Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Salaam Wakuu,
Baada ya Mdau wa JamiiForums aliyejitambulisha kama Dereva kudai NEMC imewachelewesha Mpani kwa wiki Mbili, NEMC wamewataka Madereva hao kuwasiliana na Wakala wao.
"Kwa muda wa takriban wiki mbili magari yetu ambayo ambayo yana mizigo ya skrepa kutoka Malawi kwenda Uganda na Rwanda yamezuiwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa sababu ambazo hazieleweki."
Hapa Chini ni Kauli ya NEMC kumjibu huyu Mdau wa JamiiForums.com.
NEMC wamesema;
" Kanuni ya usimamizi wa taka hatarishi ya mwaka 2021 inaelekeza taka hatarishi zinazosafirishwa kupitia nchini baada ya kupata kibali cha Mhe. Waziri mwenye dhamana ya Mazingira lazima zisindikizwe hadi mpaka wa kutokea.
Baraza (NEMC) limekuwa likifanya hivyo baada ya taratibu za Forodha kukamilika. Wakala wa wasafirishaji wa taka hatarishi wamekuwa wanaomba kusindikizwa kwa Malori pindi wanapokuwa wamekamilisha taratibu za Forodha upande wa Malawi na upande wa Tanzania.
Wakala alileta maombi ya kulipia Magari 12 ambayo aliyalipia lakini pia kaomba kulipia malori Magari 3 na kulipia tarehe 5. Wakati wakiendelea na taratibu za Forodha wakala akawasiliana na Baraza na kuomba kulipia Malori 15 Ili taratibu ya kuyasindikiza zifanyike kwa wakati Mmoja, na Jana tarehe 7/12/2024 jioni ndo amekamilisha malipo ya haya malori.
Baraza limekuwa likitaarifiwa na wakala wa wasafirishaji baada ya kukamilisha taratibu za Forodha na kutoa hiyo huduma ya kusindikiza malori kama Sheria inavyoelekeza.
Changamoto kubwa ni pale madereva wanapotoa taarifa kwenye vyombo vya habari kabla ya kuwasiliana na mawakala wao.
Wakati mwingine ofisi imekuwa ikichukuwa hatua ya kwenda kusindikiza malori na wakala kutokamilisha baadhi ya taarifa, na kusababisha baadhi ya malori kuchelewa kuondoka kama ratiba ilivyopangwa. Wakati mwingine kwa kupewa taarifa kuwa upande wa forodha Malawi bado taratibu hazijakamilika ndo maana malori yameshindwa kuondoka.
Ikumbukwe hizi ni taka hatarishi lazima utaratibu uliyowekwa kwa mujibu wa Sheria ufuatwe.
Baraza limekuwa linawasiliana na wakala wa wasafirishaji kabla ya kupeleka timu ya kusindikiza. Kwa malori haya ambayo yapo mpakani ndo jana wamekamilisha malipo na ofisi inategemea kuyasindikiza baada ya taratibu za Forodha kukamilika na wakala kututarifu kuwa taratibu zote zimekamilika.
NEMC ipo kutoa huduma kwa watu wote, hivyo tuwashauri madereva wawe wanawasiliana na mawakala wa wasafirishaji Ili kuondoa sintofahamu."