Faana
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 38,657
- 44,759
Naandika kwako Mkurugenzi wa NEMC - HQ kwamba huku mitaani hasa katika miji kelele za miziki kwenye ma bar, pub saloon za vinyozi, wauza CD, vigodoro pamoja na nyumba za ibada zimekuwa kero kiasi kwamba Mamlaka yako inaonekana ipo tu kama bendera inatumia fedha za serikali bila tija. Kuna namba za simu 0800110115 imekuwa ukipiga kutoa taarifa hazina msaada wowote, wanaokuwa directed kushughulikia kero hawana hata kipimo cha kupimia uzito wa kelele.
Nakushauri utengeneze kikosi kazi cha kitaifa, kazi yake iwe kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi na kuyafanyia kazi moja kwa moja kutokea ofisini kwako kwasababu wawakilishi wenu walioko kwenye miji hawafanyii kazi kero wanazopelekewa kutokana na kupokea rushwa.
Ikiwa kikosi kazi chako kitakuwa na ufanisi, upo uwezekano wa NEMC kukusanya fine kwa wingi kutoka kwa wavunja sheria hao na kuiongezea serikali mapato.
Kiuhalisia hali ilivyo hivi sasa ni kama Mamlaka yako haipo, na kama ipo basi watendaji wako wameshindwa kazi kabisa.
Tunaomba ulichukulie suala hili kwa uzito wake.
Nawasilisha