo wafanya kuwa na buasara kwa njia isiyo rasmi (learning through informal education).
 
Ukisoma essence ya vyuo vikuu duniani utakuja kufuta hii komment yako mkuu. Soma angalau rejea kidogo juu ya ni nn sababu ya uwepo wa vyuo vikuu, haya unayosema ya teaching, consultancy na research hayapo; yanaingia in an operational way. Chuo kikuu kinatakiwa kifundishe watu kujua jambo jema wanalotakiwa kutenda " a pursuit for goodness". Sasa namna ya kulifikia hili ndipo yanapoingia haya mambo yako unayoyataja.
HEKIMA inachangiwa na vitu vingi sio elimu ya darasani peke yake; na wala hakuna shule au chuo chochote kinachofundisha HEKIMA. Jukumu la msingi la chuo kikuu chochote ni kutoa MAARIFA so slogan ya UDSM iendane na jukumu lake la msingi - MAARIFA. HEKIMA ni matokeo ya vitu vingi katika maisha na sio elimu ya darasani peke yake!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka ya leo akitokea professa au msomi mwingine yeyote anachambua changamoto za nchi yetu huyo ni adui wa nchi na msaliti mkubwa na anapaswa kupigwa risasi mchana kweupe! Hata ukionekana umepiga picha ya shimo lililopo katikati ya barabara unasakwa na polisi usiku na mchana.
Tunaelekea gizani.UDOM tangia chuo kimeanza hawajawahi hata kufanya mdahalo wa kitaifa kuhusu kitu chochote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli kuwa hekima haifundishwi popote
Mkuu It is agreed on all sides (Eastern and Western philosophies) that wisdom involves the direction of life by relevant knowledge, and thus, that it incorporates both a theoretical and a practical element. -- source: Can Wisdom Be Taught? | Dallas Willard

Utaona kwamba chuo kikuu na taasisi zingine za elimu ndio unaweza kufundishwa maarifa flani ambayo ukiyatumia, huku ukichanganya na uzoefu na mtazamo wako kuhusu mambo flani kutokana na uzoefu wako ndio unaweza kufanya mahamuzi sahihi na ya haki ( good judgement) ambayo ndio mojawapo ya vitu tunavyo ita hekima.

Hata Sulemani (Solomon) alisifika kuwa na hekima kutokana na kufanya mahamuzi ya haki au tuite mazuri (good judgement) kwenye matukio mablimbali katika uongozi wake.
Hatuwezi kusema moja kwa moja hekima hufundishwa darasani bali vitu vinavyofundishwa darasani na nje ya darasa vinasaidia uweze kufanya vitu kwa hekima.
 
Ukiacha tafsiri iliyojificha, hata tafsiri ya moja kwa moja bado ina mashiko kwa huo moto wa UDSM. Tukumbuke hicho chuo kimeanzishwa mwaka 1961, mwaka tuliopata uhuru. Pia, ni chuo kilichoongoza mijadala ya harakati za uhuru Africa. Kina Walter Rodney hawakuja Tanzania (na kufanya kazi UDSM) kuchoma mahindi, walikuja sababu UDSM ilikuwa tanuru la fikra.

Hata ukichukua maana iliyojificha, bado moto huo una maana kwa taasisi za elimu ya juu. Chuo kikuu hakuna NECTA, wigo wa kujipatia maarifa na hekima umepanuliwa sana tofauti na shule za sekondari. Mtu yuko huru kufikiri tofauti, ili mradi tu awe na hoja za kutetea anachoamini. Elimu ya chuo kikuu inakupa hekima ya kujua baya na jema ktk maisha, kwahiyo unakuwa huru. Hufungwi na danganya toto za watawala wala sheria zao mbaya. Hufungwi na tamaduni zilizopitwa na wakati, uko huru kuwaza na kutenda kinyume na tamaduni maana umepewa hekima ya kujua lililo jema.

Mwisho, sio haki kukiweka UDSM na Tumaini Makumira ktk sentensi moja. Huo utakuwa ukoo wa Kambale, mtoto, mama na baba wote wana ndevu. Makumira kuwa na moto wa Teaching, Research and Service ni sawa na kusema kazi ya mama mzazi ni kuzaa-stating the obvious.
Asante kwa kumjibu. Ingawa wanasema aliyelala usimwamshe ukimwamsha utalala Mwenyewe. Jamaa yuko usingizini pia gizani asaidiwe nuru ikibidi apewe mwenge umumulikie. Huwezi kujadili nembo iliyoandaliwa na vichwa vya Hali ya juu wakati bado uko first year ktk chuo cha kata na ndo umebalehe. Asemehewe tu.
 
"Where is the wisdom we have lost in knowledge? Where is the knowledge we have lost in information?" —T.S. Eliot. Knowledge is gathered from learning and education, while most say that wisdom is gathered from day-to-day experiences and is a state of being wise. Knowledge is merely having clarity of facts and truths, while wisdom is the practical ability to make consistently good decisions in life.
Nikiwa nakubaliana na definition hizi.
Niambie kama "day to day experience" sio 'education.'
Kwani 'education' ni lazima mtu akae darasani?
 
Nikiwa nakubaliana na definition hizi.
Niambie kama "day to day experience" sio 'education.'
Kwani 'education' ni lazima mtu akae darasani?
... kwani UDSM wanafundisha "day-to-day experience" au formal education? Day-to-day experience ndiyo inazaa wisdom ambayo huwezi kufundishwa na profesa yeyote.
 
Back
Top Bottom