NEMC: Huku Mitaani Tunateseka Kelele za Miziki Bar Zimezidi

NEMC: Huku Mitaani Tunateseka Kelele za Miziki Bar Zimezidi

Tena hawa wenye vi library vya kuburn CD ndo kero kubwa,wanatune volume mpka mwsho..iwe mchana au usiku...na mtaani wametanda kila kona
 
Naandika kwako Mkurugenzi wa NEMC - HQ kwamba huku mitaani hasa katika miji kelele za miziki kwenye ma bar, pub saloon za vinyozi, wauza CD, vigodoro pamoja na nyumba za ibada zimekuwa kero kiasi kwamba Mamlaka yako inaonekana ipo tu kama bendera inatumia fedha za serikali bila tija. Kuna namba za simu 0800110115 imekuwa ukipiga kutoa taarifa hazina msaada wowote, wanaokuwa directed kushughulikia kero hawana hata kipimo cha kupimia uzito wa kelele.

Nakushauri utengeneze kikosi kazi cha kitaifa, kazi yake iwe kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi na kuyafanyia kazi moja kwa moja kutokea ofisini kwako kwasababu wawakilishi wenu walioko kwenye miji hawafanyii kazi kero wanazopelekewa kutokana na kupokea rushwa.

Ikiwa kikosi kazi chako kitakuwa na ufanisi, upo uwezekano wa NEMC kukusanya fine kwa wingi kutoka kwa wavunja sheria hao na kuiongezea serikali mapato.

Kiuhalisia hali ilivyo hivi sasa ni kama Mamlaka yako haipo, na kama ipo basi watendaji wako wameshindwa kazi kabisa.

Tunaomba ulichukulie suala hili kwa uzito wake.

Nawasilisha
Kweli kabisa kila familia ina Mambo yake unakuta nyingine ndani Kuna wagonjwa!!
 
Ungetaja jina la bar na kanisa. Kimara tumewakomesha wajinga fulani wanajiita LA CASA PUB walikuwa wajinga sana kelele mtindo mmoja kisa ilikuwa sijui na mahusiano na Kitila Mkumbo. Hawa wenye hizi bar hawaheshimu kbs afya ya masikio. Paza sauti.
Mkuu si rahisi kutaja kwa mfano hawa wanao hubiri na mispika mikubwaaaa, mziki kama wote masauti mpaka mwisho utawataja majina kweli watu wanatembea na midubwana wamejitwisha kichwani kelele zake sio za kawaida mkuu
 
mleta mada umekuja na
Mada yenye kuhitaji ufumbuzi,

hili kwa kweli limekuwa ni kero na sina uhakika kama ni mamlaka ipi yenye kusimamia hili kwa sababu kwenye makazi ya watu ndipo pia kunayo makanisa,baa na grocery na hata wakati mwinhine unaweza kuta kunayo hata maduka yenye kuuza albam za muziki hizi biashara tajwa zote wanasumbua sana usiku kwa kelele zao hawawapi watu nafasi ya kulala ili kesho yake waamke wakiwa safi na waweze kuyawahi majukumu

kwa
Kawaida kwa mtu mwenye kujitambua na kuijali afya yake usiku ni muda wa kulala baada ya mtu kuwa amechoka na kwa sababu pia anahitaji kuamka akiwa mwenye afya ya
mwili na akili ili aweze kwenda tekeleza tena majukumu

ikiwa atafunguliwa muziki kwa muda huo hii inasababisha shida kwa afya yake na hata kuzorotesha utendaji wake wa kazi kwa siku inayofuata

Ninashauri baa na hata grocery ziwepo lakini hii sehemu ya kupata huduma ya kinywaji na isiwe ni ya kupata huduma ya muziki
Huduma ya
Muziki ipatikane kwenye majumba ya muziki na ambayo yamewezeshwa kutengenezwa kwa namna ambayo sauti haitoki nje kuwabugudhi wasiohitaji huduma hiyo ili mtaani kuwe na ustaarabu
Asante sana mkuu, hili jambo kwa sasa linahitaji nguvu kubwa sana kulipigania kwasababu hivyo vyombo vya muziki vimekuwa vingi vinauzwa kwa bei ya chini, kila mtu ananunua na kuweka popote anapotaka ati kwakuwa hakuna sheria inayowazuia, spika kubwa zimetapakaa kila mtaa mppaka zimekuwa kero, nadhani ipo haja zitungiwe sheria, naweza kusema Mamlaka husika ijitathimini kuona kama wanaitendea haki serikali yao
 
Hawaendelei. Lakini shida kubwa ipp kwa watoa vibali na hasa wenyeviti wa serikali za mitaa.
Hivi kabla ya bar kuwekwa sheria inasemaje? Maana siku hizi unalala unaamka mtu amefungua bar hakuna wa kumgusa
 
Unaingie salon unakuta mziki mpaka wote unashindwa kusema naomba mpunguze mziki halafu unasubiri so called NEMC waje wawanyamazishe wakati na wao wananyoa humo humo
NEMC wanalaumiwa kwakuwa wanapewa taarifa wanazikalia kimya, wanapota mitaani wanaona hali halisi ilivyo hawachukui hatua
 
Mbaya zaidi wanasema muziki usizidi db 8, lakini hata wao wenyewe hawana sound meter sijui huyo mwenye bar ataipata wapi hiyo db 8
 
NEMC wanalaumiwa kwakuwa wanapewa taarifa wanazikalia kimya, wanapota mitaani wanaona hali halisi ilivyo hawachukui hatua

Hawana faida hao bora ingefutwa tu
Sioni kazi yao kabisa na serikali inawaangalia tu
Tuna watu wa hovyo sana na sisi wenyewe tunashindwa kukemea kwa virendo bali tunakubali yaendelee
 
Mkuu si rahisi kutaja kwa mfano hawa wanao hubiri na mispika mikubwaaaa, mziki kama wote masauti mpaka mwisho utawataja majina kweli watu wanatembea na midubwana wamejitwisha kichwani kelele zake sio za kawaida mkuu
Hawa wapo mitaani mchana kabisa. Mitaa ya Kariakoo ni maarufu. Nani anawapa vibali?
 
NEMC wanalaumiwa kwakuwa wanapewa taarifa wanazikalia kimya, wanapota mitaani wanaona hali halisi ilivyo hawachukui hatua
Watupe namba zinazopokelewa saa 24 na kufuatiliwa papo kwa papo.
 
Watupe namba zinazopokelewa saa 24 na kufuatiliwa papo kwa papo.
Huwezi kuamini na wao wanaishi kwenye mitaa yenye changamoto hizo ila hawajui nani wa kumpelekea malalamiko
 
Back
Top Bottom