Nembo ya TBS inatusaidia Nini kwenye udanganyifu wa bidhaa za viwandani?

Nembo ya TBS inatusaidia Nini kwenye udanganyifu wa bidhaa za viwandani?

Shoctopus

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2015
Posts
3,434
Reaction score
1,985
Niende moja kwa moja katika mada:
1. Mikate. Kila kipindi uzito na ukubwa (weight and volume) hupungua, Bei iko palepale au inapanda!
Swali kwa TBS: Hiyo nembo yenu inahusu kifungashio au bidhaa iliyomo. Kama inahusu mkate wenyewe hili la hapo juu hamlioni au ubabaishaji?
2. Dawa za mswaki, (tooth paste). Kwa mfano: tube ya 70 gm net weight; imeandikwa "Approved by: TBS..." Maana yake hiyo ni uzito sahihi wa bidhaa yenyewe au ni pamoja na hewa iliyojazwa humo kwenye tube? Kwasababu ukiona bokisi lake na tube ni kubwa, lakini ukikamua dawa unakuta sehemu kubwa limejazwa hewa? Hamuoni huu udanganyifu au mnababaisha na hamjuwi mnachofanya?
3. Vibiriti navyo, mambo ni hayohayo! Vijiti pungufu, baadhi havina baruti, wakati wa mvua haviwaki kabisa! vingine vinalipuka hovyo usipojihami utaungua. Sasa linembo lenu humo linahusu nini? Zamani kulikuwa na vibiriti vilikuwa vinawaka hata vikilowana! Kama ni hivi, jamani TBC mnatupeleka mbele au tunaturudisha nyuma?
Naweza kutaja bidhaa nyingi ambazo zina nembo yenu lakini hazina ubora kulingana na standards zinazotakiwa. Msingoje eti mpate malalamiko ndipo mfanye kitu, kama ni madhara mtawafidia waathirika?
TUMECHOKA!
 
Hawana impact yeyote ile either positive au negative
 
Back
Top Bottom