NEMC: Huku Mitaani Tunateseka Kelele za Miziki Bar Zimezidi

Tena hawa wenye vi library vya kuburn CD ndo kero kubwa,wanatune volume mpka mwsho..iwe mchana au usiku...na mtaani wametanda kila kona
 
Kweli kabisa kila familia ina Mambo yake unakuta nyingine ndani Kuna wagonjwa!!
 
Ungetaja jina la bar na kanisa. Kimara tumewakomesha wajinga fulani wanajiita LA CASA PUB walikuwa wajinga sana kelele mtindo mmoja kisa ilikuwa sijui na mahusiano na Kitila Mkumbo. Hawa wenye hizi bar hawaheshimu kbs afya ya masikio. Paza sauti.
Mkuu si rahisi kutaja kwa mfano hawa wanao hubiri na mispika mikubwaaaa, mziki kama wote masauti mpaka mwisho utawataja majina kweli watu wanatembea na midubwana wamejitwisha kichwani kelele zake sio za kawaida mkuu
 
Asante sana mkuu, hili jambo kwa sasa linahitaji nguvu kubwa sana kulipigania kwasababu hivyo vyombo vya muziki vimekuwa vingi vinauzwa kwa bei ya chini, kila mtu ananunua na kuweka popote anapotaka ati kwakuwa hakuna sheria inayowazuia, spika kubwa zimetapakaa kila mtaa mppaka zimekuwa kero, nadhani ipo haja zitungiwe sheria, naweza kusema Mamlaka husika ijitathimini kuona kama wanaitendea haki serikali yao
 
Hawaendelei. Lakini shida kubwa ipp kwa watoa vibali na hasa wenyeviti wa serikali za mitaa.
Hivi kabla ya bar kuwekwa sheria inasemaje? Maana siku hizi unalala unaamka mtu amefungua bar hakuna wa kumgusa
 
Unaingie salon unakuta mziki mpaka wote unashindwa kusema naomba mpunguze mziki halafu unasubiri so called NEMC waje wawanyamazishe wakati na wao wananyoa humo humo
NEMC wanalaumiwa kwakuwa wanapewa taarifa wanazikalia kimya, wanapota mitaani wanaona hali halisi ilivyo hawachukui hatua
 
Mbaya zaidi wanasema muziki usizidi db 8, lakini hata wao wenyewe hawana sound meter sijui huyo mwenye bar ataipata wapi hiyo db 8
 
NEMC wanalaumiwa kwakuwa wanapewa taarifa wanazikalia kimya, wanapota mitaani wanaona hali halisi ilivyo hawachukui hatua

Hawana faida hao bora ingefutwa tu
Sioni kazi yao kabisa na serikali inawaangalia tu
Tuna watu wa hovyo sana na sisi wenyewe tunashindwa kukemea kwa virendo bali tunakubali yaendelee
 
Mkuu si rahisi kutaja kwa mfano hawa wanao hubiri na mispika mikubwaaaa, mziki kama wote masauti mpaka mwisho utawataja majina kweli watu wanatembea na midubwana wamejitwisha kichwani kelele zake sio za kawaida mkuu
Hawa wapo mitaani mchana kabisa. Mitaa ya Kariakoo ni maarufu. Nani anawapa vibali?
 
NEMC wanalaumiwa kwakuwa wanapewa taarifa wanazikalia kimya, wanapota mitaani wanaona hali halisi ilivyo hawachukui hatua
Watupe namba zinazopokelewa saa 24 na kufuatiliwa papo kwa papo.
 
Watupe namba zinazopokelewa saa 24 na kufuatiliwa papo kwa papo.
Huwezi kuamini na wao wanaishi kwenye mitaa yenye changamoto hizo ila hawajui nani wa kumpelekea malalamiko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…